Umoja wa watanzania hapa uingereza umekuwa ukifanyiwa tathmini kwa muda ili kuuwezesha kuwa na mwelekeo na mfumo wenye kuleta hamasa, uwazi na ufanisi zaidi katika kutumikia jamii ya watanzania hapa UK.
Kamati kwa ushirikiano na ushauri wa wadau(wanajamii) imeweza kufanya kazi kubwa ya kuleta maono na mwelekeo utakaokuwa na ufanisi zaidi katika kuwatumikia wanajamii wote hapa UK kwa kipindi hiki.
Kamati imeweza kuangalia na Kupendekeza kurekebisha sehemu zote muhimu zilizohitaji marekebisho ili kuleta ufanisi zaidi nazo ni kama zifuatazo:
• Muundo
• Uwakilishi
• Katiba ya Umoja
• Mwelekeo wa Umoja
• Mfumo wa Uongozi wake.
Hawa ni baadhi ya viongozi wa jumuiya mbalimbali za kitanzania hapa UK wakijadili mapendekezo ya mwelekeo mpya wa jumuiya ya watanzania hapa UK.
• Umoja utahakikisha unaendelea kujifunza; na kuwa wazi katika utendaji wake; kuwaelimisha na kuwawezesha wanajamii wake,ili waweze kuwa sehemu ya mabadiliko na ufanisi katka jamii yetu.
• Mabaadiliko ndio itakuwa changamoto yake: ili kuwa makini kukidhi mahitaji wa wadau wake.
• Umoja utahakikisha unawawezesha wadau ili kuchochea umiliki na uwajibikaji wa wadau katika kuendeleza Umoja wao.
• Utahakikisha unafuatilia, unatambua, kutoa nafasi na unatumia vipaji vyote vilivyo ndani ya watanzania ili kujiendeleza.
• Umoja utahakikisha majukumu ya viongozi(uongozi) yanaainishwa kwa uwazi ili kuondoa miingiliano ya utendaji unaoleta mafarakano; na pia utaweka utaratibu wa kiutendaji utakaokuwa makini kulenga manufaa yawadau wake wakati wote.
Hawa ni baadhi ya viongozi wa jumuiya mbalimbali za kitanzania hapa UK wakijadili mapendekezo ya mwelekeo mpya wa jumuiya ya watanzania hapa UK.
Tafadhali watanzania au viongozi wa jumuiya za kitanzania waishio miji ifuatayo, Tunaomba mawasiliano ili tuweze kupata watu watakaokuwa tayari kufacilitate uanzishwaji wa Umoja wa watanzania katika miji yenu.
Cardiff, Milton Keynes, Belfast, Glasgow, Northern Ireland, Norwich, G. Manchester, Portsmouth, Southampton, Leicester, Dublin, Birmingham, Luton Slough, Coventry, London
Scotland, Westmidlands.
Tunaomba muwasiliane na kamati hii ya Umoja wa watanzania kupitia:
Email: Uniting-Communities@yahoogroups.com ,
au Simu zifuatazo:
Coordinator: 07766168471,
Secretary: 07908010344,
Members: 07799212095,
or 0788841971
Tafadhali anagalia kiambatanisho kwa habari zaidi.
Taarifa ijayo itaambatanisha repoti ya kamati ya taskforce
Asanteni
Umoja wa Watanzania UK
Kwa habari zaidi tafadhali


JAMANI NINA USHAURI NA SIJUI KAMA MTAUTILIA MKAZO. UJUMBE KWANZA KWENU NYIE VIONGOZI WA HIYO TASKFORCE NI KWAMBA CHAMA KILIISHIWA NGUVU KUTOKANA JAMBO MOJA KUBWA LA KUSHINDWA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE NA KUKIZI MAHITAJI YAOLE WANAPOYAHTAJ.
