Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi hapa nchini,
kesho Jumatatu Desemba, 14, watakutana mjini Dodoma kupanga mikakati mipya itakayofanikisha uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani utakaofanyika baadaye mwakani.

Mkuu wa Sera na Utafiti wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msadizi Mwandamizi Paul Ntobi, amesema leo mjini hapa kuwa mafunzo hayo yatafunguliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame.

Amesema kuwa mafunzo hayo pia yatawashirikisha Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia wa mikoa, Wakuu wa Upelelezi na Wakuu wa Operesheni maalum kutoka kila mkoa hapa nchini.

Kamanda Ntobi amesema mafunzo kama hayo pia yaliwahi kutolewa kwa Wakuu wa Polisi wa walaya na wa Upelelezi wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.

Amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, watahudhuria kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yatakayofanyika mjini Dodoma.

Tayari washiriki wote wa mafunzo hayo kutoka bara na Visiwani wameshawasili mjini Dodoma kwa ajili ya mafunzo hayo.

Vyama 18 vya Siasa vyenye usajili wa kudumu hapa nchini, vinatarajiwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho huku baadhi ya vyama hivyo vikiwa na wagombea wa viti vya urais na vingine vikiwa na Wagombea wa Viti vya Ubunge na Udiwani pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Waganga wakuu wa Mikoa yote hasa kule Zanzibar, nao pia wangekutana wajipange kukabilianana watakao vunjwa vunjwa viungo vya mwili na hao Polisi wetu wasio na uelewa wa ma suala ya haki za binadamu:))

    ReplyDelete
  2. Makamanda hao wangeshiriki pia kwenye tamasha la HAKI ZA BINADAMU, kwani wangeelewa utu ni nini pia DEMOKRASIA.
    Pili,hao makamada sioni kama wanahaja ya kuudhuria huo mkutano,mimi nadhani wale askari wanao kaa kambi za mabati wenye hasira kama nyuki wanaofanya kazi kutumia ugali(misuli) bila akili ndo walipaswa kuhudhulia woote kwa wingi wao.Kwani kamanda hua hapigi watu virungu ni wale wanaopewa posho ya kutuliza ghasia kwa kuua na kuvunja watu viungo.
    Mwisho wangeagiza madaktari wa mifupa,mishipa ya fahamu kwa wingi ili kukabiliana na tatizo sugu la kikatili kila wakati wa chaguzi kuu nchini,waombe kule Ujerumani kwenye mbio za`magari pia kule ohio Dytona kwenye mbio za magari wapo wengi tu.

    ReplyDelete
  3. Mimi naona Jaji makame atolewe tume ya uchaguzi apewe Tendwa wa usajili wa vyama vya siasa.Tizama Tendwa tangu achukuwe nafasi hiyo kasajili vyama vingi tu vya siasa Tofauti na George Liundi.Pia kukubali waziwazi swala la mgombe huru lililogombewa na rev.Mtikila for yearsbila mafanikio licha ya kushinda kesi mahakam kuu,ni dalili nzuri za mtu kukua ki-demokrasia.Sishabikii utitiri wa vyama ila utaona kuna haki ya kila mtanzania kupewa anachotaka kwa mujibu wa katiba ya nchi.Sasa basi Sioni kwanini Jaji Lewis makame akae kwenye Tume ya ucaguzi indefinately! WE NEED CHANGE, and wE NEET IT NOW!

    ReplyDelete
  4. huyohuyo Paul ntobi amekuwa kada mkuu wa c c m alipokuwa RPC mara leo kuna jipya gani atawaambia zaidi ya kulazimisha matokeo?ila nae hajiongezi aliahidiwa u IGP wamemwaga na bado ananyuka debe umri unaenda kaka kustaafy iz coming,mie nadhani wajifunze tu jinsi ya kufungua kampuni zao za ulinzi wakistaafu maana huwa hawapewi vyoe vya siasa baadae kama akina lt makamba,capt makongongoro nyerere,capt john komba,capt mkuchila na ma luteni na kibao JIFUNZENI

    ReplyDelete
  5. pia lingetengenezwa TAMASHA lingine kwa ajili ya MATRAFIC wote wafundishwe kuwa RUSHWA NI ADUI WA HAKI.

    ReplyDelete
  6. lol....

    kwi kwi kwi

    ReplyDelete
  7. YALE MAONI YA WAGOMBEA WATARAJIWA WA UBUNGE KUPITIA CCM WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI KUDHIBITI UPINZANI MBONA HAUKUYAWEKA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...