Baadhi ya wanafunzi wa bweni wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Sumbawanga katika Manusipaa ya Sumbawanga , Mkoani Rukwa, wakiwa mbele ya jengo la utawala shuleni hapo. Wanafunzi hao wamefanya vurugu shuleni hapo usiku wa kuamkia jana (Jumanne) kwa kupiga mawe majengo ya shule na hatimaye kuchoma moto uzio wa nyumba ya mwalimu wao wa nidhamu kudai uhuru zaidi ili waruhusiwe kumiliki simu za mkononi na pia waruhusiwe kutoka nje ya shule usiku. Picha na mdau Peti Siyame
Home
Unlabelled
vurugu shule ya sekondari sumbawanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kupiga nyumba ya mwalimu wa nidham ni upumbavu.wanachodai kama simu za mkononi hao sio watoto waruhusiwe kutumi coz wana hitaji kuwasiliana na wazazi wao,mimi shule niliyosoma A LEVEL ilikuwa uhuru kwa kwenda mbele.yaan kama UNI..,unapigiwa sim kama upo class unatoka nje bana,
ReplyDeletekweli hii noma.hiki ndicho kizazi cha nyoka..lakini jamani ni kweli au mnawapakazia tu..ni kweli wanataka kutoka usiku?au kuna mambo mengine wanayadai
ReplyDeletemadai yao ni hayo tu au kuna mengine? kama ni hayo tu basi subirini mkimaliza masomo yenu mtagundua kuwa mlikuwa mnapigania upuuzi!!!! tulipita huko na sasa tunaona upi ulikuwa mchele na zipi ni pumba, buku tu wanangu kazeni msuli yote mtayakuta mtaani mkimaliza
ReplyDeletetuliwahi kugoma shule na kufanya vurugu kabla ya hao vijeba lakini sio kwa sababu chepechepe kama hizi. simu hazikuwepo lakini tulisoma shule kwa raha. ruksa haikuwepo lakini tulitoroka na kurudi salama. tafadhali mtuambie sababu zingine. hizo sio za kweli na kama ni za kweli basi dunia imefika mwisho.
ReplyDeletena wazazi wa siku hizi nao wanachangia upuuuzi kama huu. mitihani wawaibie watoto wao, simu wawanunulie. basi vululuvululu tu.
Asilimia kubwa ya watu bongo wamekuwa watumwa wa simu na kusahau kabisa hata majukumu yao ya kila siku.
ReplyDeleteMaofisini watu wapo bize na sim na hawaoni hata aibu kwa mteja aliekaa kusubiri huduma. Na hawakumbuki hata kuweka silent ili isibugudhi wengine.
Sasa na hao wanafunzi tena wakiruhusiwa kutumia sim kila mahali hapo shule si itakuwa vululuvululu kama mdau alivyosema?
Watoto acheni upuuzi someni someni sio muda wote simu simu kama mlizaliwa nazo? Ukiangalia asilimia kubwa ya watu wanatumia garama nyingi sana katika simu ukilinganisha na lishe yao.
Wanafunzi punguzeni ulimbukeni wazazi wenu wanapata shida kujinyima ili nyie muende shule.
Kama ndo wameleta vurugu kwa sababu ya huu upuuzi wapewe adhabu inayostahili.
hanha mie M sumbawanga hiyo shule mbona siijui? ok sie tulisomea Kantalamba enzi hizo za kina mwalimu Dule mwalimu wa nidhamu subutu ,kuleta kichwa kichwa lakini kweli boys walikuwa watoroko kupitia njia ya bondeni na kurudi back swari tu,Kuchoma nyumba ya mwalimu ni uupuuzi wa hali ya juu,wote warudishwe ma mwao kwa muda hizi watafakari walo fanya maana wakiwa hapo shule wanasahau waliko toka eti simu uta kuta wengi wao hapo hata ndala nyumbani kwao niza kuchangia hapana simu za mikono badala yake shule ichenge simu(call boxes) watakazo weza pigiwa over the weekend or their free time,shule ikiruhusu za mkononi ita ongeza wizi hapo shule na budget zaidi kwa wazazi
ReplyDeletenaona mnawasingizia tuu hao vijana,hayo madai naona yameletwa na mtu wa uongozi wa shule ili waonekane wakorofi tuu,hizi ni propaganda tuu za kuwanyamazisha na siamini hata kidogo,tunajua walimu wa bongo walivyo wapuuzi inawezekana wanawaonea sana tuu,vijana njooni muongee ukweli hapa ili hao jamaa waache kuwapakazia,kuna walimu wapuuzi sana na unaweza kuwachapa na lolote liwe na liwe tuu,njooni mseme shida ni nini na mtu yeyote aliywpitia shule za bongo hawezi amini kama ni kweli mnachodai ni uhuru wa kutoka usiku...nawapa benefit of the doubt na siamini hayo madai najua mnapakaziwa tuu njooni muweke ukweli wenu hapa
ReplyDeleteSimu ya mkononi mtoto was shule ya sekondari ya nini?It is distruction and waste of time to have a cellphone while in school. Nimesoma Weruweru 1999/2001 ilikuwa ni barua kwa kwenda mbele no simu. Ukihitajika kwa simu ni kwa mkuu wa shule na awe mzazi ndio anakuhitaji tena ni very rarely kuitwa kwa ajili ya simu. Halafu hawa watoto wanataka kutoka usiku kwenda wapi?wamekuwa wachawi au majambazi? embu wakae shule wasome na hizi ni dalili kwamba shule imewashinda hao.Wazazi na waalimu wapaswa kuwaelimisha watoto jamani.
