Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka wa pili kulia, wakitembelea kituo kikuu cha kuzalisha umeme katika kijiji cha Rabai mjini Mombasa Kenya jana, wakati Makamu wa Rais alipokuwa katika mfululizo wa ziara yake ya siku tatu ya kiserikali Nchini Kenya. Kulia ni Mhandisi wa Mkuu wa Kituo hicho Peter Onail.
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kuzalisha umeme Mombasa Kenya Peter Onail kulia, akimueza jambo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipotembelea katika kituo hicho kuangali shuhuli za kiutendaji jana. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka.

Mama Mwanamema Shein akipokea zawadi baada ya kutembelea Mombasa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari mjini Mombasa Kenya Jemes M. Mulewa akimkabidhi zawadi ya Nembo ya Shirika hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania Dk.Ali Mohamed Shein, wakati Makamu wa Rais alipotembelea na kuangalia shuhuli mbalimbali zinazofanywa katika Bandari ya Mombasa jana.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kaka Michuzi Nasikia yule jamaa aliyemuomba Ngeleja atoke Kwenye ATM ili wengine wapate huduma kafukuzwa kazi ili mh.afurahi kweli hii ni sawa Wiliam Ngeleja muogope mungu aliyekuumba na kesho kuna kufa na kuzikwa mimi nawaonea watoto wa mshikaji huruma pamoja na mkewe lakini malipo hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  2. Mnaosema JK hatumi wasaidizi wake nje ya nchi si mnaona Dk Shein yuko hapo jirani.

    ReplyDelete
  3. Ha ha....ati JK hawapi wasaidizi wake safari za nje...sasa Kenya ni nje? Mbona asimpe safari za USA na Europe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...