mambo ya kuchonga chonga pia
yatakuwepo ktk blog ya culinary chamber
Asalaam alaykhum ankal Michuzi,
Wajina, blog yetu ya CULINARY CHAMBER itazaliwa rasmi tar 1/1/2010. Hivi sasa article za awali zinamaliziwa pamoja na picha baadhi. Imani yangu ni kuwa wataalamu wa fani hii watachangia kwa moyo mmoja ili wadau wote wapenda misosi waweze kufaidika kwa utaalamu wa mapishi mbali mbali yatakayoporomoshwa. Nnaimani ushirikiano utakua mzuri ili tuboreshe blog yetu. Mwanzo mgumu ila penye nia pana njia tutafika tu kwa juhudi na uchakarikaji.
Pokea picha hizo ambazo nilibahatika kushiriki pia mashindano ya finger foods ambayo lengo haikua kupata mshindi ila ni kubadilishana ujuzi toka kwenye vyuo mbali mbali vya culinary duniani vyenye ushirikiano wa pamoja toka nchi za Croatia, USA, Uk, France, Italy, Malaysia , Indonesia, India, Korea, China, Singapole, German, Austria, Swistzerland, Netherland, spain na Belgium.
Wajina, blog yetu ya CULINARY CHAMBER itazaliwa rasmi tar 1/1/2010. Hivi sasa article za awali zinamaliziwa pamoja na picha baadhi. Imani yangu ni kuwa wataalamu wa fani hii watachangia kwa moyo mmoja ili wadau wote wapenda misosi waweze kufaidika kwa utaalamu wa mapishi mbali mbali yatakayoporomoshwa. Nnaimani ushirikiano utakua mzuri ili tuboreshe blog yetu. Mwanzo mgumu ila penye nia pana njia tutafika tu kwa juhudi na uchakarikaji.
Pokea picha hizo ambazo nilibahatika kushiriki pia mashindano ya finger foods ambayo lengo haikua kupata mshindi ila ni kubadilishana ujuzi toka kwenye vyuo mbali mbali vya culinary duniani vyenye ushirikiano wa pamoja toka nchi za Croatia, USA, Uk, France, Italy, Malaysia , Indonesia, India, Korea, China, Singapole, German, Austria, Swistzerland, Netherland, spain na Belgium.
Picha za vyakula na habari zaidi watazipata ktk blog ya Culinary Chamber.
Baada ya mashindano hayo jioni ilikua ni bonge la party wanafunzi waliochukua kozi ya general hotel management na mambo ya matukio walitoa perfomance safi yenye ladha ya mataifa yao ilikua super sana ankal michuzi.
Ila kubwa kuliko yote ni pale nilipooona bendera ya taifa langu imepanda juu kama heshima ya mshiriki toka Tanzania. ohhhhhh.... nilihisi machozi kunidondoka kwa furaha.
Ndugu zangu nawaomba sana sana tushirikiane. Shule hii ni bure wala hakuna gharama yeyote kwa hiyo yeyote mwenye ujuzi atoe, msijifiche. Huu ndio wakati muafaka wa kubadilishana utaalamu kwani hakuna anaejua zaidi. Wote tunajua kiasi kwa hiyo tukichanganya maarifa inakua safi mambo yanakamilika na kunoga au vipi kaka misupu? hahahahhahaa
Ndugu zangu nawaomba sana sana tushirikiane. Shule hii ni bure wala hakuna gharama yeyote kwa hiyo yeyote mwenye ujuzi atoe, msijifiche. Huu ndio wakati muafaka wa kubadilishana utaalamu kwani hakuna anaejua zaidi. Wote tunajua kiasi kwa hiyo tukichanganya maarifa inakua safi mambo yanakamilika na kunoga au vipi kaka misupu? hahahahhahaa
HAPPY NEW YEAR TO ALL !
nashukuru sana kwa maoni yenu yote
nayaheshimu sana mungu awabariki.
Chef Issa
Chef Issa
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletenaona libendera letu ndo libaya kuliko zote hilo rangi jeusi hapo center limeharibu sana lingewekwa kimtindo kha!
ReplyDeletei love culinary art,hope utatuweka mambo kibao na aina za vifaa tunavyoweza kutumia kuchongachonga ili twende sambamba na wewe...
ReplyDeleteMimi natafuta mpishi wa familia home, naona wewe unafaa. Vipi unataka hii kazi?
ReplyDeleteNimekuwa na wapishi wengi lakini bado sijapata wa kuridhisha. Labda na wewe uje nikufanyie test angalau kwa miezi sita.
Malipo ni mazuri, hela sio tatizo. Tatizo ni mlo mzuri.
Sasa hii issue ya execution ina uhusiano gani na habari ya mapishi???
