zengwe la kumng'oa marcio maximo linapikwa na wakati wowote kuanzia sasa kocha huyu wa taifa stars atajikuta kibarua kimeota mbawa. uchunguzi wa globu ya jamii umebaini kwamba hivi sasa shirikisho la soka TFF lipo njia moja kusaka mbadala wake na mkataba wake kusitishwa kabla ya muda wake. TFF wamepata nguvu baada ya JK ambaye analipa mshahara wa kocha huyu kutoka brazil kuruka kimanga na kusisitiza yeye hamlindi wala nini na haingilii mambo ya TFF zaidi ya kusaidia kulipa mshahara wake ambao hadi sasa hakuna anayejua ni shi'ngapi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. PETER NALITOLELADecember 19, 2009

    HUYU KOCHA KUSEMA KWELI, ANATUKEJELI SANA HASA KUMUONA ONA KWENYE MASHINDANO YA UMISS NDO MAANA ANASHINDWA KUKOCHI BOLI.AKISHAANGALIA VISURA ANABAKI AKIWAZA KILA MARA YALE MALIMBWENDE BADALA YA KUTAFUTA STRATEGI YA KUSHINDA MPILA. MIMI NAPENDEKEZA HUYU KOCHA APELEKWE MUZUMBE AKASOME KIDOGO NDIO TIMU LETU LA TAIFA LITAFANIKIWA KUFIKA KOMBE LA DUNIA VINGINEVYO SISI SIKU ZOTE TUTAKUWA WASINDIKIZAJI TU KAMA KAWA. HUYU KOCHA HAFAI KABISA. NA MIMI NITAMTUMIA RAIS JK AMTIMUE AU NIMUOMBE NAMBII YOHANA MASHAKA AANDIKE MAKALA KALI SANA YA KUOMBA WADAU WAMTOE KWA NGUVU, LASIVYO US-BULOGA ACHUKUE HATAMU YA KUMLIPA HELA ZAKE ZA KIFISADI ZA KUUZA GONGO MITAANI HUKU ANAJIDAI HETI YEYE NI TAJILI TAJILI GANI HAJAKANYAGA HATA MUZUMBE, BWANA ASITUZINGUE KAMA MAXIMO MBABAISHAJI

    ReplyDelete
  2. US Blogger)
    Maximo hana lolote, ni mbabaishaji tu. Huyu alikuwa anakochi Salsa Dance siyo mpira, kwa hiyo achukue Taimu. Mimi naenda Hispania kutafuta kocha mpya na nitamlipa Dola kubwa na kumpangishia nyumba kule Masaki na kumpa VoGUE V8

    Wadau nimasheni, nasikia nabii naye kafulia kweli kweli ndo maana siku hizi haandiki tena? Ikiwa nabii kafulia, basi nitamlipa mimi ili akafanye kazi ya kufundisha wanangu

    Maximo mimi nilijitolea kumlipa mshahara wa $30,000 kwa mwezi lakini ujuaji wake ulinishinda. Bado niko tyari kudhamini timu ya taifa kwa hiyo mnipe muda hadi Machi mwakani ili nitoe offer nyingine kwa kocha mpya

    US blogger

    ReplyDelete
  3. With all due respect,I've read some comments from my fellow Tanzanians.It seems like we all like our national team to win othewise we would all remain silence.But we should understand that soccer is a professional business.It's a career just like any othe career.For someone to be a medical doctor,he/she needs to go through several stages of academic trainings theoretically and practically before practicing medicene.That was just a fraction of millions of examples.We will never go to the next athletic level in terms of soccer if we continue with our current trend of recruiting players.We must start building a foundation with our young teens,hopefully,five years down the road we will see glory.Expensive coaches will never transform our aged players into professional soccer playes.We're just wasting our time and resources.However,I commend our current players for trying the best they could.They tried over and over to prove that they cannot walk on waters but at least they can sweam.Let's agree that our wrongfull preparation will get our nation to no where.
    Toto tundu-Upper Marlboro.

