Baadhi ya warembo wa Miss East Africa
wakiwa kambini hoteli ya Kunduchi jijini Dar leo
warembo wakiwa kambini
msosi time
Tiketi zaanza kuuzwa

KIINGILIO cha juu katika shindano la Miss East Africa kitakuwa sh 100,000 ambapo watakaolipa pia watapewa na chakula cha jioni.

Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, msemaji wa Miss East Africa, Petter Mwendapole alisema katika shindano hilo litakalofanyika Desemba 19 kwenye ukumbi wa Mlimani City, kiingilio cha chini kitakuwa sh 50,000.
“Kiingilio cha laki moja kitakuwa kwenda na chakula ambacho kitatolewa na kampuni ya Ako Catering Service,” alisema.

Alisema tiketi kwa ajili ya shindano hilo litakaloshirikisha nchi 10 zitaanza kuuzwa leo sehemu mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Baadhi ya sehemu ambazo tiketi hizo zitapatikana ni pamoja na Tina Maria Boutique, Engen Mbezi, Engen Ubungo, Engen Mbezi, Samaki Samaki Mlimani City, TCC Club Chang’ombe, Steers, Best Bite Namanga, Shear Illusion.
Tayari warembo kutoka Mauritius, Kenya, Djibouti, Somalia,Rwanda wameshawasili na wako kambini hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Miss East Africa inaandaliwa na Rena Events na kudhaminiwa na CMC Automobile, Kings and Queens Worldwide, New Habari (2006) Limited, East Africa Radio na Televisheni, DD Whole Sale.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pesa zinaenda kwa watoto yatima? Laki si Mchezo Jamani..... Kula tu na kukaa kwenye kiti kazi kwelikweli. Kimaro

    ReplyDelete
  2. safi sana huyu mtayarishaji wa hili shindano anaakili sana,kiingilio ni laki 1 kama huna baki nyumban manake sisi wengine tunataka kujinafas hatutak joto mara mojamoja sio mbaya unajua kiingilio cha elf 5 tano au kumi kumi siku hiz kimepitwa na wakat manake wataingia watu wote kuanzia vibaka mpaka mateja sasa ili kuchuja inabid iwe hivyo.

    ReplyDelete
  3. duu watoto wazur hau wangeweka kiingilio laki mbili kabisa

    ReplyDelete
  4. MI SILIPI LAKI MOJA KWENDA KUINGALIA MILUPO!

    ReplyDelete
  5. Let me see...aaaah nope ,can't pay that much for vinyago kama hao..wacha niweke hela Benki,kwasababu najua fika hizo pesa kufikishwa kwa walengwa ni mzozo..watu washazitolea mimacho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...