Na Anna Nkinda – Maelezo
Jeshi la Polisi Mkoani Mara linafanya operasheni maalum katika wilaya ya Serengeti kwa ajili ya kumkamata mtu ambaye amewaua watu wanne na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi.
Hayo yamesemwa jana na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Robert Boaz wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu.
Kamanda Boaz amesema kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji vya Gesarya, Rung'abure na Msati vilivyopo katika kata ya Rung'abure na Kibanchebanche Tarafa ya Ikorongo ambako mauaji hayo yametokea wanafanya msako huo pamoja na kuimarisha hali ya usalama katika wilaya hiyo hadi watakapomkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Akielezea kuhusu mauaji hayo ambayo yametokea kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 14 na 15 mwezi huu ACP Boaz amesema kuwa muuaji alikuwa anatembea barabarani katika maeneo ambayo yapo mbali na makazi ya watu na kumshambulia kila aliyekuwa anakutana naye na baada ya mashambulizi hayo alikuwa anatoweka bila kuchukua mali yoyote ya marehemu ama majeruhi.
"Tarehe 14 mwezi huu majira ya saa mbili za usiku katika kijiji cha Gesarya mtu huyo alimpiga risasi mbili kifuani Samson Chacha mwenye umri wa miaka 48 ambaye alifariki Dunia", alisema.
Majira ya saa mbili na nusu usiku muuaji huyo akiwa katika kitongoji cha Nyamase kijiji cha Gesarya alikutana na Marwa Mwita mwenye umri wa miaka 42 na kumshambulia kwa risasi kwenye mkono wa kulia, majeruhi amelazwa katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza ambapo hali yake inaendelea vizuri.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kufanya mauaji hayo muuaji huyo alihamia katika maeneo ya kijiji cha jirani cha Rung'abure kilichopo katika kata ya Rung'abure ambapo majira ya saa tatu za usiku alikutana njiani na Beneth Wambura mwenye umri wa miaka 48 na kumpiga risasi ya kifuani na kusababisha kifo chake.
Siku iliyofuata ya tarehe 15 majira ya tatu usiku muuaji akiwa katika kijiji cha Msati kata ya Kibanchebanche alimpiga risasi mgongoni Michael Marwa mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Nyarukongo na kusababisha kifo chake.
Aidha katika eneo hilo hilo alimjeruhi kwa risasi Samweli Wambura mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Kibanchebanche ambaye alifariki wakati anapata matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Serengeti.
Kamanda Boaz alisema, "Mpaka sasa muuaji huyu hayatambuliwa na wala nia ya kutekeleza mauaji hayo bado haijajulikana lakini uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa bunduki aliyokuwa anaitumia inatumia risasi za kivita zinazotumika katika bunduki aina ya SAR au SMG".
ACP Boaz alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtu huyo wajitokeze na kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali katika maeneo yao ama kwa viongozi wa Polisi ili mtu huyo aweze kukamatwa.
"Ninaamini Askari wetu kwa kushirikianna wananchi wa vijiji husika wataweza kumkamata mtuhumiwa ambaye atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani", alisema ACP Boaz.

Du poleni sana ndugu zetu wa maeneo hayo huyu ni Serial killer hawa watu hatari sana anastahili kunyongwa
ReplyDeleteuwezekano wa kuwa ni serial killer ni mdogo sana japo anaweza kuwa.
ReplyDeletehuyu possibility kubwa ni kwamba amepata matatizo ya ubongo na hivyo ni hatari sana kwa jamii.ndo maana huwa nasisitiza kwamba watanzania wanatambia mbaya wanaposikia mlipuko badala ya kukimbia mbali wanakimbia kwenda kutazama,je hii ingetokea wakaenda kutazama unategemea nini kama sio ingekuwa balaa?
jeshi la polisi inabidi litumie uwezo wake wote na vifaa vyake vyote ku-mlocate na kumkamata huyu kabla hajaleta madhara zaidi,na kama hawawezi bora waombe msaada ktk vikosi vya karibu vya TPDF.nayafahamu maeneo hayo vizuri sana .poleni muliofikwa na tukio hili.