    ReplyDelete
  4. NADHANI WATU WENGI TUNAKUBALIANA KWAMBA HAPO ALIPOFIKIA NDIYO UWEZO WA MWISHO. HAKUNA JIPYA ANALOWEZA KUFANYA TENA KUIPANDISHIA TIMU YETU KIWANGO.

    KWA KWELI TFF WALITAKIWA KULIONA HILI MAPEMA. PAMOJA NA KIBURI CHAKE AMBACHO KIMECHANGIA SANA KUANGUKA KWAKE TUMSHUKURU KWA ALIPOTUFIKISHA.

    SASA TFF WASIVUTE SANA WANATAKIWA WAMUANDALIE HAKI ZAKE MAPEMA AONDOKE KWANI UWEPO WAKE SASA HIVI HAUSAIDIA LOLOTE NI BORA TUOKOE PESA ZETU.

    SIKUKUU NJEMA.

    ReplyDelete
  5. oya saingine jamani tuna mlaumju tu maximo wa watu.wabongonao vichwa vyao ni vigumu sana kuelewa.unamfundisha kitu hicho chicho lakini kinaingia sikio la kuchoto kinatoka sikio la kulia.Mi nawajua wa bongo vizu azwa wale ambao awajaenda shule.wagumu sana kuelewa.Plus wachezaji wengi wa bongo katika maisha yako 99 % wamesha onja baki.So akili zao zimeganda kidogo.

    Mdau Pakistani

    ReplyDelete
  6. maximo tunamlaumu bure tuu wabongo vichwa ni vigumu angalia asilimia 90% ya watanzania wanaomaliza vyuo vikuu hawajui kuongea KINGEREZA wakati huohuo wamesoma kiingereza zaidi ya miaka 13 (i.e. darasa la 3-7 miaka 4, form 1-4 miaka 4, form 5-6 miaka 2,chuo 1styr - 3rdyr miaka 3) wote waliomaliza wenyewe wakiwa wanawaza ndani ya mioyo yao wanahisi wanajua kuongea ukiwaambia hamjui ni wakali hao... hata wacheza wetu, waandishi wa habari na makocha wa kibongo vilevile techniques na skills za soccer zipo mioyoni mwao (theoretically)

    ReplyDelete
  7. Jamani!
    Wakati sisi tunamponda Maximo wenzetu wanamlilia sana kwakuwa wao timu zao ziko tayari. Kule haendi kudundisha kupiga dana dana " mafunzo ya awali wa mpira wa miguu"
    Unumda wa wachezaji wetu ni tatizo sana. Atapata timu na atakuja nayo tutapigwamabao kama tumesimama.
    Tujiulize tumempa maximo watu wa aina gani kufundishaaaaa

    ReplyDelete
  8. Maximo tunamlaumu bure. Mi nadhani hata akija kocha wa Arsenal au Man U hawezi kuwapeleka wachezaji wa bongo kombe la dunia.

    ReplyDelete
  9. nyinyi watu kuna haja gani ya kumuweka huyu kocha ikiwa hata zanzibar wametufunga hawana hata kocha kutoka popote afukuzwee asap.

    ReplyDelete
  10. Nilishikwa na shauku kubwa pale TFF ilipotangaza Maximo anachukua timu yetu ya Taifa na mpaka nikatafuta profile yake na kuisoma kwa ufasaha hasa ili kumjua kabla hata hajaanza kazi rasmi.
    Lakini cha kushanga za ni hii MIKATABA TULIYOMSAINISHA HUYU JAMAA. Kwanini nasema hivyo sababu kama navyojua mimi na nitawaeleza kwa mifano kidogo. Mf(1) Kama kocha anachukua timu iko chini kwenye ligi au haijapata mafanikio kwa muda Kochaanapokuja kuangalia soka la nchi au timu kabla hajasaini mkataba lazima anatoa AHADI kwa mfano kuwa timu hii nitaibakisha kwenye ligi na tutafamaliza juu ya nafasi ya kumi au nafasi nne na kushiriki ligi shirikishi. Kwa timu ya taifa anahidi kwa mfano kuipandisha nafasi kwenye kiwango cha fifa nafasi juu ya 65 ili wachezaji wapate nafasi ya kucheza nje kirahisi au kipindi cha muda mufali nitahakikisha nafudhu kitu au jambo fulani.

