Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Omar Makungu akizungumza na waandishi wa jijini Dar leo wakati viongozi hao walipotangaza rasmi halmashauri za Wilaya na Mikoa kupeleka maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na tume hiyo kwa mikoa na Wilaya zinazoomba kugawa majimbo yao. Kulia ni Katibu wa Tume hiyo, Mh. Rajabu Kiravu.
Jaji Makungu ametaja Februari 28 2010 kama ndiyo tarehe ya mwisho kupokea maombi hayo, na baada ya hapo tume hiyo itapitia maombi hayo na kuona ni mikoa na wilaya gani zimekidhi na kufuata maelekezo ya tume hiyo ili majimbo yao yaweze kugawanywa.
Kwa mujibu wa Mh. Kiravu, gharama za zoezi zima la uchaguzi mkuu zimegawanyika katika awamu tatu ambapo uboreshaji wa Dafrtari la wapiga kura awamu ya kwanza uligharimu shilingi Bilioni 27 na awamu ya pili uligharimu shilingi bilioni 42 na uchaguzi mkuu utagharimu shilingi bilioni 64.

Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani hapo baadae mwaka huu na vyama mbalimbali viko katika pilikapilika za kujiandaa na uchaguzi huo baada ya awamu ya kwanza ya kipindi cha miaka mitano ya Rais Jakaya Kikwete kumalizika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. MUSOMA VIJIJINI IGAWANYWE IWE NA MAJIMBO MAWILI.

    WITO KWA WANANCHI:
    WAKATAENI WABUNGE WOTE WALIOPO SASA WA MUSOMA (MJINI NA VIJIJINI) MAANA WOTE WANA MATATIZO MAKUBWA.

    CHAGUENI WATU WENGINE WENYE ELIMU YA KUTOSHA, UZALENDO WA KWELI NA WASIO NA MADOA YA UFISADI.

    ReplyDelete
  2. hii ni njia ya kupata power kwa kuzipa viti zaidi sehemu ambazo unaona zina ku-support.

    ReplyDelete
  3. lazima iwepo njia nafuu kabisa hata mtoto wa chekechea afahamu. kwa mfano kila mkoa uwe na wabunge sawa na mkoa mwingine mbali ya ukubwa au idadi ya watu wanaoishi katika mkoa.
    Na mwisho chombo cha kuhesabu watu kiwe huru bila ya kuwa na uhusiano wowote na serikali au chama chochote cha siasa ili kugawa viti vya wawakilishi wa serikali za mitaa kulingana na idadi ya watu.

    ReplyDelete
  4. Hili ni jambo la kusikitisha , yaani kugawa majimbo kunakuwa na maombi ? ....This is plainly a prescription for corruption and cronyism. The govt must devise a a mechanism that will be impartial and will put under consideration the district's population. The govt is spending millions of dollars every decade for censors, they should those data..

    ReplyDelete
  5. idadi ya wabunge iliyopo imezidi na bado mnataka kuongeza majimbo, huu ni ufujaji wa hela za walipa kodi.Hapo bungeni kunatakiwa kuwepo na active MPS maana hata takwimu zinaonesha kuna baadhi ya wabunge ktk kipindi cha miaka mitano hawajawahi kufungua mdomo

    ReplyDelete
  6. Tume ya uchaguzi, Tanzania na watanzania ni muhimu kuliko chama chochote. Gaweni/ongezeni majimbo mapya kwa haki na usawa na simamieni uchaguzi na kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa haki bila kupendelea chama chochote.Umaskini tulionao unatosha tujihumie sisi na vizazi vyetu vijavyo.

    ReplyDelete
  7. Kuna umuhimu wa KUUNGANISHA majimbo ili kupunguza idadi ya wabunge tulio nao. Wanakula hela za walipa kodi bure. Sheria zinazotungwa ni mbovu ndio maana madini yetu yanapakuliwa bure. Wanashindwa kuikomalia serikali isiingie mkenge wa mikataba ya miundombinu-reli, ndege. Kukosa ubunge kwa wanene fulani fulani isiwe sababu kuongeza majimbo. Taifa lilipata maendeleo makubwa zaidi na wabunge wachache enzi za mchonga kuliko utitiri wa sasa.

    ReplyDelete
  8. OOH!! its alot of money kwa hayo machaguzi for poor country kama Tanzania,that money zingesaidia kujenga taifa na sio kuchagua tena walaji. its toooo much money!!!!!!,bilioni....bilioni...mbunge akikohoa bilioni..wakati mpaka leo watoto wanakaa sakafuni mashuleni???shame on you guys...!!!

    by mlalahoi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...