Twiga akiwa na mkia wake mzima


Imegundulika kwamba twiga wengi katika hifadhi ya wanyama ya Momella na Arusha National Park mkoani Arusha hawana mikia, wengi wao wakionesha kuwa imekatwa ama kung'atwa.

Wataalamu wanashuku kwamba huenda hii inasababishwa na kukosekana kwa simba katika hifadhi hizo, hivyo fisi ambao hutegemea kula mizoga iliyoacha na simba kama mlo hukosa cha kutafuna na kuvamia mikia ya twiga.

Askari wanyama pori wa Momella Bw. Bosco Kessy Atanasio amenukuliwa akisema kukiwa hakuna wanyama wawindaji kwenye hifadhi ambao huacha mizoga imezagaa kila mahali inakuwa ni njaa kwa fisi.

"Wakiwa wala mizoga wa asili na kukiwa hakuna mlo huo fisi huvamia twiga na kung'ata mikia yao kila wapatapo nafasi", anasema Bw. Atanasio, na kuongezea kuwa si ajabu twiga wengi katika hifadhi hizo hawana mikia ama wana vingunguti tu.

Twiga ndiye mnyama mwenye mkia mrefu katika wanyama wa ardhini ambapo mkia huwa na urefu wa futi 8 takriban mita 2.4 ikiwa ni pamoja na usinga wake. Watalaam wanasema mnyama huyu mrefu huishi miaka kati ya 20 na 25 tu.

Habari zinazidi kudatisha kwamba majangili nao wamekuwa wakiuwa twiga kwa ajili ya ngozi na mikia yao, na pia kuna makabila yanajulikana kutengeneza bangili kutoka usinga wa mikia ya twiga na kuwauzia watalii.

Vile vile katika miaka 2006 hadi 2008 ujangili mkubwa wa mnyama twiga ulirekodiwa katika hifadhi Kilimanjaro magharibi ambao ni ukanda unaojumuisha Momella, Arusha National Park na Kilimanjaro National park na kwamba ulichangiwa kwa sana na imani kwamba mafuta ndani ya mfupa wa twiga ni dawa ya ukiwmwi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ha ha ha ha this might be a joke.Kimo cha twiga na kimo cha fisi.Make you own math

    ReplyDelete
  2. Ukatili kwa wanyama

    ReplyDelete
  3. mashallwahu twiga kakaa vizuri nae sema mrefu tu kumfikia tabu.mmmmmkaumbika haswaa

    ReplyDelete
  4. siamini twiga anaishi miaka mitano tu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...