ReplyDeleteHao wanafunzi wafukuzwe shule! Ni dawa yao! Eti waruhusiwe kutoka usiku, wanakwenda wapi? Na pia simu wanahitaji kwa ajili ya nini? Hebo!
ReplyDeleteMtu anayewalaumu hawa vijana hajasoma Bongo. Walimu wa Bongo ni very unreasonable. Pengine ni kwa sababu walioshindwa shule ndio huenda huko kwenye ualimu. Ni waonevu. Wana-enjoy kutesa watoto hata wa chekechea. Wanawapiga kama wanampiga adui vitani. Halafu sekondari mnapewa ugali maharage muhula mzima! Halafu ambao hamna uwezo wa kulipa tuition zao mnaadhabiwa kwa kutokufundishwa au kutokupewa notes nzuri km za tuition! Watu tulilazimishwa kulishwa chakula kimeandikwa "SPECIAL FOR PIGS". Chakula kimeoza. Ukisema unapigwa, unasimamishwa shule au unafukuzwa! Mtu akinifanyia hivyo muda huu, natoka na roho yake.
ReplyDeleteWadau acheni roho mbaya. Sasa km nyie mlisoma wakati hakuna simu mngepata wapi simu. Hawa wanasoma enzi za simu, wana haki ya kuwa na simu. Hawa wamezaliwa kukiwa na kompyuta, lazima wazitue pale inapowezekana. Hawa wanasoma kukiwa na internet lazima watumie internet. Tukubali kwenda na wakati.
ReplyDeleteBWIRE NA BUTMAN MPO KASAIDIE VIJANA-MAMBO YA AZANIA NA TAMBAZA YANARUDI
ReplyDeletemkemia mkuu afanye utafiti haraka wa bangi wanazovuta hao vijana zitakuwa zimechanganywa na poda, pia pusha wao afutiwe kibali
ReplyDeletekutoka usiku sikubaliani nalo la simu labda ni kweli manake walimu wanajua saaana kupakazia hasa wale walimu vihiyo taratibu za kazi hawazijui wao ni uonevu tu ndo ishu kama hizi zinatokea enyi form six mmebakiza mwezi na nusu tu mpige paper achaneni na vurugu mtihani upo kwenye kona february sio mbali december ndo hii inakatika kama mnataka kwenda ud mzumbe na vyuo vingine vyenye hadhi someni someni someni
ReplyDeletemdau canada
Siamini kama ni kweli madai yao ndiyo hayo. Simu pengine hata baba zao hawana na hiyo kutoka usiku wamekuwa misukule? Watoto wa siku hizi wanaweza kulilia kutoka usiku kwenda kufanywa mchezo mbaya ili wapate simu wanaacha kilichowapeleka shule ambacho ni kitabu kwa kwenda mbele. Sisi tuliopitia Box 2 shule ya wanaume Songea hatukuwa na upuuzi huo. Hiyo kama madai hayo ni ya kweli ingawa siamini ukweli wa madai hayo
ReplyDeleteHilo dai la mwisho la wanafunzi la kutaka kuruhusiwa kutoka nje usiku wala siliafiki na sidhani kama kuna mzazi anayemtakia mema mwanae ambaye ataliafiki. Ni madai ya kipuuzi sana.
ReplyDeletesitaamini...nasubiri taarifa kamili
ReplyDeleteHivi hao watoto wanawaza kweli au wanakurupuka tu? Sasa hiyo ndio sababu gani ya kufanya wagome?? Hawana Adabu kabisa hao tena ni wakupewa adhabu matata mno!!
ReplyDeleteUpuzi huo,ni shule gani inaruhusu simu hapa tanzania? na ni shule gani inaruhusu wanafunzi wa bweni kutoka usiku? Hao wazazi tu wanakukatalia ije kuwa shule!! Shule ni kusoma tu hayo mambo mengine wakafanye makwao.Wapewe Adhabu..
Kizazi kipya kweli!!
Bwana hii inasikitisha,nimesoma coment karibia zote hapo juu yaani ni sad.This is year 2009 about to be 2010,bado watu wengine wanaona cell phone ni anasa,nyinyi watu mnaishi dunia gani? utamkataliaje mtu kuwa na cell phone ati kwa sababu ni mwanafunzi,ati distruction,do you even hear your self?Well mimi nimesoma Dar- frm the begining to high school,wala haikuwa tatizo kwa mwanafunzi yeyote kumiliki simu ya mkononi,watu mliosoma Dar you know about this.Its stupid and if you don't suport them for having cellphones you also stupid and old fashioned.Let them have cellphones.Oooh ati sisi hatukuwa na simu za mkononi wakati unasoma,simu ya nyumbani haukuwa nayo iwe ya mkononi,i see wivu kwa sabu mwalimu hana simu them you are not alowed to have it either.Come on people its just cell phone so let them have it if they want to.
ReplyDelete