Tanzania Professionals Network (TPN)
Nyumbani Ni Nyumbani 2009


Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo

1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini

5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi Wake

6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua Za Kuleta Mabadiliko Na kwa Namna Gani?

7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/

Siku na Muda:
Ijumaa; 18th December 2009; Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni

Mahali:
Golden Tulip Toure Drive, Msasani Peninsula

Washiriki:
Wanataaluma na Wasomi Wote Wazalendo Mnaombwa Kufika Bila Kukosa

Ada ya Ushiriki:
TZS 50,000 (Kwa ajili ya Ukumbi; Chakula; Tea na Snacks, PA, Documents nk)

Angalizo:
Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo Walioko Mikoani Wamewekewa Nafasi Zao na Watalipiwa Ada ya Ushiriki; Tuwasiliane. Huu si wakati wa Kulaumu. Kama Umeguswa naMada, usikose kuja Kutoa Mawazo yako.

Kujiandikisha na Maelezo Zaidi:
0715 740 047 ; president@tpn.co.tz; www.tpntz.org

Waandaaji: TPN – Costech - TSN– OUT – UDSM - Serikali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wanataaluma = academicians

    ReplyDelete
  2. No. Wanataaluma=Professionals...

    ReplyDelete
  3. TPN,

    Ukichukulia kongamano hili halina sitting allowance, (na badala yake lina ada ya ushiriki) hiyo siku mliyochagua haifai kabisa.

    Ni siku ya kazi. Na ni siku ya swala ya Ijumaa.

    Mngeweka Jumamosi ingekuwa poa zaidi.

    ReplyDelete
  4. wanataaluma waishio nje ya nchi au walio nje ya mchi watashiriki vipi?Hebu mwanataaluma tufafanulie kidogo.!!!

    ReplyDelete
  5. Tanzania msomi ni mtu mmoja tu, naye ni Dr. US Blogger wa Oxford, wengine ni wababaishaji tu.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  6. TPN leteni mtu aje kurekodi proceedings za mkutano huo, Halafu tengenezeni Videos/DVDs ambazo mtawauzia wale ambao hawataweza kushiriki hasa kwa wale ambao wako nje ya nchi.

    Mdau

    Mtaalam Mzalendo
    (Nitahudhuria Kikao Bila Kukosa)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...