Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania ( TBF), ambao uongozi wake uliingia madarakani Octoba, 2005, limepanga kuitisha Mkutano wake Mkuu wa Uchaguzi tarehe 19, Desemba, 2009 mjini Dar es Salaam
Nafasi zitakazogombewa ni kama ifuatavyo:
Rais
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu
Katibu Mkuu Msaidizi
Mweka Hazina
Kamishna wa Mipango na Maendeleo
Kamishna wa Watoto
Kamishna wa Wanawake
Kamishna wa Walemavu
Kamishna wa Ufundi na Mashindano
Kamishna wa Waamuzi
Kamishna wa Makocha
Kamishna wa Tiba
Nafasi zitakazogombewa ni kama ifuatavyo:
Rais
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu
Katibu Mkuu Msaidizi
Mweka Hazina
Kamishna wa Mipango na Maendeleo
Kamishna wa Watoto
Kamishna wa Wanawake
Kamishna wa Walemavu
Kamishna wa Ufundi na Mashindano
Kamishna wa Waamuzi
Kamishna wa Makocha
Kamishna wa Tiba
Baraza la michezo la Taifa ambalo ndio wasimamizi wa uchaguzi huu wamekwisha tangaza na kutoa fomu kwa waombaji. Mkoa wako utawakilishwa na wajumbe halali waliochaguliwa katika uchaguzi wenu ambao ni Mwenyekiti, Katibu na mwakilishi wa Wachezaji. Mkoa wako unatakiwa kuchangia gharama za usafiri kwa asilimia 25 tu.
Hivyo wajumbe wote watarejeshewa gharama zao za usafiri kwa asilimia 75 baada ya kuonyesh risiti halali ya usafiri. Aidha wajumbe watalipwa posho ya siku mbili ambayo itajumuisha malazi na chakula kwa kiwango cha Shs 30,000 kwa siku.
TBF inawakumbusha viongozi wa mikoa kuleta taarifa zao za utendaji wa Vyama vya Mikoa yao wakati wa Uchaguzi Mkuu pamoja na kukumbushwa kuwa Ada ya uanachama wa TBF ya Shs 30,000 itatakiwa ilipwe ili kuwa hai katika Shirikisho.
Mkutano utafanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru (uwanja wa taifa wa zamani) kuanzia saa 3.00 kamili asubuhi.
Nawatakia maandalizi mema kuelekea Mkutano Mkuu
Nawatakia maandalizi mema kuelekea Mkutano Mkuu
Lawrence Gideon Cheyo
KATIBU MKUU-TBF
KATIBU MKUU-TBF
Viongozi washawazidi waongozwa,kazi kwelikweli.
ReplyDelete