Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akikata Utepe Kuashiria Ufunguzi wa Benki ya Federal Bank of Middle East (FBME) tawi la Zanzibar huko Kisiwandui Mjini Zanzibar katika shamra shamra za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Shoto ni Mwenyekiti wa FBME Farid Saab.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(kushoto)akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa tawi la FBME Fonal Majichia,baada kuifungua benki hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na wafanyakazi wa FBME Bank alipowasili katika ufunguzi wa Benki hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(kushoto) akipongezwa na watoto wa Skuli ya maandalizi wakati wa ufunguzi wa Benki ya FBME tawi la Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akifuatana na Mwenyekiti wa FBME Bank Farid Saab, mara baada ya kuifungua benki hiyo iliyopo Kisiwandui Mjini Zanzibar jana,na kutembelea sehemu mbali mbali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. unaacha kuwasha umeme watu wanalala giza hukoo ww ndo kwanzaaa unafungua vibanda vipyaa au kwa sababu ww unalala na umeme sio ndo hujali , but thanks kufungua hichoo kwani ndo maendeleo wenewee hayoo ba amanii sawaa mhhhh

    ReplyDelete
  2. It is a shame kwa viongozi wa Tanzania, bara Raisi anafungua hoteli na visiwani nako Raisi anafungua benki! Mwe!!! Mi nimeshachoka sasa.

    Hivi mawaziri siku hizi kazi zao ni zipi? Au na wao wachukue majukumu ya wabunge? Na je wabunge watafanya kazi gani? Bila shaka na wao watachukua majukumu ya madiwani, na hatimaye madiwani kuishia kufanya kazi za m/kiti serikali za mitaa. Kwa mchakato huu kiongozi wa chini kabisa ataishia kua mlezi wa familia za watu na hatimaye wazazi kujihisi kutokua na majukumu.

    Tunajua kabisa hatima ya mzazi kua irresponsible! Haya!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...