timu ya taifa ya vijana enzi hizo ambapo kila klabu ilikuwa na timu ya watoto na michezo ya shule za msingi na sekondari ilikuwa imeshamiri. Na ndipo iliweza kupatikana timu ya taifa iliyo imara iliyofanikiwa hata kucheza kombe la mataifa kule nigeria. mfumo huu, ambao uliwekwa kando kwa kisingizio eti vijana wanaenda zaidi michezo kuliko masomo, ndio kwanza umerejeshwa na kuna matumaini hali ikarejea kama zamani endapo utatiliwa mkazo.
wadau wenye data msaada tutani. hapo ankal anaanza na kocha mohamed msomali waliosimama wa kwanza kulia na raha msigala wa mbele kulia pamoja na abdul amasha wa pili kulia kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Umetoa reference nzuri sana kuhusu timu ya taifa ilivyokua ikipatikana.
    Wote tukiwa tunakumbukumbu nzuri kama wewe then tutakua hatuna sababu ya kumlaumu Maximo(Simtetei Maximo).
    Huyu baba wa watu(Maximo) amepewa kazi ngumu sana ya kufundisha hawa wachezaji wetu hasa kutokana na source yao(wamepatikana wapi?).
    Nilikua naangalia mechi zilizomalizika sunday,you can tell by seeing the faces our players wanaonekana ni wavuta Bangi(midomo imeungua na moshi) ndio maana hata sikuwa nikishangaa wanapokua hawana maamuzi sahihi uwanjani(Nyoso,Muharami(kipa),Yondani).
    Sasa huyu maximo amepewa wavuta bangi awafundishe soka,si kwamba hawajui lahasha bali anakua na sample ndogo ya kuchagua wachezaji ndio maana ana rely on those "academic misfit"(wavuta bangi).Tujiulize swali hakuna wachezaji walio katika university level?(problem with our academic curriculum),kwahiyo point yangu ni kuwa kama tunataka tuendelee kisoka mambo haya manne yanatakiwa kuzingatiwa

    1.Turudishe umitashumta
    2.turudishe umiseta
    3Turudishe utaratibu wa kupata timu za taifa za vijana(from 2 sources above)
    4.Change of academic timetables katika vyuo ili wanachuo waweze participate katika machezo.

    Tukifanya haya tutapunguza utegemezi wa wavuta bangi and "academic misfit" katika kuliwakilisha Taifa.

    "Mungu ibariki Tanzania"

    ReplyDelete
  2. Zamoyoni mogella, wa pili kushoto waliosimama nyuma.
    Kwa nyuma kabisa kuna vikombe vingi sana, ina maana timu yetu ya taifa ilifanikiwa kuvichukua vyote hivyo. Au tuliomba kupiga picha kwenye stoo ya Real Madrid?

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi naikumbuka hii timu ya taifa ya vijana katika miaka ya 80 walikwenda Norway kwa ajiri ya mechi za kirafiki na hiyo ilikuwa ni msaada uliotolewa na Norway ili kuendeleza soccer la Tanzania na katika timu hii ni wachezaji wachache sana walioweza kufanikiwa kuchezea club za daraja la kwanza(A)kwa mfano Zamoyoni Mogella, Athumani China,Kassim Matitu,Malota soma lakini wengine wote waliishia kwenye timu B ya club zao za daraja la kwanza.

    ReplyDelete
  4. Kwa Anonymous wa 01:24 PM ningekuwa mimi mchezaji mmojawapo na sivuti bangi ningeudhika sana na kauli zako. Siamini kwamba wachezaji wetu wote ni wavuta bangi - japo yawezekana wapo wa namna hiyo kama ambavyo hata ligi kubwa duniani zisivyoachana nao. Pili kufikiria kuwa na wachezaji wa kiwango cha usomi wa chuo kikuu ni ndoto - karibu duniani kote. Hii ni kwa sababu si rahisi kufaulu kwa ngazi ya juu katika michezo na masomo kwa wakati mmoja - hususan pale ufanisi huo unapotakiwa wakat mtu akiwa na umri ule ule (takriban miaka 18-28). Miaka ya nyuma huko Uingereza mbunge mmoja alitoa rai wachezaji wa ligi kuu wapewe fursa ya kujiendeleza kimasomo ili wamalizapo kucheza waweze kuchukua kazi za kulipwa. Nakumbuka Arsene Wenger aliuliza kama mbunge huyo alikuwa kweli anajua kilichomo ndani ya vichwa vya wachezaji wengi wa ligi kuu au alikuwa anaota! Nafikiri muhimu ni kuwa na taasisi za michezo zenye kulenga kukuza vipaji vya wachezaji - hizi zinaendelezwa duniani kote na vilabu - kama Yanga ya watoto ilivyowatoa kina Tostao, Kassim Manara, Pondamali na wengineo. Wapo mitaani kina Adolf, Pondamali nafikiri wakitimiwa ipasavyo inaweza kusaidia taifa kuondokana na kuwa kichwa cha mwendawazimu (Mwinyi et al, XXX).

