Home
Unlabelled
uwanja wa ndege wakimataifa wa julius nyerere usiku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mdau ulioweka hii picha nakushukuru sana, maana huu uwanja unatia haibu hauna tofauti na lile shamba la bibi - uwanja wa uhuru...serikali ituambie lini itajenga uwanja wa maana? uwanja wa ndege jamaani ni kitega uchumi...hivi viongzi hawaoni aibu kwa haka kajengo pale weenzao wanapowatembelea...Dar inabidi kuwe na uwanja wa maana then mikoani ndo wajenga design hii...tunakosa mamimilioni kwa ukosefu wa ubunifu.
ReplyDeleteWe bana umechemsha...Ni uwanja wa ndege wa Julius nyerere Airport...siyo kama ulivyoandika
ReplyDeleteHamna kitu hapo...HEATHROW funga kazi.
ReplyDeletekazi kweli jumatano 23/12 kazi ninayo hapo nashuka saa 1 usiku kupambana na vibaka uliyeweka picha umenipa fleva za watu wa ushuru wanavotoa macho. kweli uwanja hatuna ndugu yangu heathrow mbona unaenda mbali sana anzia Nairobi. we have longway to go na wasiotoka ktk nchi hii wanaona we leading all over the world
ReplyDeleteUnafuga wezi tu wamizigo yetu.
ReplyDeleteafadhali ya huu..yaliyomo uwanja wa zenji je??mhhhhhhhhh...........na giza hili ni balaa..
ReplyDeletehabari za kazi kaka michuzi? napenda kuwakumbusha hao watanzania wenzangu walio toa maoni yaojuu ya uwanja wetu wa kimataifa wa ndede,jamani watanzania tuwe tunajiangalia tumetoka wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi, sio kuwa tunalaumu tu hata mambo yasio kuwa na mbele wala nyuma, Tanzania ya leo ina mambo mengi sana ya kuyapa kipaumbele zaidi ya hilo la kujenga uwanja wa kisasa kama Heathrow(london), John F.Kennedy(New york) au Oliver Tambo(SA), kuna mambo ya msingi kama kujenga barabara za kuunganisha mikoa au wilaya, vile kuna kujenga zahanati ili kila mtanzania apate afya bora na pia kuna kujenga madarasa ya shule za msingi au sekondari ili angalau kila mtanzania apate angalau elimu ya awali hayo yote ni mambo ya muhimu sana kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu, sio kuwaza kujenga uwanja wa kisasa jamiani kabla ya kutoa maono yetu tuwe tunafikilia sio kukurupuka tu, na kutaka kufananisha kila kitu cha tanzania na hizi nchi zilizoendelea, bado tuna safari ndefu sana ya kufika hapo, mdau Ngamanya
ReplyDeleteMnaorudi Bongo kwa likizo au kazi mna moyo sana.
ReplyDeletenyinyi mnasikitika hamna kiatu sisi wenzenu zanzibar hatuna mguu wa kuvalia kiatu,naomba mdau akashukie kule zenji alafu atupe habari.
ReplyDeleteTanzania uwanja wenye hadhi za kimataifa BAADO KABISA YANI. Tunajikanyaga tu.
ReplyDeleteni kweli hapo zenji looo uwanja wao mbaya
ReplyDeleteUwanja bomu bwanaaa. Unanuka vyoo. Rushwa kibao na wezi ndio usiseme. Aibu tupu.
ReplyDeleteDUUUUHHHH...IT LOOKS LIKE A PETROL STATION....!!!!HAHAHAHAHAH
ReplyDeleteKama ni suala la wizi wa mizigo nadhani Nairobi inaongoza. Kuhusu kauwanja ketu kwa kweli ni aibu sana ukona hata Ethiopia wanatushinda mara 200.
ReplyDeleteDuh afadhali wadau mmezungumzia suala la wizi wa mizigo hapo eapot,mimi nilifikiri ni mimi tu peke yangu ndo niliyelizwa kumbe tuko wengi..ni aibu mno eapot yetu ina lundo la wezi na wadai rushwa..tunaomba watu waelewe kuwa kusafiri sio ishu sisi nasi ni watafutaji tu na sio wote mamilionea wala nini..acheni wizi jamani..Dah tena mm nashuka hapo tar 30 usiku na klm mabegi yangu nimeyatia kufuri mbaya!!na vijisent vyangu vyote viko atm so hakuna rushwa wala mapene loose
ReplyDeleteTanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo woteee. Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana ......
ReplyDeleteJamani watanzania tunapokoselewa tusikasirike ila iwe ni challenge. Kwa kweli huo uwanja haufai kabisa kuwa na hadhi ya kimataifa, kama kawaida yetu usafi ni Kasheshe juzi niliingia chooni kidogo nitapike. You don't need billons of Shs for cleaness. Hoa waosha vyoo wenyewe wamekaa pembeni wanasogoa, nilijistukia nikisema I have never seen the dirtiest air port like this in my life yaani is just yakii
ReplyDeleteHivi wewe Ngamanya unazungumza nini?kwa nini tusikemee?nyinyi ndiyo mko wengi na ndiyo mnaoleta matatizo hapa TZ.unatetea nini sasa?hebu tuambie hiyo afya,elimu na barabara,bado hukusema chochote kuhusu maji na umeme vitu ambayo ni muhimu kwa kila binadamu,kwetu TZ tumeafikia wapi? Ni aibu tu mjomba ukubali au ukatae, ni aibu kwelikweli kwa nchi yetu yenye uwezo mkubwa tu wa kuweza kutatua matatizo yote hayo na kuwa mfano mzuri kwa nchi nyingine,nchi ambayo haikuwa na vita kupata uhuru inashindwa na nchi kama angola na mozambique zilizokuwa na vita,badala yake kuweka rushwa mbele na wizi wa mali za uma bila aibu, kununua marada mabovu na kuingia mikataba mibovu kwa kuwa tu wanapewa rushwa,sasa fedha zote hizo walizokula na wanazokula zingeshindwa kujenga uwanja mpya wa ndege wa kimataifa? acheni kutetea maozo.
ReplyDeletejamani mimi nasikiauchungu sana
ReplyDeletemnisaidie ule mchango tunatoa pale kwa gate unaenda wapi nani ninani msimamizi maana mchato mzima pale siuuelewi walaah
ni rushwa na dili kila kona ....
mmh halafu wafanyakazi wa hii airpot wengine wamezidi kuomba hela..eh inatia aibu jamani, yaani mpaka tunaogopa kupita.. ebo.
ReplyDelete