Kampuni ya Flora Promotions ya jijini Mwanza imeaandaa shindano la kutafuta, kukuza na kuwezesha vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili liitwalo ZABURI GOSPEL SEARCH 2009, ili kueneza neno la mungu kupitia nyimbo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Flora Promotions ambao ndiye mratibu wa shindano hilo Bi.Flora Lauwo alifafanua hivi karibuni jijini Mwanza kuwa “Suala la zawadi liko wazi kabisa, ni kwamba mshindi wa kwanza atajinyakulia gari aina ya Vistar yenye thamani ya milioni nane,mshindi wa pili ataibuka na seti ya vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Samila Mobile Sound,mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi laki mbili,lakini pia mshindi wa kwanza mpaka tano watarekodiwa albamu moja moja na studio za Habari Maalum” alisema Flora.
Flora amesema kuwa,kwa mara ya kwanza mwaka 2009, kipindi cha ZABURI GOSPEL SEARCH kimeanzia kanda ya Ziwa kwa kutafuta washiriki kila mkoa na kufanikiwa kuibuka na waimbaji watano ambapo jumla wamekuwa 20,anasema na kuongeza kuwa washiriki hao tayari wameingia kambini kujinoa tayari kwa michuano ambayo tayari imekwishaanza anza kurushwa hewani kupitia Star Tv na wananchi kuwapigia kura wakisaidiana na majaji kutafuta mwimbaji bora.”alisema Flora.
“ZABURI GOSPEL SEARCH 2009 itakuwa na matamasha makubwa matatu moja litakuwa ni robo fainali litakalofanyika mkoani Shinyanga tar,25/12/2009 na nusu fainali itakuwa Musoma mkoani Mara tar,27.12.2009, na fainali yenyewe itafanyikia jijini Mwanza Januari 1, 2010 siku ya mwaka mpya”alieleza Bi Flora.
Bi Flora alimaliza kwa kusema kuwa lengo lao ni kukuza na kuwezesha waimbaji wa muziki wa injili na kuwatangaza Kitaifa na Kimataifa, ili waweze kijipatia kipato na kufaidika kwa namna moja ama nyingine kama wasanii wengingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...