TIMU YA TAIFA YA BARA KILIMANJARO STARS IMETOLEWA KATIKA MASHINDANO YA CHALENJI MWAKA HUU JIJINI NAIROBI BAADA YA KUFUNGWA BAO 2-1 NA RWANDA KATIKA MCHEZO WA NUSU FAINALI. NA MCHEZO UMEISHA SEKUNDE CHACHE ZILIZOPITA....
FAINALI ITAKUWA JUMAPILI AMBAPO RWANDA WATAKIPIGA NA UGANDA AMBAO WAMEWATOA ZANZIBAR HEROES.
MSHINDI WA TATU ATAPATIKANA KWA MECHI KATI YA KILIMANJARO STARS NA ZANZIBAR HEROES
Aksante kwa taarifa. Ila mtoa habari nafikiri ni mtu wa Rwanda!! Any way, kombe mtalichukua Wanyarwanda maanake mtacheza wenyewe kwa wenyewe!!
ReplyDeleteSijui Kili Stars tusubiri kombe la nini tena!!
Ninaweza nikasema kwa jinsi mchezo nilivyouona vijana wamecheza vizuri sana ila tu bahati haikuwa yao. Kipindi cha pili chote walikuwa wako 10 na still wali-dominate mchezo. Bahati tu haikuwa upande wetu. Hongera kwa vijana, kilichobaki ni kuelekeza mashambulzi dhidi ya Znz kwa ajili ya nafasi ya 3.
ReplyDeleteTaifa Stars Wamecheza Vizuri. tatizo lina kuja Nizamu ya Mpira yule Juma Nyoso wasimuweke Tena na Maximo lini utajifunza na Makipa? muwekeni Kaseja.
ReplyDeleteMaximo tizama Rwanda walivyoshinda wakipata mpira wanauweka miguuni wanajuwa Mabeki wa Taifa stars nizamu Ziro wanakuja na nguvu miguuni Foul, Mafunzo yako yako wapi?
Mwisho Pale imekuwaje Kocha wa Rwanda katukana Ugomvi na Maximo?
Kina mGosi wanawekwa Baadae kabisa tushachoka sasa Timu ichanganywe Tutizame wa Visiwani waliofanya Vizuri na wa Taifa Stars iwe Timu Ya Tanzania Na Baazi wapya basi. Maximo kama hajafanya hivyo afukuzwe. Ndosi.
Michuzi Pole naona Umechanganyikiwa na Kuandika Rwanda Watakipiga na Rwanda. Maximo Njeeeeeeeee tushakuchoka Beki hakuna Nizamu na Kipa Mbovu anatetemeka. Timu Maximo anafanya kama Yake peke yake.
ReplyDeleteJe, hii ndo timu yenye nidhamu ya Maximo? Timu kila mechi unapata red card na yellow kibao za kipuuzi puuzi!!! Timu haina nidhamu, kwa maana hiyo basi naomba "watovu wa nidhamu" wote walotemwa timu ya taifa warudishwe , wajiunge na watovu wa nidhamu wenzao waendeleze libeneke.Tujue moja kuwa timu haina nidhamu basi, sio tunaambiwa hawa hawataitwa timu ya taifa ng'o sababu ya nidhamu wakati timu nzima ilobaki haina nidhamu...Maximo,,hatutaki kusikia ukitaja tena neno nidhamu, hiki kisingizio kimeexpire!!!Please!!
ReplyDeletenilishasema kama stazi haitabeba kikombe hiki basi MAXIMO ajikatae mwenyewe..
