
Kaka Michuzi (Ankal) habari za kazi!
Mimi sijisikii vizuri Uwanja wa Uhuru hapa Dar es salaam Tanzania kuitwa “shamba la bibi” kwa sababu zifuatazo kimtazamo wangu: Bibi kimalezi si hodari(mkali) kwa wajukuu zake yeye akiamini ni kuwaonyesha upendo kumbe huwa anawaharibu kitabia.
Hii husababisha mali za bibi huyu kutumiwa vibaya na (wengi wa) wajukuu hawa. Kwa hio basi Uwanja wa Uhuru kuitwa shamba la bibi maana yake “Bibi” ni Serikali na “wajukuu” ni wadau wa uwanja huo hasa wale waohusika na usimamizi kimapato na utunzaji mali zake.
Hii inaleta picha kwamba mali na mazao kutoka hapo shambani (pesa) hazipo katika uangalizi makini na “wadau” hao wapo huru kuzitumia wapendavyo. Je hamuoni jina hili linaweza kuakisi (Reflect) ukweli fulani katika maeneo fulani kwenye uwanja huo? Je wahusika wa uwanja huo (Meneja wa uwanja, Mkurugenzi wa michezo wizarani na Waziri wa Utamaduni na Michezo) mnalionaje jina hilo? Mmeliona la kawaida kuburudisha mdomo au nanyi mnaliwaza kama nionavyo?
Sijui nani alilianzisha jina hili ila kwa vile upande wa pili lina tafsiri tete basi AMUENI WENYEWE kwamba halina madhara liendelee kutumiwa au kuwaelimisha wadau hasa “vyombo vya habari” kutolitumia tena. Huu ni mtazamo wangu, wadau naomba mchangie hoja hii.
Tena wengi wa waandishi hao ukiwauliza nini asili ya neno 'Shamba la Bibi' wala hawajui, kama kawaida yao wamekuwa kasuku bila kujali kufanya utafiti japo kidogo tu. Basi ndugu zangu wanahabari jina 'Shamba la Bibi' linatokana na hifadhi za taifa za wanyama ambapo enzi za ukoloni zilikuwa chini ya malkia wa Uingereza na ilikuwa mwiko kuwinda bila kibali. Hivyo kila mtu akawa anayaita 'Shamba la Bibi' (kwa maana ya Malkia)
Naomba kuwasilisha!
Mdau Mlaule DJ,
Arusha , Tanzania
Mdau naona umekosa kazi ya kufanya. Hoja gani hii?
ReplyDeleteMdau unaonekana uko free sana na huna kazi ya kufanya...garbage!
ReplyDeleteYani mdau kweli wewe bila bila! Pili nyie ndio mnaofeli mitihani kwani huwa mnapenda sana ku complicate maswali. Unaweza ukapewa swali rahisi kama 1+1=( ) na badala ya kuandika jibu mbili basi wewe utaanza kuaply LOG na CALCULUS!! Yani umeamua kuchukua maana tata baada ya maana rahisi! Haya bwana Good luck!!
ReplyDeleteThis is crap for real!
ReplyDeletewee hujui kuwa huo uwanja umeanza kuitwa hilo jina baada ya uwanja mpya wa Taifa kujengwa hapo pembeni yake?thats why ukabaki kuwa uwanja wa zamani wa Taifa a.k.a Shamba la bibi,sasa bado tuu hujapata uhusiano wa maneno "wa zamani" na "bibi"?
acha kukomplikate mambo mdau,chukua jembe ukalime,nchi inataka maendeleo na sio kudiskas utumbo usio na maana!
Ninachojua mimi maneno 'shamba la bibi' lilikuwa linamaanisha National Parks wakati Tanzania ikitawaliwa na Mwingereza chini ya Malkia. Kwa sababu maeneo yale yalikuwa yanamilikiwa na Malkia ndiyo yakawa yanaitwa Shamba la Bibi. Shamba ni mbuga zenyewe za wanyama na Bibi alikuwa Malkia mwenyewe. Hiyo ndiyo maana iliyokuwa rasmi ya shamba la bibi. Sasa siku hizi hata mimi sielewi maana yake.
ReplyDeleteNashukuru Mdau kwa kuleta hoja hii, kwani kila mtu anao uhuru wa kuzungumza!
ReplyDeleteIla hoja yangu mimi ni pale viwanja vyetu vinapowekwa "nyasi bandia". Hivi kweli wenzetu wa SUA wameshindwa kutusaidia katika hili? Jamii (Species) zote za majani tulizonazo kweli wameshindwa kufanya utafiti na kuja na better solution?
Wenzetu ughaibuni kila kukicha wanafanya utafiti kupata better solutions za kupunguza gharama na kuwaongezea sifa duniani. Chukua mfano wa katani na nylon; ni miaka michache tuu nyuma walikua wakitegemea katani kutengeneza kamba. Lakini sasa ni tofauti, na mbaya zaidi na sisi ndio wakwanza kutumia vya kwao.
Kama maoni ya wengi wanavyosema, Watanzania TUBADILIKE! Tuachane na kulalama, na tusikubali kuwa watumiaji tuu.
Mdau Ireland