    LAKINI CHA KUSHANGAZA HATA WAANDISHI WA HABARI WALISHINDWA KUMUULIZA HAYO YOTE WAKATI ANACHUKUA KAZI NA SASA WANASHINDWA HATA CHA KUMSHIKIA BANGO SABABU HAKUAHIDI CHOCHOTE WAKATI ANACHUKUA KAZI. AU SABABU NI RAISI NDIYE ANAYEMLIPA MSHAHARA?
    MIMI KILA SIKU NAJIULIZA HUYU JAMAA KWENYE MKATABA WAKE ALIAHIDI NINI KAMA ALIAHIDI JAMBO AU KITU NA KAWEZA KUKIFANIKISHA BASI HAMNA SABABU YA KUKATIZA MKATABA WAKE LAKINI KAMA AMESHINDWA KUTIMIZA AHADI ZA MKATABA WAKE AFUNGASHE SASA HIVI NA LAZIMA IWE NA MUDA WE WILL NOT WAIT FOREVER, WE SHOULD HAVE A TIME LIMIT FULL STOP.

    Hivyo mzee wa Ankal naniiinhii tunaombe tutafutie kwenye kumbukumbu zako huyu jamaa aliahidi nini pale alipopewa kazi.

    mdau wa soka Ukerewe hapa

    ReplyDelete
  11. Wewe (anon:Sat Dec 19, 01:26:00 PM). kingereza unakijua kukiongea na kukiandika?
    Kwa kusema hivyo unakuwa unaongea pumba. Maximo ni anatoka Brazil lakini hicho kiingereza hakijui vizuri si ndio? Ni kama baadhi wa hawo wabongo wanaomaliza vyuo.
    SYSTEM ya michezo Tanzania inatakiwa kurekebishwa kiujumla na watu ambao wanaweza kurekebisha michezo ni sio mimi na wewe bali hawo can i say POLITICIANS?

    Naona soma history ya michezo duniani ndio utanielewa.

    Mbeba box UK

    ReplyDelete
  12. MICHUZI...MARCIO MAXIMO ANALIPWA DOLA 12,000 KWA MWEZI, YAANI SHILINGI MILIONI KAMA 15 ZA KITANZANIA KWA MWEZI...KITU KINACHOMFANYA APOKEE DOLA 150,000 KWA MWAKA, AMBAO BADO NI MSHAHARA MDOGO SAAANA KWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA AMBAYE AMELETWA TOKA NCHI NYINGINE....HATA HAO TFF WAKIKATISHA MKATABA WAO, SERIKALI ITATAKIWA KUMLIPA HELA YA MUDA WOTE ULIOBAKI KTK MKATABA...THINK BIG!!

    ReplyDelete
  13. mimi nadhani tumuachie aendelee kwani kuyaanzisha majungu na fitina hivi vitu vimepitwa na wakati kwani hii hoja ya yeye kubaki au la ni suala la wanao husika kama muheshimiwa Rais alivyo sema, namfagilia JK kwa hekima na busara na ukali kidogo pale linapotokea jambo lisilo mpendeza kama Rais au lisilopendezwa na wanachi!!! Amesema yeye ataendelea kumlipa ila suala la maximo kubaki au la nisuala la TTF!!! so wao ndio wanajua kama maximo anafaa au la, ukizingatia kwamba kabla ya maximo Taifa stars ilikuwa ya 167 ktk takwimu za Fifa kwa sasa hivi ni ya106!! hivyo tunaona kabisa huyu maximo ni cocha mzuri!! tumuachie muda wake umalizike!!!!!