ReplyDeletenalala sasa hivi nategemea nikitoka tu kitandani kesho mungu akipenda nikute kichwa cha habari hapa kikisema
"BREAKING NEWS.......... MAXIMO ABWAGA MANYANGA STAZI"
Kazi yoyote unafanya valuation kwa mafanikio kwa hiyo mpirani mafanikio yake ni vikombe maximo umeshindwa kuleta vikombe anza mbele. Na Kikwete kama anazidi kumtetea basi tuwaachie timu wao wawili na hata mpirani tusiende. Mtu poor performer halafu analindwa.. kila siku timu inabadilishwa sasa kila siku antakuwa anajenga timu.. JK uwe serious .... yani kwenye Richmond unatetea wakosaji hatat kocha wa mpira unaona kazi kumfukuza badala yake unamtetea .. au na wewe ni poor performer kwa unatetea wenzanko .. yeah kuna hiyo tendence .. unakuwa unajiweka kwenye position yake na kufeel kama na wewe unavyolaumiwa.. wapenzi tuchukue hataua .. Maximo arudi nyumbani imetosha
ReplyDeleteKipindi starz inashinda ohhh sasa hivi hamna majina watoto wanagusa ngozi kinoma, mnafungwa Maximo ajui kazi anabadirisha kikosi kila mara. Jamaa ameshakuambieni anatafuta timu ya kudumu kwaiyo mwaacheni na anachofanya laa hamkubaliani na anachofanya basi muandame mpaka TTF mutake jamaa aachie ngazi, lakini maneno yenu yatakuwa bure. Kwani makocha wangapi wamekuja Tz ha2jaenda popote. Maximo ame2peleka CHAN na nusu twende Kombe la Africa kama 2ngemfunga Msumbiji au mmesahau? Mnapenda kushinda 2 mkubali na kufungwa pia. Yaani hamjui 2 au hamjajifunza kama sisi Wa Tz ni bado kisoka. Musimlaumu Maximo wachezaji ndio wanapaswa kuji22mua yaani kucheza kwa bidii. Maximo anafundisha 2 lakini ukiwa uwanjani mda wote unatakiwa u2mie akili yako. m2 anaesema Maximo aondoke aende akafundishe yeye au akatafute yeye Kocha, mimi sioni Maximo amefanya kazi mbaya Taifa Starz. Unapogewa shavu muoneshe Kocha mimi ninafaa na uliniacha bure ndio maana Kocha anabadirisha kikosi kila mara sababu ajapata wa2 wa kudumu.
ReplyDeleteNafikiri huyu Maximo safari imeiva ,mafanikio ya timu yoyote ni kuchukua kombe.Sasa huyu bwana inasemekana aliikuta timu mbovu, sasa miaka mingapi imepita timu bado vile vile anajidai anakazania nidhamu ,hiyo ndiyo timu yenye nidhamu kuliko yote . Maximo akubali kushindwa na ajiuzulu.
ReplyDeletenyie hamna heri mmeingia mashindano haya kuifunga zanzibar tu,haya basi na tuone jumamosi itakuaje!Bara hamna tim peke yenu,hebu angalieni visiwani,magazeti yote yanasifu kwa kandanda safi hata walipocheza na Bara,washabiki walishangiria znz,kwa mpira wa umakini haya basi na tupapatue ushindi watatu ambao lazima ubakie TANZANIA SAFARI HII WATU WAKITAKA WASITAKE,PIA TUACHE KULALAMIKA,MAXIMO ALIIPONDA ZNZ SASA JE ANSEMAJE?
ReplyDeleteKwa heri MAXIMOOOOOOOOOOOOOOOOO!
ReplyDeleteAibu tupu, huyo Maximo atolewe nduki anataka kuchezesha waafrika mchezo wa legelege kama Brazil.
ReplyDeleteTZ inataka makocha kutoka Ulaya,haswa uholanzi wanakuwa na mkocha maridadi kabisa...na pia ni vizuri katika kutengeneza upenyo wa kuingia ktk soka la ulaya...Kocha wa Brazil hafai ktk soka za afrika....
Haya mambo ya kusema Maximo aliiponda Znz ni kutafuta mtafaruku pasipo na mtafaruku. Maximo hakuitaja Znz kama timu ambayo anaona itafika mbali. Zanzibar imefika fainali???? Kwa hiyo kauli yake ni sahihi au sio sahihi?
ReplyDeleteNimesikitika kwamba mechi ambayo nilikuwa naombea iwe fainali imeishia kuwa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu. Hata hivyo nafarijika kwa sababu ina maana kwamba tukichanganya vipaji vya timu zetu mbili hizi tuna uwezo wa kutoa kitu kizuri zaidi.
Mungu ibariki Tanzania.
