DJ RICHIE WA BONGO DJsTAARIFA KWAMBA NDUGU YETU MPENDWA ALMAARUFU KAMA DJ RICHIE WA BONGO DJ'S AMETUTOKA USIKU WA TAREHE 23 JANUARI 2010 KWA PRESSURE YA GHAFLA SI ZA KWELI, GLOBU YA JAMII IMETHIBITISHA.
HABARI HIZO, AMBAZO ZIMESAMBAZWA KILA MAHALI KWA NJIA YA SIMU NA MITANDAO, ZIMEKANUSHWA VIKALI SASA HIVI NA DJ RICHIE MWENYEWE BAADA YA GLOBU YA JAMII KUFANYA UTAFITI WA KINA KABLA YA KUZICHAPISHA.
"DAH! KAKA WALA SI KWELI KUWA MIMI NIMEKUFA, NA SIJUI NI NANI AMESAMBAZA HABARI HIZO ZA UZUSHI NA KWA SABABU IPI.
IMENISIKITISHA SANA KWANI NIMEPOKEA ZAIDI YA SIMU 200 TOKA KILA KONA YA DUNIA KUULIZIWA."NINACHOWEZA KUSEMA NI KWAMBA MIMI NAMWACHIA MUNGU ILA NASHUKURU KWAMBA NIKO SALAMA NA NINA AFYA NJEMA KABISA. PIA NAWATAKIA POLE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOPATWA NA USUMBUFU BAADA YA KUSIKIA HABARI HIZI ZA UWONGO.
"NINA WASIWASI KUNA MTU AMA WATU WANAOTAKA KUHUJUMU ONESHO LETU BONGO DJs WIKIENDI IJAYO AMPABO MIPANGO YOTE IKO SAWA NA ALI KIBA AMEKWISHATUA UK TAYARI KWA ONESHO HILO", ALISEMA DJ RICHIE KWA MASIKITIKO MAKUBWA ALIPOONGEA NASI KWA NJIA YA SIMU.


Kama sijakosea ndugu zangu haya ndio mambo yanayovuka mipaka kama vile binadamu.Kifo ni hitimisho ya maisha yetu katika ulimwengu wa kimwili na mwanzo wa kimaisha ya kiroho.Kifo ni taarifa ambazo kila mmoja wetu zitamgusa kwa namna moja au nyingine kulingana na mahusiano ridhawa na mlengwa.Kwa kweli inavunja moyo saaana kuona jinsi tulivyokosa maadili ya kijamii na kuvuka mipaka inayokiuka haki ya mtu kuishi.Kumzushia mtu kifo kwa sababu binafsi(labda chuki au wivu hasa wa kimaendeleo)ni upungufu wa kutumia busara za kibinadamu.Binadamu saa nyingine huombeana mabaya lakini siyo kifo asilani!.Ukiona mwenzako anafanikwa kimaisha usimchukie ila mvute karibu akupe siri ya mafaniko!!.
ReplyDeletedamn haters get something to do with your life loosers
ReplyDeletepole Richie,we got ya back
pamoja kaka
mdau Slough
DJ Richie utaishi maisha marefu. Pole sana lakini. Nadhani umekosa usingizi baada ya kusikia habari hizi!
ReplyDeleteNdugu yetu Richie mungu akujaalie maisha marefu! Hao wazushi ni wivu tu. Tupo pamoja siku zote...BF BOYS FOREVER!!!!!
ReplyDeleteMzee pole sana, wabongo nuksi. Isaac Mgwassa
ReplyDeleteBabu Richie watu wa Flats nini wamekuzushia.....au akina Shulwa nini?
ReplyDeleteduh wabongo noma, yani mnamzushia mwenzenu kufa kisa wivu wa show ya ali kiba?
ReplyDeleteBrother Richie pole sana .... Mungu atakujalia kuwa na maisha marefu zaidi ..inasikitisha kuwa watu wana wivu wa kijinga just for the Ali KIBA's Show . Hawajui kuwa u DJ hukuanzia hapo UK nakumbuka tangu miaka ile ya early 90's ulikuwa unachakarika kinoma i.e BF Boys parties chini ya kina Libe , Kaburu na Michael Jackson wetu bob Zeno. Keep it up bro .
ReplyDeleteNB ... inasikitisha mdau aliyemusisha Shulwa na habari hizi ... kijana wa watu hana hili wala lile ..chakula tu ni shida sasa hizi propaganda ataanzia wapi ..
Musa
Osaka ,Japan
DJ Richie, pole sana.
ReplyDeleteUkifanya kazi ya jamii kwa moyo wako wote, ifanye kwa nguvu zako zote...haya maneno maneno ni ya "marafiki" wanayoihusudu kazi yako nzuri na hawawezi kubuni wala kuboresha za kwao.
Vita ya maisha hupiganwa mpaka pumzi ya mwisho.Hakuna kilio cha upendeleo ktk mapinduzi ya kweli.
Adui wako akikusifia basi tafakari kwa makini kazi hiyo unayoifanya.
Matusi, Uongo,Fitina,Husuda na Uzembe ni Ufisadi vile vile. Endeleza 'MAKAMUZI', Usiogope MALIMWENGU kaka, lazima tuishi nayo ili tuboreshe WAJIBU wetu.
J'mosi kwa ALI KIBA mie tiketi yangu namba 1. Kamua sauti za kizalendo.
Maina A Owino.