    Mdau university of USA!

    ReplyDelete
  14. Habari za Ligi Uingereza:
    Kocha Mark Hughes wa timu tajiri duniani ManCity atimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Roberto Mancini.

    ManCity imetumia zaidi ya paundi 100 millioni(tshs 200 bilioni) kusaini majina makubwa msimu huu Carlos Tevez, Adebayor n.k

    ManCity ktk mechi 77 chini ya kocha aliyetimuliwa Mark Hughes, imeshinda mechi 36; draw 16; kushundwa 25; sawa na asilimia 45% ya ushindi kutoka mechi 77. ManCity imeshindwa mechi chache ktk premier league yaani mechi 2, wakati Chelsea imeshindwa 3 na ManUtd imeshindwa mechi 5 mpaka sasa.

    Wakati vigogo wa soka waadhiriwa leo, Fulham 3 ManUtd 0; Portsmouth 2 liverpool 0; Arsenal 3 hull 0; ManCity 4 Sunderland 3.

    ReplyDelete
  15. we anonymous wa Sat Dec 19, 01:26:00 PM tatizo lililoko hapa sio kiingereza ni shule je wameenda shule?nyie ndio wale ambao mkiona mtu anaongea kingereza mnamwita msomi,uwe unafikiria kwanza kabla ya kukurupuka mahouse boys and girls kibao wa kimalawi wako bongo hawajafika hata darasa la tatu wanaongea kingereza sasa utawaita wasomi?acha hizo wewe nyie ndio wale mnaowapeleka watoto english medium mkijua watoto wakiongea kiingereza ndio wameelimika.Kama mtu ameenda chuo kutafuta degree ya kingereza sawa,KWANI HUYO MAXIMO UNAYEMTETEA ANAJUA KIINGEREZA AU KWA VILE UMESIKIA JINA TZ TU NDIO UMEONA UPONDE?kwanza lugha yetu ni kiswahili acha kuabudu lugha za wengine.

    ReplyDelete
  16. Mimi nadhani pia tuangalie naupande wa pili ambapo kwa sasa mpira ni biashara ukiachilia mbali raha tunayopata watazamaji; toka move ya Kikwete kumleta huyu jamaa mabadiriko makubwa tu yametokea pale TFF ikiwa ni pamoja na wadhamini kibao, mimi nadhani tuangalie huko zaidi, huyu bwana kwa sasa basi, hapa panatosha. Maoni yangu tumlete kocha kutoka ulaya tena ufaransa, holland au Ujeumani, tena awe wa kawaida tu asiye na sifa tele (well known) bali awe ambaye anakuja kutafuta sifa (kuuza jina). Kocha wa kibrazil wabakie kuwa wa vijana kufanyaorganisation ya soka huku chini. Tatizo tunaandika wausika hawasomi.

    ReplyDelete
  17. Livingston Football Club Scottish association football

    * Scotland Jim Leishman (1995–1997)
    * Scotland Ray Stewart (1997–2000)
    * Scotland Jim Leishman (2000–2003)
    * Brazil Marcio Maximo Barcellos (2003)
    * Scotland David Hay (2003–2004)
    * Scotland Allan Preston (2004)
    * Scotland Richard Gough (2004–2005)
    * Scotland Paul Lambert (2005–2006)
    * Scotland Alec Cleland (Caretaker, 2006)
    * Scotland John Robertson (2006–2007)
    * Scotland Dave Bowman (Caretaker, 2007)
    * England Mark Proctor (2007–2008)
    * Italy Roberto Landi (2008)
    * Scotland Paul Hegarty (2008–2009)
    * Scotland David Hay (Caretaker, 2009)
    * United States John Murphy (2009)
    * Scotland Gary Bollan (2009–)



    Na papaa Stan
    Moshi. kilimanjaro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...