Aliyetuna kwa majigambo na tasamu la mbali ni mdau John Choma ambaye juzi kala nondozzz ya LLB kwenye International laws (Masters Degree in International Laws) chuo kikuu cha LEEDS University. Pili shoto kaka Silver Ambokile afisa wa ubalozi U.K aliyekuja hapa LEEDS hususani kwa kumpongeza kaka Choma. wengine ni wahitumu wengine katika kitivo cha sheria kutoka nnchi mbali mbali.Tunampongeza sana kaka yetu John Choma na kumtaka mafanikio hayo akayatafsli kwa vitendo pale wizara ya mambo ya ndani
Tunakushuru Michuzi na tunashukuru globo yetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. LLB kumbe kwa kiswahili ndiyo degree ya Uzamili(Masters of Law?) kama LLB ni masters basi LLM inaitwaje?

    Tuwe makini jamani tunapotuma habari kwenye glob yetu ya jamii;unaweza potosha wengi kuwa LLB na wala sio LLM ni masters degree in Law!

    ReplyDelete
  2. hivi master in laws pia inaitwa LLB?

    hongera Mr John Taifa linahitaji wataalam wengi tu wa sheria ili haki ipatikane kwa uhalali na urahisi.

    ReplyDelete
  3. LLB ni first degree in laws nadhani mwandishi wa hiyo thread amekosea au hajui na kama hajui basi awe anauliza kabla ya kuandika.

    ReplyDelete
  4. So confusing ..LLB mara LLM in international laws hee.

    ReplyDelete
  5. Jamani let me put the house in order. LL.B. is the award of the degree of Bachelor of Laws (Shahada ya Sheria). LL.B ni kifupi cha neno la kilatini linalomaanisha ‘Legum Beccalaureus’.

    LL.M. pia ni kifupi cha neno la Latin linalomaanisha ‘Legum Magister’ yaani Master of Laws (Shahada ya Uzamili ya Sheria)

    Pia kuna LL.D. ambalo humaanisha ‘Legum Doctor’ ikimaanisha Doctor of Laws. Shahada ya Udaktari wa Sheria. Kwa ngazi ya udaktari wapo pia wanaopata Ph.D ambayo huitwa Shahada ya Uzamivu, na wengine hupata S.J.D. au D.C.L.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli jamaa aliyetuma taarifa hii kwenye blog amekosea kwa usahihi Mr john amepata LLM in International Law kutoka Leeds University Leeds UK na sio LLB. Hivyo tafadhali kosa Lirekebishwe ili kutoa taarifa sahihi

    ReplyDelete
  7. MZEE NAONA MAMBO SAFI SANAAAA,SASA VICTORIA PUB TUNAKUTANA LINI ILI VIJANA WAKO WA LEEDS TUKUPE ZA MWISHO MWISHO.HONGERA SANA BONGO WATATIA ADABU

    ReplyDelete
  8. WITH GREAT HOHOUR, I EXTEND MY EARNESTLY THANX FOR THOSE NOTED AND WITH GOOD BLESSED HEART COMMENTED BLANTANTLY ON MY MISTAKES BETWEEN (B & M) TO FORM LLM, I AM SOORY, IT WAS DUE TO (TYPING ERROR). THANK YOU AGAIN
    GOD BLESS YOU ALL

    ReplyDelete
  9. sasa nyie umu kama annon mmoja eshatoa ufafanuzi wengine mna-parade nini sasa???vishankupe nyi

    tumeelewa sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...