Nimekuwa mdau wa ankal kwa muda mrefu na kupitia chombo chake nimejifunza ni jinsi gani watz wanavyopenda kuona nchi yao ikitenda yale yanayotarajiwa kutendwa.
hayo hayatakuja bila sauti za watu zitakapoweza kusikakika.wengi wataniunga mkono kuwa vyombo vyetu vya habari havina makali ya kuinyoosha mifumo yetu.vina kasumba za woga.Ndugu yetu michuzi yuko tofauti mno ana mchango mkubwa sana ila tatizo ni kuwa habari zake ziko mtandaoni na wadau wa mtandao wakubwa ni diaspora na wakazi wachache.

Diaspora wengi sana wanapenda kufanya vitu vyao hapo nyumbani ila mara nyingi wanakata tamaa kutokana na system ya hapo nyumbani.diaspora wana exposure ambayo inaweza kuleta mabadiliko makubwa hapo nyumbani.Wazo langu ni kwamba mr ankal amekuwa sauti yetu sisi diaspora na mawazo yetu mara nyingi ni yenye nia njema na nchi yetu hivyo basi kwa kuwa naamini kuwa mtandao si reliable kwa kufikisha habari kwa walengwa kutokana na wengi kutopenda kupitia mtandao.
Nashauri ndugu zangu ma diaspora tujadili ni jinsi gani michuzi anaweza kuwa sauti yetu awafikie walengwa zaidi ya mtandao.

Mfano naamini kabisa tuna uwezo wa kumchangia bila masharti na akaweza hata kuanzisha gazeti la sauti ya diaspora inayoweza kuwa moto kwa upuuzi unaotendeka nyumbani.tukipigana tutarekebisha tu.ankal kutokana kuwa na exposure kubwa kwa mawazo ya watu anaowaandikia ndo maana tunamuona tofauti sana na waandishi wengi hewa.
naomba tu mnistahi na natamka ankal nimemjua kwenye mtandao tu na nimemuona mara moja tu alipokuja kwenye mkutano London tulipoanzisha ka mkoa ketu ka ughaibuni.so naamini hata hawezi nikumbuka ila ni kwa nia njema na nchi yetu na naahidi wadau wakipatikana wa kuunga wazo hili nitakuwa bega kwa bega kuchangia libeneke la sauti ya diaspora ili tuwe na mwelekeo kwani mwendo wetu hata kinyonga hatumkuti.
Naamini inawezekana kwani hata haiti hapa tunatoa tulicho nacho hatimae kinakuwa kitu kizima.
TUNAWEZA.
UMOJA NI NGUVU.
Mdau London.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ndugu mdau tunashukuru kwa wazo lako zuri, sote tunatamani mawazo yako yangetimia kwa vitendo. Lakini ujue blog ya jamii inaviewers zaidi ya 6Milioni naomba unisahihishe Bro. Misupu kama nimekosea idadi hii ni kubwa mno zaidi hata ya magazeti ya habari yanayonunuliwa kwa siku. Sio wananchi wote wanaosoma magati kila siku. Faida ya blogu hii ni inatazamwa kwa wadau wote duniani hasa majority wapo nje ya nchi, na habari zinafika kwa haraka sana kwa wale waliona access na mtandao. Huwa wakati mwingine ninashangaa huyu Bro Misupu anapata muda wapi wa kufanya haya mambo yote, mimi ni mtaalamu wa computer na katika masaa 24 angalau masaa 10 nipo kwenye matumizi ya computer, lakini kila ninapofungua blogu hii ninakutana na habari mpya iwe usiku iwe mchana na nipo nje ya nchi na tunatofautiana kwa masaa 8. Lakini tumekuwa tunapata habari mpya hata kabla ya watanzania waliopo nyumbani.
    Tuje kwenye wazo lako la kuanzisha gazeti huo ni mradi mwingine na masharti yake ni tofauti na blogu, jamaa watamzima kwani habari tunazozipata kwa blogu hii ni nzito na faida ni watu wanapata fursa ya kutoa maoni wanavyotaka. lakini kwenye gazeti hakuta kuwa na nafasi ya kutoa maoni yoyote. Ujumbe unawafikia wahusika direct na kama kujirekebisa wanajirekebisha right away.
    Ninavyofikiri tukimwingiza Michuzi kwenye biashara ya gazeti itamwia vigumu sana na kutakuwa na comflicts of interest hapo kwani tayari anamkataba na kampuni ya magazeti ya Daily News bila kukosea, ni process ndefu labda yeye mwenyewe aamue kwamba anajiengua kwenye mkataba alionao na hatujui kuna masharti ya aina gani. Labda tumuulize mwenyewe anaona vipi kuhusu swala hili.

