Juma Nkamia a.k.a 'Kocha Mtangazaji' ambaye ni mtangazaji mwenye uzoefu na mvuto mkubwa katika fani hiyo sasa amejiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Washington Dc, akitokea TBC Tanzania.
Utamsikia Nkamia kwenye matangazo mbali mbali ya habari hadi michezo kutoka Washington,Dc kwa kupitia radio washirika Afrika Mashariki na kati ikiwa ni pamoja na Radio Free Afrika Mwanza, Citizen Radio Kenya au kwenye mtandao wao wa
Juma Nkamia, jina linalonikumbusha enzi zangu za kusikiliza kabumbu redioni kwenye kiredio changu mkulima baada ya kuanika betri juani mchana kutwa kusubiria saa kumi na nusu mpambano...
ReplyDeleteBila shaka ujio wako VOA utaongeza ubora wa matangazo ya VOA. Ni changamoto tosha kwa BBC, DW, NHK, CRI,Idhaa ya Iran nk.
Kazi njema Juma.
Kila la kheri katangaze mpira wa kina Beckam, Simba watamis mchango wako kwenye matangazo.
ReplyDeleteHalafu ivi Bin Sued Mwinyi nae yuko wapi?, Uncle J Nyaisanga je?
Hongera sana kaka, unastahili
ReplyDeleteMichu umenifurahisha sana na hiyo title ya habari..huyu jamaa binafsi huwa ananifurahisha sana kwa comment zake anapokuwa anatangaza, ingawa baadhi ya watu huwa wanamponda kuwa jamaa anapenda misifa. Kuna cartoonist alikuwa anamchora kila wiki kwenye gazeti kumzodoa lakini mwenyewe alichemsha ! Well big up Nkamia and wish you all the best in your new career, ukirudi huko uje na kitu kipya kama vile bro Tido Mhando tuendeleze nchi yetu.
ReplyDeleteTunasubiri Ligi kati ya BBC ulimwengu wa soka Vs VOA Michezo...patamu hapo.
ReplyDeleteHuyu bwana kaenda VOA sio kutafuta pesa ila alikuwa anakuwa frustrated pale TBC for nothing. Angekuwa anapata mshahara kama ule aliopewa Gerry Muro Juma najua hangekwenda Marekani. He loves the country, and he is also ready to serve it with dignity. TBC msipochunga mtampoteza kinara wenu mwingine SHABBAN KISU. Sababu mnazijua. shauri yenu.
ReplyDeleteShabban Kisu utanfuata rafiki yako Juma?? Nakusihi chonde chonde usiondoke japo nasikia wewe hapo TBC unapata manyanyaso fulani hivi.
ReplyDeleteSasa ubunge kule nyumbani Singida itakuwaje bro??
ReplyDeleteHongera kwake na kila la kheri, ila apunguze jazba na majigambo. Nakumbuka nilipokuwa naangalia alipokuwa aki-simamia matangazo ya TBC1 kwenye mashindano ya CHAN alikuwa akikasirika sana na anaonyesha waziwazi kwa watazamaji wapiga picha wanapochelewa kumuondoa kwenye screen anapokuwa amemaliza matangazo. Wenzio huwa wana-smile mpaka watolewe kwenye screen, sio kuwakasirikia na kuwakaripia wapiga picha.
ReplyDeleteHongera sana na all the best. Msalimie home girl Ndimmyake Mwakalyelye, mwambie huwa nafurahi sana ninaposikia wazungu anaowa-interview wanapojaribu ku-pronaunce jina lake, hakuna aliyewahi kupatia!.
ReplyDeleteNdugu yangu Juma Hongera sana kwa kazi yako mpya.
ReplyDeleteBora ameondoka manake alikuwa anaboa tu anapotangaza mpira kwa kuwalaumu waamuzi hasa pale timu yake ya simba inapofanya vibaya.
ReplyDeleteLingine anatakiwa aishape tone ya sauti yake inayotafsiriwa kama ni jazba hata ktk mazingira ya kawaida tu na vile vile awe anajitahidi kuacha kukunja sura anapokuwa kwenye runinga.
Juma Nkamia BBC London walikupa offer nzuri tu ukakimbia kurudi TZ for making excusess that you want to go home to look after your family, Je huko VOA DC Vipi utachemsha pia? les wait and see. Gluck buddy!
ReplyDeletewe anonym wa hapo juu..jambo usilolijua ni usika wa kiza! wacha porojo! give the facts and stop rumor mongering!!
ReplyDeleteHongera Juma Seleman Nkamia,ninachokimic ni sauti yako katika matangazo ya mechi za ligi kuu Tanzania,nakutakia maisha mema huko VOA,
ReplyDeleteSweetbert Rwabukambara.