JESHI la polisi nchini kwa kushirikiana na ofisi za Interpol Kanda ya Kusini mwa Afrika(SARPCCO) wameendesha operesheni maalum ya siku mbili inayojulikana kama “NAMUTUNI” nchi nzima na kukamata watuhumiwa 110, na vielelezo mbalimbali yakiwemo magari 54 yaliyoibwa nchi tofauti.

Polisi pia wamekamata pikipiki sita, nne kati ya hizo ziliibwa nchini Kenya.

Magari 48 kati ya waliyokamatwa yaliibwa nchi mbalimbali ikiwemo matatu Afrika Kusini, 38 Japan, magari manne England, na moja moja katika nchi za Jamuhuri ya Dominic, Australia, na Kenya.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, ameyasema hayo katika taarifa iliyosomwa na Kamishna wa polisi, Dominic Hayuma wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Amesema, operesheni hiyo ilifanyika Novemba 23 hadi 25 na ilifanikisha kukamata dawa za kulevya zikiwemo kete 28 za Heroine, kilo 608 za mirungi, ekari 6 na kilogramu 801,335 za bangi, na misokoto 40 ya bangi.

“Pia tulikamata silaha mbalimbali zikiwemo bastola mbili, gobore moja, mabomu mawili ya kutupa kwa mkono, magazine 11, SMG nne na risasi zake 607 pamoja na wahamiaji haramu 25 kutoka nchi za Ethiopia, Burundi, Marekani, Jamaica na DRC” amesema Manumba katika taarifa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. naona hizi phD za wizi bongo zinafanya kazi yake lol! hadi mnaiba hadi gari huko autralia kuingiza nchini kweli mna kasi mpya na ari mpya

    ReplyDelete
  2. Haya waungwana mnaonunua magari ya bei rahisi kisa limetoka UK nadhani fikirini mara mbili mnaweza kuchukua mkenge ukakosa hela na gari. Watanzania tuna tamaa ya magari expensive wakati pesa hatuna!!!!

    ReplyDelete
  3. magari mnaiba nyinyi wa ughaibuni mnakuja kutuuzia huku bongo

    ReplyDelete
  4. ebwanaaaeee...
    yani wamekamata SMG 4 na risasi 607,magazine,pamoja na MABOMU mawili?? Duh! hii mbona ni soo,hata kujilinda sio kihivyo,ni vita kabisa hiyo si masihala ati!
    Kazi bado ipo.

    Potz.
    (Mashariki ya mbali)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...