    Binafsi nilishauri mwanzo tumnunulie vifaa more sophisticated vya kufanyia kazi hasa camera za digital na video ili aweze akatupatie habari katika video za High Definition na badala ya kuwa na blogu afungue website iliyochanganyika na blogu.
    Hilo ndo wazo langu la leo.
    Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  2. I BELIEVE IN MICHUZI THAT IS MORE THAN CAPABLE, EXPERIENCED WELL TRAVELLED, EXPOSED AND HE CAN DO INCREDIBLY IN MDEIA ARENA, AND NOT JUST A SMALL NEWSPAPER BUT EVEN RADIO AND TV HE CAN, BUT AS YOU HAVE SAID THE PROBLEM HERE IS MONEY, CASH, START UP CAPITAL, ALL IN ALL TO START A SMALL RADIO STATION OR TV CHANNEL EVEN FOR DAR COVERAGE IS ENOUGH AND IT DOES NOT NEED A COLLOSSAL AMOUNT OF MONEY, HE CAN START A RADIO/TV STATION EVEN AT HIS HOME FOR THAT MATTER. HOW TO GET THE MONEY FROM THE PEOPLE THEN IT IS A NIGHTMARE IN OUR TRADTIONAL, IT IS CLOSE TO IMPOSSIBLE TO ACCOMPLISH THAT, BUT WE CAN TRY, IT IS POSSIBLE. I REMEMBER GIVING THIS ADVISE TO HIM LONG TIME AGO.

    ReplyDelete
  3. Naona ni wazo zuri sana kama tukijiorganise tunaweza kuweka sauti ya kukemea maovu.kuna sauti zenye jumbe nzito humu mtandaoni na nina imani tunaweza kuboresha jinsi ya kufikisha ujumbe.Mimi naunga mkono hoja hii kama tukipatikana wadau nina imani tutachangia na tunaweza kutoa mfano kwa ndugu zetu wanaokanyaga haki zao kila siku.Naunga mkono ankal aanzishe account tumchangie ili apanue wigo wa kufikisha ujumbe hasa kwetu sisi tulio mbali atatuwakilisha vizuri sana.mdau nimekubali kuwa ni creative yenye manufaa makubwa.MDAU OXFORD

    ReplyDelete
  4. Wazo lako ni zuri, ila napingana na wewe kwamba bwana Michuzi ni mwandishi mzuri...hata yeye namchallenge na ni ukweli hata katakaa kwamba yeye si mwandishi mzuri wa kumtolea mfano,,

    Kwanza, professionally Michuzi ni mpiga picha na ameajiliwa na gazeti la serikali (analipwa na wananchi). Na sijawahi kusoma habari yoyote iliyoandikwa na Michuzi zaidi ya vichwa vya habari vikielezea picha flani

    Pili wanasema, ukitaka kujengea watu nyumba, jenga kwanza kibanda chako kama mfano then ndio ulete wazo la kutujengea nyumba. Kwa maana hiyo basi, Michuzi kama angekua mpenda mapinduzi (mfikisha kelele zetu) kama unavyomuelezea angekua ameshaonyesha kupitia magezati ya serikali.