ReplyDeleteKUTOKANA NA SABABU HIYO KILA MJI UKAONA NI BORA KUWA NA VYAMA VYAO AMBAVYO WATAWEZA KUWASILIANA NA KUTATUA MATATIZO YAO KWA URAHISI ZAIDI NA KUONGEZA CHANGAMOTO, HIVI VYAMA VIMEWEZA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA NA VINAZIDI KUKOMAA NA VINGINE VIMEFANYA MAMBO MAKUBWA MNO. SASA HAITAKUWA RAHISI KWA WAO WAJE WAANZE UPYA, WAJE WAJIUNGE NANYI WAKATI KATIKA VYAMA HIVI VINGI VINA KATIBA ZAO ZINAZOWEZA KUKIDHI MAHITAJI NA SHIDA ZAO.
NYINYI MLICHOTAKIWA KUFANYA NI KUANDAA KATIBA AMBAYO ITAKUWA NA MFUMO TOFAUTI NA MNAVYOFIKIRIA NYINYI WA KUWAONGANISHA WATANZANIA UINGEREZA NZIMA.KWA USHAURI WANGU MNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUWAITA VIONGOZI WA VYAMA VYOTE VYA WATANZANIA HAPA NCHINI NA KUFANYA UCHAGUZI NA KUUNDA KAMATI KUU AMBAYO ITAKUYOWEZA KUWAKILISHA WATANZANIA WOTE NA VYAMA VYAO. HII KAMATI KUU KAZI YAKE ITAKUWA KUWAKILISHA TU NA KUACHA KILA CHAMA KIENDELEE NA SHUGHULI ZAKE NA KUJIENDESHA VYENYEWE.NA NYIE HAPO LONDONCHUKUENI CHANGAMOTO HII ANZISHENI VYAMA VYENU HALAFU MJISAJIRI KWENYE HIYO KAMATI KUU.
LAKINI MKITAKA CHAMA KIMOJA NCHI NZIMA KWA MFUMO UPI MLIYOKUWA NAO YA KUWAWEZESHA KUMTENDEA HAKI SAWA MWANACHAMA WA BELFAST NA LONDON WAKATI VIKAO VYOTE VITAKUWA VINAFANYIKA LONDON.
TUNACHOTAKA NI KAMATI KUU YA WATU WACHACHE ITAKAYOWEZA KUWAKILISHA WATANZANIA WOTE NA VYAMA VYAO. IWE KAMATI HURU NA VIONGOZI WATOKE KWENYE VYAMA VYA MIJI NA NYIE LONDON MUUNDE CHAMA CHENU ILI VIONGOZI WENU WAPATE NAFASI ILIYO HURU WAWEZE KUCHAGULIWA KWENYE HIYO KAMATI SAWA NA KAMA LONDON MNAONA KUBWA CHAGUENI KWA POST CODE HALAFU VIONGOZI WAO WATAPATA NAFASI ILIYO HURU KABISA KUCHAGULIWA.
KAMA MTANAHITAJI UFAFANUZI ZAIDI TUMA POST HAPA HALAFU NITAJARIBU KUFAFANUA ZAIDI KWA MANUFAA YA WOTE
ASANTE, MDAU BUCKINGHAMSHIRE
Very interesting; it's a big task to accomplish all this...
ReplyDeleteI wonder where the money to run this Umoja will come from..??!!
Walisema "subira huvuta kheri" mimi nasubiri.
NE,
Reading, UK
Ndugu zangu watanzania tuache utumwa wa kifikra, nyie mnaongelea umoja wa watanzania lakini hata minutes tu za vikao vyenu mnashindwa kuziandika kinyumbani? Kulikuwa na ulazima gani wa kuziandika kwa lugha ya kingereza?Kwanini hamko proud na lugha yenu?
ReplyDeleteKana-Ka-Nsungu
Mimi nina swali moja tu kwa hizi kamati au vyama vya Watanzania waishio mataifa mbalimbali hapa Duniani-Uingereza ikiwa mfano mkubwa. Nini madhumuni ya hivi vyama?? Natumaini wahusika watanijibu kupitia Globu ya jamii kwa faida ya wengi. Ahsanteni.
ReplyDeletenow you are talking!