ReplyDeletekaka misupu inamaana hayo mamboga mboga ndio yamechongwa hivyo duh kila mtu na fani yake aisee si mchuzi ni fani jamani poa tupo pamoja kijana
ReplyDeleteblog itazaliwa muda muafaka safi sana kijana unajipanga kama obama vile au JK mambo tratiiiiiiiiiiiibu safi mapaka tutafika ziba masikio majungu yasikuumize chapa kazi juhudi ya kwako mola ndio kakuwezesha jitume mdogo wangu
ReplyDeletesasa hapa inapendeza maana tunapata blog tofauti kabisa na habari tofauti kabisa michuzi big up kwa kumpa nafasi huyu kijana tusingemfahamu na tusinge ijua blog yake itatufaa sana tu na huu ndio usomi bora ulichokipata unashea na wenzio mdau SAYANSI
ReplyDeleteBlog itakua online ndio lakini sio wa tanzania wote wanatumia internet so nasikitika wengi watakosa utamu huu duh basi bwana atakae bahatika abahatike ila ningeshaur recipe ziwe zinakaa wiki nzima ili watu wote wapate nafasi ya kusoma usibadilishe badilishe haraka wengine hawataweza kusoma maana hatuna internet home mpka tuende cafe na kila siku hatutaweza kuingia cafe litilie umakini ombi hili pls pls Mdau Chef arusha
ReplyDeleteacha upuuzi wewe geuza coin kwa upande wapili kama nikakaako huyo au babaako unge unga mokno kuuwawa kwake?hio ni kinyume cha haki za kibinaadamu,kuuana sio dawa hasa kwa kesi kama hizo,siungi mkono hoja napinga ka asilimia mia adhabu ya kifo ifutwe na isirudishwe nchini mwetu.zitafutwe adhabu nyengine vifungo vya muda mrefu kwa tuhuma nzito kama mauaji ya kukusudia,ufisadi a mali za umma nk.mdau greece
ReplyDeleteKaka Michuzi kwanza mi namuunga mkono huyo jamaa hapo juu, kilichobaki ndo hicho tu Bongo, km ilivyokuwa Rwanda watu sasa hivi wanaheshimiana.
ReplyDeleteBack to the topic,
Kaka Isa mi nitakuwa mdau namba moja wa blog yako, japo elimu yangu ya cookery iliishia form 4. ila cooking is my passion. utupatie recipe zinazopatikana bongo au kwa kiswahili. naisubiria blog yetu kwa hamu.
Mungu akubariki.
Mdada Bongo
Chef Issa, chunga sana dhidi ya vishavu ndugu yangu, manake mambo ya jikoni haya usipokuwa makini ...
ReplyDeletekaka misupu hayo maoni ya kunyongana yatoe hapa sio sehemu yake yaweke kwenye front page watu waone hapa unaharibu kabisa utamu wa chefu wetu issa pls itoe bwana pls pls itoe hiyo mada hapa unamchafulia kijana Mdau mpenda kula
ReplyDeleteSasa wadau wa secta ya mahotel kijana anaanzisha blog yake nyie ndio watu wakumuunga mikono na migiuu hii ndio sehemu pekee mtakaoweza kujimwaga na kutoa taaluma yenu madukuduku na kero jinazojiri ktk sehemu zenu za kazi chef issa usibague maoni ya watu weka hewani kila kitu umeamua kujitosa basi jitose kama wajina lako michuzi HONGERA KIJANA ISSA SUPER misupu hiyo mada ya kuchinja itoe hapa bwana
ReplyDeletesasa huu ndio utamu kozi ya bure hiyo wadau tumekombolewa na kakijana ketu kazuri jamani duh unakuja bongo au utamuvuzisha mavitu huko huko uliko duh tunakupendaga sana kachef ketu kazalendo uwiiiiiiiii NGOSHA ORIGINAL
ReplyDeletetuna ankal michuzi original na ankal issa misosi duh hapa ni full blog ya kufa mtu michuzi kijana ulimfahamu vipi huyu? mpe mautaalamu ya blog ili blog yake iwe bomba kama yako mzee
ReplyDeleteduh hilo la kijani ni litango? au lirungu? duh mamboga ya ulaya hayo wajameni duh na kale kandegeeee hiii wajameni duh! kakuchonga au liveeee? hii wajameni yaani nimetupendega sana huto tuulaamu wajameni yeeeeeeee kakijana kamefanyaga mambo kabisa hiiii sasa tungoje mambo live tuone hiiiiii wajameni NGOSHA ORIGINAL
ReplyDeleteHizo finger foods ulivyozidecorate hapo hata kwa mwanangu asiyependa mboga za majani mbona angekula. Basi ukianzisha libene lako uwe unatuwekea stage by stage jinsi ya kukata hayo matunda...Mimi nimpenzi sana wa mabo yangu...actually nina homebase catering business na food network TV is one of my favorates. Lakini kupambiza hivyo sifanyi kwa mtajii huu wataniua...ila ningependa kujua kufanya hivyo kwa faida yangu..HONGERA SANA kaza buti polepole na wewew utaown restaurant yako au kesho utakua kama kina Wolfgang Puck, Bobby Flay, Nigella, Giada na Rachel Ray lakini usije ukawa mkali kama hells kitchen chef ramsey (sp) ...Good luck in all you do.
ReplyDeleteNaona sasa ni wakati wa muvi la Kurinali Part4. Tumeshapata series kibao hapa za m-BBA; Binti Machozi; Nabii wa Shirati; MissTz,Tigo, ...wa Voda n.k.
ReplyDeleteDogo wewe teremsha hilo chemba la maakuli kwa kupunguza muda wa kutuelezea historia ya maisha yako.
MIMI NAKWENDA KWA MANDONDO TANGA, WEWE KIJANA NI HATARI KWA KAZI YANGU.
ReplyDeleteNashukuru sana ndugu zangu pamoja na wadau wote wa blog ya jamii, michango yenu na maoni kwa ujumla sasa kazi kwenu kuendeleza kutoa maoni ktk libeneke hili jipya la mambo ya maakuli michango na mawazo yenu yatasaidia sana kuboresha na kila mmoja wetu afaidike na kitakachofundishwa kama nilivyoahidi libeneke litakua live siku ya tar 1/1/2010 hapaha kwa ankal. nawatakia kheri ya mwaka mpya tukutane live ktk libeneke la maakuli. Ankal akhsante sana Chef Issa
ReplyDelete