    Tatu, Huko nyumbani kuna magazati lukuki, tatizo asilimia zaidi ya 80 ya wasoma magazeti wanasoma Habari za Udaku.

    Nne, tunaomba ushahidi wa kisayansi kwamba tukianzisha hiyo sauti ya "Diaspora" ni kweli kelele zetu zitafika!??.

    Tano, tuyaongezee makali magazeti yaliyopo kwani mengi yapo mtandaoni, tuchangie na sauti zetu zitafika, sio kuanzisha magazeti lukuki wakati yaliyopo bado hayajawa na makali. That means tunaweza kuyaongezea nguvu magazeti anayofanyia michuzi na sio kuanzisha gazeti lingine

    Mwisho, kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo i.e Michuzi endelea kutuletea picha za mnato zikiambatana na habari kwani ni kitu muhimu na ninakusifu kwa hilo, Na nyie wana Diaspora someni kwa bidii, kuna mambo mengi ya kujifunza kupitia mtandao na sio kila siku Kushinda Facebook na kuchapa starehe kana kwamba huko nyumbani teyari kuna maisha bora kwa kila Mtz.

    Ni Mtazamo Tu

    NB; Michuzi itoe mbele ya ukurasa na roho yangu itapona;

    "Desert Eagle,,H-City"

    ReplyDelete
  5. Mdau London una mawazo mazuri sana sana. Michuzi anaweza kabisa kutufanyia hilo ukweli unabaki kuwa sisi diaspora kama tutakuwa na nia basi sidhani kama yeye atakuwa na kusita kufanya hivyo ukizingatia hilo gazeti litakuwa na uwezekanao mkubwa sana wa kupendwa nyumbani sababu wengi watataka kuwa wanajua watanzania waishio nje wanasema nini na wana msimamo gani. hata kama litakuwa likiuzwa bado litanunuliwa tu ukizingatia baadhi yetu diaspora ni wasomi sana tu. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba wengi wetu tutakuwa hatupendi kutoa mawazo ambayo ni hasi sababu nimegundua wengi wetu tupo huku kwa neema ya serikali ya tanzania, kwani wapo watoto wa mawaziri wa zamani, wa sasa na hata viongozi wengi wa serikali kwa hiyo kwa aliye pata mkate wake kupitia neema hiyo usitegemee aunge mkono mawazo hasi nk. suala jingine ni kwamba michuzi utanisamehe kwa hili lakini ndugu yangu sijui ni kwakuwa ni muajiriwa wa serikali umekuwa ukitukatisha sana tamaa tunapotoa mawazo ya kupinga mambo fulani fulani katika suala zima la miongozo ya nchi yetu, labda unaogopa utafungiwa au sijui ni kwanini. ni vema ujue kuwa hii sasa ni dunia ya uwazi na ukweli, wewe hutapaswa kulaumiwa kwa mawazo ya watu kwenye mtandao wako, kama ambavyo huwa unasema mwenyewe kuwa ''Tarishi Hauwawi'' sasa woga wa nini?, wewe kazi yako si ni kurusha tu maoni labda kama yana lugha chafu isiyofaa kwa jamii waweza kuyachinjilia baharini lakini kama ni challenges, uwazi na ukweli ungekuwa unayaweka tu. mbona JF hawafungiwi au wanabidii?? jaribu kuliona hilo kaka michuzi. kuna siku nyingine ukiamkaga vizuri huwa unafungulia bomba maoni hasi yanamwagika lakini siku nyingine ukilalia sijui upande gani ni kuyachinjilia baharini tu maoni hasi sasa hiyo inatukatisha sana tamaa. vinginevyo wazo la mdau wa londoni ni zuri sana sana tulifanyie kazi, mimi ni mmoja nitakaye toa mchango wa kifedha mzuri tu kufanikisha hilo kama itahitajika kufanya hivyo na kama likuwa na uwazi bila uwoga basi litakuwa gazeti zuri sana. unalisajiri mtandaoni kunakuwa na mada watu tunachangia wewe una hariri na ku-sum up then unapata habari ya kuweka gazetini isn't???. tupenda pia kusikia position yako michuzi katika hili.. je unafikiri waweza kutufanyia hili??
    ahsante
    nawakilisha
    Mdau wa Pajazzzz+titizzz

