Hii ndiyo hali halisi ya Kilosa makazi mengi ya watu bado yamezingirwa na maji shughuli nyingi bado haziendi vizuri kutokana na athari za mafuriko hayo yaliosababisha hasara ya uharibifu wa mali na maisha ya watu ambapo kwa sehemu kubwa wananchi hao wanaishi kwa shida.
Baadhi ya Mitaa ya Mji wa Kilosa bado imezingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na mali za wananchi na kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi.

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akitoka kukagua moja kati ya mahema ambayo yatatumika kama makazi ya muda kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa katika eneo la Kimamba alipotembelea Wilaya hiyo leo kuangalia kiwango cha athari na misaada inayohitajika.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo ya ujenzi wa makaazi ya muda toka kwa Mkuu wa wilaya ya kilosa Halima Dendegu katika eneo la Magomeni mjini Kilosa leo wakati Dk shein alipofanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko ambayo yameikumba wilaya ya Kilosa kutokana na mto Mkondoa kujaa maji ya mvua na kina chake kupungua.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiwafariji baadhi ya waathirika wa Mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa wakati alipowatembelea katika eneo la Magomeni jana ambako inajengwa kambi ya muda ya kuwasitiri wananchi hao ambao kwa sasa wamehifadhiwa katika ghala la kilichokuwa kiwanda cha mazulia Kilosa. Picha zote na mdau Clarence Nanyaro





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hiiii! kilosa nako bongo tambarale? ya kamanda ras wa ffu ya ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Wadau tulio nje tufanyeni harambee ya kuwasaidia ndugu zetu. Kidogo tutakachokusanya ni kikubwa kwa walioathirika.

    ReplyDelete
  3. GADAFFI ANATAKA KUWAJENGEA NYUMBA, NAZO MUWALIZE, MAANA MMEZOWEA HATA KIDOGO MNATAKA KUNYANG'ANYA MASIKINI WA WATU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...