
Kutoka shoto ni Tresor Mputu,
Samuel Eto'o, Michael Essein, Yaya Toure na Didier Drogba.
Wachezaji watano wametajwa kugombea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anayetambuliwa na BBC mwaka 2009.
Waliotajwa ni: Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast), Michael Essien (Chelsea na Ghana), Samuel Eto'o (Inter Milan na Cameroon), Tresor Mputu Mabi (TP Mazembe na DR Congo) na Yaya Toure (Barcelona na Ivory Coast).
BOFYA HAPA uweze kupiga kura kwa njia ya wavuti
Ama kwa simu na Namba ya kutuma ujumbe au SMS ni:
Ama kwa simu na Namba ya kutuma ujumbe au SMS ni:
+447786 200 070
ama
+447786 200 070
( kwa wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili
ya BBC, hii ni tofauti na namba ya kawaida).
Unaweza kumpigia kura mchezaji wa chaguo lako mpaka tarehe 4 Januari na mshindi atatangazwa siku nne baadaye, Januari 8 huko Angola wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Tuzo hiyo ya hadhi kubwa ndiyo pekee ya aina yake kutolewa kutokana na idadi ya kura zinazopigwa na mashabiki wa soka. Mshindi wa mwaka jana alikuwa Mohamed Aboutrika wa Al Ahly na Misri, aliyeisadia nchi yake kutetea kikombe cha kombe la mataifa ya Afrika na kuiwezesha timu yake kuchukua kombe la ligi ya vilabu bingwa Afrika.
Waliowahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika:
mwaka 2008 - Mohamed Aboutrika
mwaka 2007 - Emmanuel Adebayor
mwaka 2006 - Michael Essien
mwaka 2005 - Mohamed Barakat,
mwaka 2004 - Jay-Jay Okocha
mwaka 2003 - Jay-Jay Okocha
mwaka 2002 - El Hadji Diouf,
mwaka 2001 - Sammy Kuffour
mwaka 2000 - Patrick Mboma
www.BBCSWAHILI.com
Eto'o the king,
ReplyDeleteUCL,LA LIGA,KING.. vinajieleza
Waweke Mputu sababu yupo ndani ya Africa tushachoka kuona mchezaji bora wa Africa anachezea Ulaya, Sawa na wachezaji wengi Bora wa Ulaya wanatokea Amerika ya Kusini. kuwe na Lazima awe anchezea mulemule Aboutrika na Mputu ndio wlaitakiwa wapate au kama ndio hivi ni Drogba japo mie ni Liverpool. Hakuna Striker kama Drogba duniani sasa hivi.
ReplyDeleteOf the list mentioned, one player stands out: Didier Drogba. He is outstanding and at the top of his form. I will be waiting to see who will FIFA pick as the World's best player of the year, next year. I hope racism won't feature in selecting the best player of the world, let alone Africa.
ReplyDeleteTunapenda blog yako kusoma..lakini kinachoshangaza Timu yetu ya tanzania
ReplyDeleteHimecheza juzi na leo..lakini sijaona habari yoyote hile..mpka hivi sasa huku ni saa 19:49 nadhani huko nyumbani ni saa 21:49...lakini
hakuna chochote..AU WATANZANIA SIKU HIZI WANAAFUATILIA LIGI YA ENGLAND TU??
Tuwe wazalendo kidogo wana blogg
baada kuacha utoto pembeni na maringo hatimaye sasa drogba yuko tayari kuchukua hii tuzo mwaka huu.
ReplyDeleteTrepor Mputu na Etoo ndiyo waingie kwenye kupigiwa kura kwa sababu hizi 2
ReplyDeleteKwanza Etoo bao lake ndiyo liliashiria safari ya Man U kwenye kombe la club bingwa ya Ulaya na Trepor Mputu alitoa sana mchango na mwenzanke Kuyindula kutwaa ubingwa wa Afrika!Hata Keita na Yaya nao walijitahidi lkn mchango wao ni limited kulinganisha na akina Etoo!
Drogba yeye hana alililofanya mwaka jana la kustahili hata awemo kwenye kinyang'anyiro hiki!
Essien kiboko ya wote hao!
ReplyDeleteESSIEN THE BULLDOZER, THE MIDFIELD POWERHOUSE, ROHO YA PAKA, A REAL DEAL. KAMA CHELSEA WALIWAHI KUSAJILI MCHEZAJI MZURI, BASI WALISAJILI ESSIEN!
ReplyDeleteMbona wachezaji wa Tanzania hawamo, kama mrisho ngasa, mgosi au kina chuji wengine wengi vipi huu utakuwa upendeleo sasa
ReplyDeleteAfrikan Player of the Year should be playing in Afrika! Let CAF create another award for Afrikan Player of the Year in the Diaspora na ndio hilo washindanie wale wote wanaocheza mpira wao nje ya Afrika. Anyway, thats my opinion which I am entitled to.
ReplyDeleteAfrican Player of the Year: Tresor Mputu Mabi.
mechi ya tanganyika na zanzibar iko wapi???
ReplyDeletemchezaji bora awe anachezea afrika tu sio hao wa nje!!!should be playing in afrika alone not outside our continent...
ni sawa na kucheza eti mchezaji bora wa dunia tennis,golf,kuogelea nk ilhali afrika haihusishwi kabisa
ujinga mtupu
mnaosema mchezaji bora atoke afrika jueni ya kwamba kuna ranking za ligi duniani na ulaya ipo juu,, labda wawaanzishie tuzo ya mchezaji bora wa ndani kama caf walivyofanya CHAN
ReplyDeleteHizo zao kina BBC na wenzao, Afrika bado inawekwa pembeni kwa mikakati, huu ni mfano mmoja katika mingi, ili kukatisha tamaa na kuonyesha bado hatuna ubora bila ulaya kutaka.
ReplyDeletejamani uzalendo ni mzuri ila tuwe wakweli.
ReplyDeleteMashindano haya hayazuii Mchezaji anayechezea ligi za nyumbani kushinda. Lakini ukweli ni kwamba wachezaji walio bora zaidi huwa mara nyingi wanaenda kuchezea ligi za Ulaya. Tuwe wakweli, ni mshambuliaji gani anayechezea ligi nyumbani unaweza kumshindanisha na kina Eto'o na Drogba? Kitu cha muhimu ili mradi uraia wako uwe wa nchi ya Afrika, haijalishi unacheza mpira Japan, Australia au Uingereza.