Juma Kaseja
SWALI: Unadhani kwa nini wachezaji wengi wa Tanzania hushindwa kupata vilabu vya kuchezea soka la kulipwa nje?

JUMA: Si wachezaji,bali waliotutangulia nyuma hawakuwekea misingi mizuri ya sisi kuweza kupita kwa hiyo mimi ninachoshukuru mungu,kizazi chetu sasa hivi kidogo kimefungua njia ina maana wanaokuja nyuma yetu sisi watakuta misingi mizuri ambayo sisi tumeijenga ya wao kuweza kupita. Ukiangalia nchi za wenzetu zina mawakala tangia miaka hiyo lakini sisi ndio kwanza miaka miwili hii ndio mawakala wameanza kujitokeza kwa hiyo mimi nasema misingi haikuwa mizuri nyuma,lakini sasa hivi kidogo naona mwanga umeanza kuonekana wapi tunaenda.

SWALI: Unazungumziaje kiwango cha Timu ya Tanzania “TAIFA STARS” tangu ilipoanza kufundishwa na mbrazil Marcio Maximo?

JUMA: Mimi naona kuna mabadiliko tena makubwa sana,kwa sababu mimi nakumbuka kipindi cha nyuma timu ya Taifa ilikuwa haipendwi, ikiwa inacheza mechi timu ya Taifa unaweza ukahesabu watu lakini sasa hivi Timu ya Taifa ikicheza inajaza uwanja, na hata performance imebadilika ya Timu ya Taifa.

SWALI: Kwa maoni yako unadhani Tanzania kunaweza kupatikana kocha atakayefundisha Timu ya Taifa na Kuonyesha mafanikio?au lazima kocha atoke nje?
JUMA: Makocha wapo. Kuna uzuri wa kuwa na kocha mzawa na kuna uzuri wa kuwepo kocha kutoka nje ya Tanzania. Kocha mzawa sidhani kama atapewa facility ambazo anapewa mwalimu wa kutoka nje kwa hiyo hicho ni kitu kikubwa kinachoweza kumwangusha asifanye vizuri kama wanavyofanya vizuri makocha kutoka nje.
Kupata intavyuu yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...