    ReplyDelete
  6. Mdau umesema jambo jema sana, nadhani ankel anajitahidi sana, ingawa mapungufu hayakosekani lakini hiyo ni kawaida maana hata ktk comment yangu hii waweza pata mapungufu. Namsifu ankel maana anakubali kukosolewa na pia kuweka hoja wazi nadhani bila masharti. Sasa kuanzisha kagazeti ni wazo zuri sana ila nadhani pia yeye mwenyewe ankel aweke wazi dreams zako na pia aje na proposal ili wadau wa blog hii wajadili, naamini wasomaji ni wengi na mawazo mazuri yatapatikani, na tujivunie kufanya jambo kwa ajili ya nchi yetu!!!

    ReplyDelete
  7. Mimi nakuunga 'mikono' mdau niwazo zuri sana,ikiwezekana ankal Michuzi gombania hata kiti cha UBUNGE utapita tu kwani wadau tumekukubali,nahii itasaidia sana katika kuliendeleza libeneke.fikilia jambo hili mjomba tena ikiwezekana tuwakilishe sisi wa TEMEKE kwani tunakero nyingi sana.

    ReplyDelete
  8. naaam sana tunaongea ya maana naamini wegi wataunga mkono mimi mwenyewe nikiwa mshabiki na mpenda haki na ukweli uonekane ndugu yangu nimesubiri kusikia mabadiliko na mapya ya mwaka mpya watanzania tuko tayari wala hakuna mkono wa stop tuko tayariiiiiii

    ReplyDelete
  9. wazo lako ni zuri nami nakubaliana nalo,lakini wasiwasi wangu unakuja katika mambo yafuatayo:
    1.sina uhakika kama ankal(michuzi) atakuwa na ujasiri wa kuliweka hadarani gazeti hilo likiwa ktk makali hayahaya ya blog. kwani huenda wale wakandamizaji watataka kulisakama na kuingiza vipengele kama kawaida yao ya kutaka wasifikiwe hadharani kwakuwa hapa ktk blog wengi wao huwa hawafiki.
    2.inapokuwa gazeti litatakiwa kufuata taratibu za usajiri wa magazeti na hapo ndipo nadhani panaweza ingia mushkeli na kuwekewa kiwingu.
    3.kuna watu walikuwa moto sana akina jenerali ulimwengu lakini nakumbuka walizimwa kwa nguvu,je matumaini tuliyo nayo yanaweza fikia matunda kweli na ukizingatia wengi wetu humu tunatoa dukuduku zetu kwa anonymity?
    sina zaidi labda tupate maoni ya ankal na yeye anasemaje ktk hilo.
    mdau.

    ReplyDelete
  10. atafute kurasa awe anaweka hoja zinazotolewa na maoni yake. Hivyo ana print selected comments.
    hizo kurasa zinaweza kuwa zinabebwa ndani ya gazeti fulani ili kurahisisha usambazaji.
    issue ni mshiko wa kuandaa na kuchapisha

    ReplyDelete
  11. Mdau unachekesha kweli. Kesho na utaambiwa sio raia. Watu kama Prof Baregu ambaye ni msomi kuliko asilimia kubwa ya mawaziri wa baraza letu wananyamazishwa halafu wewe unajidanganya unaweza kutoa mawazo ya kujenga nchi ukasikilizwa.

    ReplyDelete
  12. Obama-KikwetelizedJanuary 18, 2010

    Wazo zuri na kwa ujumla Michuzi kwa asilimia kubwa ni Mtaalamu Mhabarishaji mzuri.

