Mgeni rasmi Naibu Balozi Mh. Suleiman Saleh (katikati) akisaidiwa kukata keki na mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania Bw Mwesigwa na Meya wa jiji la Vallejo Bw Osby Davis huku kina dada wa kitanzania Bi Mwajuma Na Bi Pricilla wakishuhudia na kushangilia tukio hilo.
Mgeni Rasmi Naibu balozi wa Tanzania Washington DC Bw Suleiman Saleh akitoa nasaha zake

heshima zote wakati wimbo wa taifa ukipigwa
ni wakati wa mahanjumat..

keki ya uhuru day
Baadhi ya wadau waliohudhuria sherehe hiyo, kutoka kulia kwenda kushoto ni mdau Peter Glenn, Maalim Mrisho na Erick Rweikiza juu na chini ni wakati wa libeneke kusherehekea uhuru wa Tanganyika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mbona keki ina bendera ya Tanzania, wakati sherehe ni za uhuru wa Tanganyika?

    Kile kibabu Nyerere kimetuletea vurugu !!

    ReplyDelete
  2. Ndio, uhuru wa Tanganyika na sio wa Tanzania kama wanavyosema wale wasiojua mambo.

    ReplyDelete
  3. Sherehe kweli ilifana Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. Braza Michuzi mi naimba kutofautiana kidogo na hawa watu. Mi nafikiri hi bora hawa jamaa wange-organise kitu kama kilio hivi, kwamba wanasikitika nchi yetu miaka karibia 50 tangia tupate uhuru kila kitu kinazidi haribika badala ya kuboreshwa. Kilio chao kingekolezwa makali baada ya wahudhuriaji kuweka kongamano la kujadili mustakabali wa nchi yetu, hasahasa kwenye mambo ya kifisadi yasiyochukuliwa hatua yoyote, matumizi ya wabunge yasiyowiana na maisha ya watanzania wanaowapigia kura, ukosefu wa "the rule of law", na mengine mengi tu.

    Vilevile mimi naona bora Mjarumani angeendelea kututawala mpaka leo kwamba lazima angejenga reli nyingine na kuiboresha iliyokuwemo, maana mpaka leo hii reli yetu ya uhuru iko choka mbaya. Sisi wenyewe tunashindwa kuikarabati na hatijawahi jenga reli yoyote tangia tupate uhuru.

    Ni hayo tu ndugu yangu Michuzi. Naomba usibanie comment yangu kaka.

    ReplyDelete
  5. Hii keki ni sahihi kabisa kwani inaashiria kuwa Tanzania inaanzimisha uhuru wa bendera kama keki inavyoonyesha lakini bendera yenyewe ilitakiwa iwe ya Tanganyika.

    Kusema kweli Watanzania hawana haja ya kusherehekea sana kwani miaka karibu 50 sasa baada ya uhuru hakuna cha maana kilichofanyika ili kuinua kiwango cha maisha. Miaka 50 ni umri wa mtu mzima kabisa. Hali za maisha ya wananchi walio wengi zinazidi kuwa duni kila kukicha. Viongozi wetu wameshindwa kabisa kuwaletea wananchi maendeleo muafaka zaidi wamekuwa wanafanya siasa za kisanii na kujali interests zao binafsi badala ya kuweka utaifa mbele.

    Kwa mfano kwa kuwa uchaguzi utafanyika mwakani sasa wale wanaotaka kugombea ubunge wanaonekana kutembelea wananchi na kuwapa vicement na vibati eti wanachochea maendeleo. Hizi ni siasa za kisanii kwani wakati wote walikuwa wapi? Na uchaguzi ukiisha tu hawataonekana tena mpaka uchaguzi mwingine.

    Kuna mambo mengi ya kufanya Tanzania sasa kwani nchi ina matatizo mengi zaidi ya yaliyokuwepo wakati wa uhuru unapatikana. Hivyo basi kuna haja ya watanzania wanaoitakia mema Tanzania kujadili nini kifanyike na kuhakikisha kinafanyika badala ya kusherehekea kwani hakuna cha kusherehekea. Mtanzania wa leo hatasheherekea nini wakati hajala na hata kama amekula hana uhakika na mlo ujao. Mtanzania wa leo hatashehekea nini wakati hana maji ya kuoga baada ya sherehe na ya kunywa wakati wa sherehe.

    Seriously viongozi wa Tanzania wanatakiwa kuandaa kongomano ya kitaifa kujadidili ni kwani nchi hajapiga maendeleo katika kuinua maisha ya wananchi wake walio wengi miaka karibu 50 baada ya uhuru. Nchi za Asia zilipata uhuru miaka ya sitini lakini sasa zimepiga hatua kubwa kimaendeleo, Tanzania na inashindwa nini kufanya hivyo.

    Michuzi weka hii comments please na nakaribisha wadau watumie siku hii ya uhuru kutoa dukuduku zao.

    ReplyDelete
  6. Hongera Tanzania kwa kusherehekea miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika.

    Ni jambo zuri kutambua historia kamili ya Tanzania inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar.

    Tusione taabu kukubali kuwa asili ya Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar.

    Mdau
    Mtanzania

    ReplyDelete
  7. kinacho wafanya mchezeee kiivo ni nn hasa???ivi tunasherekeaga nn hasa jamani na ufedhuli huu uliowajaa hawa watu tuliowapa dhamana????

    mngeandika kwa kiswahili iyo siku ya uhuru ebooo,afu ni siku ya tanganyika

    inaboa kishenzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...