ReplyDeletewe don't want to hear associations with political inclinations like that of Maina
watanzania kwa siasa na vyama huwatoi. Hata nje ya nchi! Huku kuna mambo kibao ya maana ya kufanya, wengine mmekomalia vyama tuu?
ReplyDeleteMtanzania hata ukimpeleka antactica utasikia amefungua tawi la umoja wa vijana wa CCM... du!!!
ReplyDeleteNini ubaya wa lugha yetu ya Kiswahili. Nimesoma ripoti ya PRESENTATION FOR TA-UK na kuona hiki kipengele kina utata wa lugha ambayo nilishindwa kuendelea kuisoma ripoti yote kwa kuchanganyikiwa na kushindwa kuamini kwamba kimetoka kwa wale wanaodaiwa kuwa viongozi "TA-UK is a unification of all Tanzanian voices into one, so as when it speaks, it is all Tanzanians have spoken. It is a voice that could speak for them nationally on national and strategic issues." Ushauri wangu ni mdogo: Tumieni Kiswahili. Hasa pale ambapo lugha mnayotaka kuitumia kwa kuonesha kwamba mmesona na kufaa kuwa viongozi, inawapiga chenga.
ReplyDeleteMy dear friends! what is wrong with us ? Let me remind you that so long any language such as english is not your mother tongue-it is obvious and understandable to make some errors when you have to use it. It is absurd to assume that any educated person should have a good command of a foreign language (in this case- english language), no, this is absolutely false.
ReplyDeleteA graduated person in mechanican engineering here in UK cannot have a good command of english language like some one who have graduated in linguistic! But this should not be an obstacle to those who still want to use an english as a means of communication in order to improve it.
I am very sorry for those who are using their time just to find out whether the written reports contain some errors based not on the contents but merely on the fact that any foreign language has its difficult.
There you are my friends.
Mdau hapo juu umesema Watanzania hata wakikutana wawili tuu Antactica wataanzisha chama na michango, halafu watapika maandazi na chapati na pilau. Hapo kwenye picha hukawii kuona maandazi.Jamani kashangaeni mahekalu ya malkia na Oxford huko acheni uswahili. KIDUMU CHAMA!!
ReplyDeleteAsanteni sana wadau watanzania wenzangu, ambao mmechukua muda wenu kutoa feedback kuhusiana na umoja wenu. Kila feedback ni ya muhimu, na pls waacheni watu waseme kilichoko mioyoni mwao.
ReplyDeleteLakini tujue tumekaa sana kwenye shida, muda umefika wa sisi kujikwamua.
Tuambie unataka nini, na nini kifanyike na wewe utafanya nini ili kuchangia maendeleo ya jumuiya yako hapa uingereza, hakuna watu fulani au viongozi watakaoleta mabadiliko.
Kama hutushiriki na kuchangia maendeleo ya umoja wetu huu, nani atafanya; wenzetu wanajua umoja ni nguvu ndio maana wanashirikiana, ni vizuri nasi tukalijua hilo.
Ni only our strengths kama watanzania ndio zitatupeleka mbele na sio our weaknesses. Ni vizuri tukaangalia ni zipi halafu tuka-dwell on them, badala ya kukazia matatizo yetu, though ni vizuri kuyajua ili tuyatatue.
Asanteni, tuendelee kushirikiana pamoja tunge nchi yetu
MDAU BUCKINGHAMSHIRE na wengineo pia .
ReplyDeleteAsanteni sana kwa feedback zenu, zote ni za maana na muhimu kwetu sote.
Tafadhali tunaomba mawasiliano zaidi kwenye e-mail hii: Uniting-Communities@yahoogroups.com
Tunatamani kufanya kazi na watu wengi wenye ushauri mzuri, na wenye moyo wakuona watanzania tunaendelea mbele.
Tafadhali wasiliana kamati.
Asante.
hasani nimekuona, nimekubali unatuwakilisha, kidumu chama popote pale antacrtica kiwe wapi kitadumu tu, hamna ujanja
ReplyDelete