    Lakini swali je kwa kuhama kutoka Blogu na kuwa na gazeti unafikiri kusudi lako la kuwa na 'makali ya kunyoosha mifumo' litafanikiwa?
    Je unayafahamu vyema mazingira na sheria zinazodhibiti magazeti kuwa tofauti na blogu?

    Mwisho niseme kuwa pamoja na kumsifia, Kaka Michuzi si Malaika, binafsi na wachache pia aliwahi kutuminyia wakati hatujachafua hali ya hewa ama kwa makusudui au bahati mbaya. Kinachotakia akigundua kosa awe anaomba radhi ni kitu cha kawaida na kitamuongezea hadhi maana hata akina BBC, CNN, ITV, DW n.k nao huomba radhi wanapokosea.


    Mimi naona elimu ya uraia bado haijatuzama sisi wananchi wenyewe. Maana ukifika uchaguzi kwa nini tukubali kuhongwa na viongozi tunaowafahamu kuwa ni wabovu au wasio na sifa na kisha tunawachagua? Makali yaelekezwe kwenye vichwa vyetu na siyo magazetini au kwenye blogu!

    ReplyDelete
  13. tupo pamoja,tutachingia hii kitu.
    cha chandu-uk

    ReplyDelete
  14. watanzania tunakwama kwa kuwa na lakini.wadau ukitaka kuingia msituni angalia ushindi tu.Sauti ya diaspora ni kali itawaovercome hao jamaa tu.HAKUNA NJIA YA USHINDI UKISHAKUWA NA LAKINI.KAZA BUTI.CHANGIENI MAWAZO TUONE NI JINSI GANI TUTAWEZA.

    ReplyDelete
  15. KWanza mdau "Desert Eagle,,H-City" naku wawa, nakufagilia umeongea pointi zaidi ya pointi !
    pili ujue kwamba kwa kupitia mtandao ni vigumu kumshika mtu na kufungia blog bila kuwa na vizibitisho tosha.

    Tatu ni rahisi kwa mtu kupata habari katika muda wake na wakati anaotaka tofauti na gazeti amablo hata commentz mtu utakuwa unashindwa kutoa !

    Labda kwa mawazo yangu labda mdau ungeelezea na kupeleka nguvu katika gharama za internet na usambazwaji wa net katika nchi yetu ili kila mtanganyika aweze kuapata habari kwa urahisi !
    tunahitaji huduma za internet ziweze kuwafikia kila mtu na sio kuanzishwa kwa gazeti ambalo litafungiwa tu kwa jazba za wakiojuu !

    ReplyDelete
  16. michuzi anatupa sana habari nzito na wakati mwingine naogopa labda jamaa watampiga chini siku moja anakosoa bila kuogopa hata polisi ana wakosoa wanapo fanya mabaya. HONGELA SANA MICHUZI.
    NI MIMI FORTUNATUS MWAKIPESILE

    ReplyDelete
  17. Wadau mnafurahisha sana!!! naona wote mmekubadiliana na swala hili inabidi mjadala huu uendelee, sasa Anko Misupu itabidi usubiri kwanza tuone watu wangapi wanasupport swala hili kisha to sign petition ya kuunga mkono swala hili.
    Ila kwa wewe binafsi lazima utakuwa una mambo unayoyatamani kufanya katika maisha yako au mipango yako ya baadae itabidi ueleze nini unataka kufanya katika ulimwengu wa habari kisha wadau tujue tufanye nini. Tupo wadau wa damu katika nchi mbalimbali na tunautaalamu katika nyanja za information tutatoa mawazo ya kitaalamu. Kwahiyo unachotakiwa ni wewe kuwa wazi kwani unaelewa siasa ya Tanzania kwani upo kwenye system kwa muda mrefu.
    Tupe mawazo yako binafsi tunataka kusikia toka kwako umeshuhudia mwenyewe wadau tunavyokumind! Tunaipenda kazi yako na wewe anko upo down to earth! very generous na wote tunakuombea maisha marefu!

    Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  18. Mimi napinga suala hili kwa sababu ifuatayo: Sisi binadamu hatukawii kulaumu iwapo bro. michu hataripoti habari ambazo sisi tunazitaka ziwepo kweny hilo gazeti. Nasema hivi kwa kuwa sote tunaijua nchi yetu na sheria zake kuwa hazifuatwi. Na pia bro. michu hawezi kabisa kuandika habari ambazo anajua fika zitamletea yeye na familia yake matata, na tukumbuke kuwa bro.anafanya kazi serikalini(ehehehehehhehe) siendi mbali ya hapa nafikiri yeye anajua namaanisha nini. Jambo zuri abakie hapahapa atupe taarifa sisi tuliopo nje na tuchangie mawazo yetu kupitia blog yake.Naomba tuwe makini kwa hili.
    Wenu Mkulima hodari, Army.

    ReplyDelete
  19. MICHUZI ANGALIA SANA HAWA WATU WASIJE WAKAKUPONZA UKATILIWA MASHAKA URAIA WAKO, UKAFANYIWA JARIBIO LA TINDIKALI USONI. WEE TULIA TU JILIE VIKUKU NA JUISI YA NGANO. SEMA KITU KIKUBWA AMBACHO NINGEKUSHAURI NI.

    1. MAKE SHUA UNA DOKUMENTI ZOTE ZA URAIA

    2. WEKA SEKURITI KALI YA MAISHA YAKO

    3. ZENI ANZISHA HILO GAZETI LA KINOKO ILI WAKISHINDWA KILA KITU CHA KUKUFANYA WALINUNUE KWA PESA NZURI UENDELEE KUJILIA MIKUKU TARTIIIIBU.Kama sijaeleweka mtafute Gen Ulmwengu nayeye alitumia gia kama hiyo juzi nimemuona beach anakula mafao.

    ReplyDelete
  20. Nafikiri tunachohitaji Watanzania ili tuendelee ni kujenga mfumo wa kuinuka kiuchumi, kama gazeti ni mradi wa kiuchumi hapo sawa. ...na nguvu kubwa mojawapo kwa mfano ni kuanzisha unit trust (mutual fund)ambapo watu watakusanya ndguvu za pamoja kuwekeza, na baadae kuingia kwenye miradi mikubwa inayochukuliwa na watu wengine wageni.

    Muhimu tujenge uhusiano kati yetu (trust), wataanza wachache lakini nina uhakika baadaye tutakuwa na kitu kikubwa zaidi.

    Tuache udhaifu wa kulalamika na kuandamana kila tutakapokutana na vizingiti!! We should face all situations head-on, and then go on the other side stronger!!

    Otherwise, tutakuwa wanyonge daima na uwezo mdogo kiakili na kiuchumi wa kukabiliana na mazingira!!

    Poleni ndugu zetu wa Haiti!!

    ReplyDelete
  21. HAKUNA KUANZISHA GAZETI KWANI GAZETI LINA SHERIA NA KANUNI ZAKE. HIVYO ANKAL HATAKUWA NA UWEZO WA KUWEKA HOJA ZINGINE KUTOKANA NA KUBANWA NA SHERIA! HIVI HIVI TU MPKA KIELEWEKE!

    ReplyDelete
  22. Wazo zuri kabisa na linalotia matumaini kuwa wadiaspora ni wazalendo pengine kuliko hata marais wetu (nimepata shida kupata kipimo cha uzalendo!!). Hata hivyo, kama wadau walivyosema hapo juu, ni vigumu kwa ankel kuanzisha gazeti la kuwakosoa watawala! Lakini pia tukumbuke kuwa tayari yapo magazeti mengi tu yanayofanya kazi nzuri sana ya kuelimisha umma juu ya haki zao - kwa mfano RAIA MWEMA, MWANAHALISI,nk hata lile la ndugu Mjengwa KWANZAJAMII. Kama anony wa Mon Jan 18, 12:26:00 AM alivypendekeza, tunachoweza kumuuliza ankel ni iwapo inawezekana akaingia mkataba na mojawapo ya magazeti hayo ambapo angaa mara moja kwa mwezi ataandaa kijarida cha "WASEMAVYO WANA-DIASPORA" chenye muhtasari wa maoni mbalimbali ya wadau na kukiambatisha na gazeti litakalokuwa limekubali kuingia mkataba. Sisi tutachangia pesa za kukitoa hicho kijarida (kurasa kama mbili au nne tu za gazeti la kawaida).
    Mlalahoi
    Kwa mfugamafisadi