SOTE TUMEONA UKWELI NI KUWA WATANZANIA TUMEKULA HASARA MIYAKA YOTE TULIYOKUWA NAE HUYU MAKISIMO UKWELI HAKUNA TIMY PALE NI KIGENGE CHA WAHUNI KILE JANA ILIONYESHA WAZI WACHEZAJI HAWANA NIDHAMU YA MCHEZO SI DHANI KAMA KUNA MCHEZAJI ANASTAHILI KUITWA MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA HAWANA NIDHAMU KABISA MCHEZAJI ANAMKWATUWA MCHEZAJI WA ADUI HATA PASIPO NA MPIRA YALE NI MAMBO YAKIZAMANI HAKUKUWA NA TV WATU WANASAKA WACHEZAJI LAKINI KWA HALI ILE TUSITEGEMEE KUOPATA MCHEZAJI WA KIMATAIFA NANI ATACHUKUWA UWAZO ULE HALA HUYU MAKISOMO TUMUULIZE HASA IPI TIMU YA TAIFA AMESHINDWA KUUNDA TIMU YA TAIFA KUNA SIKU MTAMKUMBUKA MZIRAI SASA MNA MUONA KAMA ANA CHUKI BINAFSI SIKU ITAFIKA MTAMKUMBUKA WABONGO ACHENI KULAZA BONGO ZENU HUYO SI MWALIMU WA MPIRA HUYO NI KADA MUHAMASISHAJI NDICHO ALICHO FANIKIWA HAMAN KITU PALE BORA WAKATI WA JOEL BENDERA TULIKUWA NA TIMU IKIFAHAMIKA
ReplyDeleteMAXIMO!! alipotaka kuondoka ilikuwa imetosha, sasa amekuwa mdaku, mfitini, na mpenda mademu na ndio sababu ya kuwachukia baadhi ya wachezaji maana wanabanana humohumo, aaaondokeee kiasi chake kimetosha miaka mitatu hajapata timu kamili? Kila kukicha anabadilisha timu kama mashati!! Aliipandisha chati TZ kisoka kiasi sasa inashuka maana hawezi tena kuipandisha, ila sasa anabahatisha aende mbele, Makocha wanaotufaa ni wa ulaya si Brazil KACHEMSHA na pia ANADANGANYIKA, tuagane nae akaangalie ustaarabu mbele. DEFF
ReplyDeleteYULE KIPA MWENYE MIONDOKO YA KUDAKADAKA MMEONA ALICHOTUFANYIA???
ReplyDeletekawaida ya stars wakishakula ng'ombe kumaliza mkia ni ngumu sana usimba na uyanga mnajiona mnawezaaa sasa huko nje mnavurundaaa basi muwe mnacheza bongo tu nje msiende ni aibu tu haya sasa wenzenu ivory coast wanakuja kupiga tizi hm kwenu na nyinyi je mtaenda lini kupiga tizi kwenye maandalizi ya world cup?? kwani waweze wana nini hata nyinyi mshindwe mna nini??? kocha wa brazili mnae lakini mhhh!!!
ReplyDeleteMaximo aondoke tu, hajapandisha chati soka la Bongo hata kidogo. Enzi hizo Tanzania ilikuwa inalichukua kombo la challenge mara kwa mara, lakini Maximo anashindwa hata kuiwezesha timu kuchukua kombe la Challenge. Maximo aliikuta timu ya taifa ila ya kwanza kabisa ilikuwa nzuri, akaanza kuipangua sasa ndio kavuruga kila kitu. Haiingii akilini kusema bado anatafuta timu, huu ni uongo. Wachezaji wetu wana vipaji sawa na DRC, Msumbiji, Zambia na Angola. anachokosea kocha huyu ni kubahatisha kupanga wachezaji, anawapanga mid field wengi washambuliaji wachache, Mgosi anamuingiza mwishoni, hawezi kuusoma mchezo kisha akafanya mabadiliko yenye tija, aige mfano wa Sir alex furgason wa kuusoma mchezo na kuibadilisha timu. Mimi naona heri ya huyu kocha Hemed Morocco ameonesha ana uwezo wa kuwa kocha mazuri.
ReplyDeleteShida watz legelege sanaaaa, kamata taifa star yoote na Maximo wao piga keko kwa wiki tatu wajue nn maana ya uzalendo, na wajue hawapewi pesa ili kuuza sura!!!
ReplyDeleteWakati tunasema fulani hafai mlikuwa mnaona tunachuki. Asante Rwanda kwa kuthibitisha kwamba fulani ni mbovu.
ReplyDelete