    ReplyDelete
  5. Aisee enzi hizi we acha tu. waliosimama wa2 toka shoto ni Zamoyoni mogela na wa2 toka kulia ni James kisaka
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete
  6. Mbona hawajavaa magwanda ya kijeshi?Maana enzi zile za Mwalimu kila mtu ni mwanajeshi...

    ReplyDelete
  7. Ankal na wanajumuiya wote nimewatambua wachache kwenye hiyo picha wa pili kushoto waliosimama ni Zamoyoni Mogella na anayemfutia ni Marehemu Albert Rweyemamu.

    Tanzania Daima...

    ReplyDelete
  8. Toka kushoto waliyochuchuma wa pili ni Said George (BEST) winga machachari wa enzi hizo!!! (dRU)

    ReplyDelete
  9. Waliochuchumaa chini wa kwanza kushoto ni Sospeter Mwaluko, alicheza Reli Morogoro kisha akachezea wekundu wa msimbazi, sasa hivi anafanya kazi manispaa ya ilala.

    ReplyDelete
  10. ankal mimi nadhani yule ulomtaja wewe kwa jina la abdul amasha mi nahisi ulishikwa na kwikwi kidogo yule ni ahmed amasha

    ReplyDelete
  11. Huyu mwenye nywele ndefu (afro) Nadhani ni Abdalah Mwinyimkuu aka Pele.

    ReplyDelete
  12. Mchezaji wa zamani Omary Chogo "Mluya" wa Simba ndiye pekee alikuwa mvuta bangi na pia mchezaji mzuri.Chogo alikuwa akivuta bangi...hapiti mtu!!.Bonge la senta-hafu.Old school player.

    ReplyDelete
  13. SOSPETER MWALUKO, KUSHOTO MACHO MAJANJA NA SMILE AS ALWAYS. UYU NI JINA KUBWA ALIKUA ANACHEZA NO.11, TZ LABDA AIJAWAI KUPATA WINGA KAMA ANKO SOS TANGU AACHANE NA MPILA KWENDA KUFANYA KAZI JIJI. ALIKUA NA MASHOTO YA HATARI. HII NI HISTORIA ISIYOKUA YAKUPOTEZA KABISAA.SOS NI MTU POA SANA MKARIMU NA MWENYE KUJALI SANA BINADAMU WENZIE. MUNGU AKUBARIKI MJOMBA SOS. DU NIMEMISS SANA VITUKO VYAKO MJOMBA.

    HASH...

    ReplyDelete
  14. dah kweli we mdau unayedai bangi inamsaidia sentahalf kudhibiti mshambuliaji asipite umepinda kweli..bado unaishi dunia ya mwaka 47! mabeki bora wa dunia ya soka ya sasa hawategemei bangi ili wazuie washambuliaji..kipaji juhudi ya mazoezi na uelewa mzuri ndio siri ya mafanikio

    ReplyDelete
  15. Mwenye afro nina uhakika 150% ni Abdallah"Pele" Mwinyimkuu,alianza kucheza mpira wake Shycom then Simba.
    mdau uk

    ReplyDelete
  16. waliosimama- mogella (wa2),rweyemamu(wa3), malota soma (wa5), james kisaka (wa9)

    katikati- abdallah mwinyimkuu (afro)

    waliochuchumaa chini- mwaluko (wa1), gordian mapango (2nd)

    ReplyDelete
  17. Si amini kama atakuwa Abdallah Mwinyimkuu kwani yeye na kina Zamoyoni wanapishana sana umri Abdallah ni mkubwa.
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...