Mwenyekiti wa wabunge wanawake wa nchi za
Jumuiya ya madola Mh. Anna Abdallah (shoto)
wakati wa mkutano wa jumuiya hiyo huko Arusha


MBUNGE wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM) ameteuliwa kupokea nishani ya Kitaifa ya Uongozi inayotolewa na Afrika Kusini. Atakabidhiwa nishani hiyo ijulikanayo kama Order of the Grand Companions of O.R. Tambo, Silver.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ndiye atakayemvisha nishani hiyo ya juu nchini humo; kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam.

Ilieleza kuwa barua ya uteuzi inaonesha kwamba hafla ya kutunukiwa tuzo itafanyika leo katika Ikulu ya Afrika Kusini mjini Pretoria. Mbunge huyo ameondoka nchini jana kwenda Afrika Kusini kupokea nishani hiyo.

Katika msafara wake, Mbunge huyo aliyewahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT), atafuatana na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo (CCM) na maofisa wawili wa Bunge, Justina Shauri na Ernest Zulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mwenyekiti, Huyu wa kati ni Mzee nani vile?

    ReplyDelete
  2. HUYU ZUMA SI YULE ANAYEPENDA KUOA WANAWAKE WENGI? MIMI SIMUAMINI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...