    ReplyDelete
  23. TATIZO LA TANZANIA SI KWAMBA WATU HAWAPATI HABARI KUNA MAGAZETI, RADIO, TV, NA ONLINEMEDIA ZA KUTOSHA. TATIZO NI KATIBA. KATIBA YETU INAMLINDA MTU MMOJA TU NCHI NZIMA AMBAYE NI RAIS. EBU FIKIRIA MTU MMOJA PEKE YAKE ANAATHIRI MAISHA NA MAENDELEO YA WATU WOTE? BUNGE NA MAHAKAMA ZINAMTUMIKIA YEYE. WABUNGE HAO HAO NI MAWAZIRI AMBAYE ANAWATEUA YEYE WATAFANYA KILA ANACHOKITAKA HATA KAMA HAKINA MANUFAA KWA KUOGOPA KUPOTEZA KAZI.MAHAKAMA NI KANYABOYA HAINA NGUVU YOYOTE,RAIS ANA DICTATE YUPI AFUNGWE NA YUPI AFIKISHWE MAHAKAMANI KWA SABABU ANAWEZA KUWAFUKUZA ASKARI POLISI YOYOTE YULE KUANZIA MKUU WA POLISI KWA MAANA ANA NGUVU HIYO.HAUTAWEZA KUENDELEA KAMA HAKUNA HAKI KWENYE JAMII. UTAENDELEA VIPI KAMA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WANATEULIWA NA RAIS? HAWAJUI LOLOTE KUHUSU MIKOA,WILAYA NA MAHITAJI YA WAKAZI WAO. VIONGOZI HAO WAKIJUA JINSI YA KUMRIDHISHA TU RAIS NA SI WANANCHI WANA UHAKIKA WA KAZI ZAO.
    EBU KUMBUKIA TUKIO LA MWAKA JANA (2009) KATI YA BOSTON POLICEMAN VS PROF.GATES VS PRES.OBAMA. ASKARI ALIDAI HAKUFANYA MAKOSA YOYOTE NA AKAKATAA KUOMBA MSAMAHA THAT "HE ACTED STUPIDLY" AS IT WAS SUGGESTED BY THE PRES.OBAMA.WAKAISHIA WOTE KUNYWA BIA KAMA ISHARA YA MAPATANO. NAJUA WENGI MTAKIMBILIA KUSEMA HAYO NI MAMBO YA MAREKANI LAKINI UKWELI NI KWAMBA KATIBA INAMLINDA KILA MTU NA HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.

    ReplyDelete
  24. Jambo usilolijua kama usiku wa giza....Michuzi nampenda sana personal lakini na yeye ni mmoja wa hao hao tu. Tuma comment isiyo na matusi wala nini lakini ina ukweli ndani yake haiweki. Hivyo kama nyie comment zenu zote zinawekwa huku basi hamuongei ukweli, mnapamba mambo tu. Comments nyingi sana ambazo hazina tusi wala nini lakini watu wanaspendi muda wao kueleza kitu, kusupport au kukanusha lakini zikiwa zimegusa anga zake haweki humu.

    by the way hata hii comment kama ikifika ni majaliwa lakini ujumbe umeupata...be fair my dear....Our country needs help, the people deserve to know the truth...IF YOU HAVE THE PLATFORM TO DO THAT do it with your all heart otherwise you will answer this to the person upstairs

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...