Profesa Mwesiga Baregu (kuume) akiwa na Tahir Haroub Othman katika hafla ya kuadhimisha maisha ya hayati Profesa Haroub Othman mwaka jana ukumbi wa Nkrumah Hall jijini Dar

Siku za karibuni Wizara ya Utumishi kupitia Waziri Hawa Ghasia imelalamikiwa kuwa imemnyanyasa Profesa Mwesiga Baregu, kwa kumsitisha ajira yake UDSM kwa sababu za kisiasa.

Sijui kwa nini Waziri alaumiwe huku Waraka uko wazi kuhusu mipaka na nafasi ya watumishi wa umma katika kushiriki mambo ya siasa ambayo haina budi kuzingatiwa kwa ukamilifu na kila mtumishi wa Umma.
Waraka huo umeweka bayana Watumishi wote wa umma wanapaswa kutambua na kuzingatia maadili ya msingi ya utumishi wa umma ambayo ni yafuatayo:-

Kutekeleza wajibu wao kama watumishi wa umma bila upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha siasa (Political Neutrality/ Impatiality)

Kuwa na utii kwa serikali ya chama kinachotawala(Loyalty) kwa kutekeleza kwa dhati na ufanisi Sera za Serikali. Hiyo serikali ni ya Chama kinachotawala.
*Kutoshiriki katika mambo ya siasa yanayozuia utendaji mzuri katika vyombo vya umma.

*Kutoa huduma kwa misingi ya haki.(faireness)

*Kufanya kazi kwa hekima na uadilifu.(intergrity)

*Kutunza siri za serikali, Serikali za mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma(confidentility/secrecy).

*Kuheshimu maadili ya taaluma(proffessional ethics).

Watumishi wa Umma wanaruhusiwa kushiriki katika mambo ya siasa kama wakipenda. Hata hivyo, kwa kuwa hakuna haki isiyokuwa na wajibu wala uhuru usiokuwa na mipaka, watumishi wa umma wanaruhusiwa kushiriki katika mambo ya siasa kwa utaratibu maalum ili kuhakikisha kwamba wanazingatia maadili hayo.

Sasa swali hapa ni je Profesa Baregu kama mtumishi wa umma aliye chini ya mkataba baada ya kustaafu amezingatia masharti hayo? Kama hapana basi Ghasia yuko sahihi. Ghasia kama Waziri ni wajibu wake kuhakikisha maudhui ya Waraka yanazingatiwa. Lakini kama ni Waraka ndiyo unaolaumiwa basi hilo ni suala lingine. Ila tusisashau Waraka huo umekuwepo tangu mwaka 2000.

Kwenye jambo hili Profesa Baregu katendewa haki. Lakini iwapo Profesa Baregu angekuwa bado hajafikisha umri wa kustaafu kwa maana ya Waraka huo bado angebanwa nao. Kwa sababu yeye kama mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA bado anabanwa na kanuni za utumishi.


Suala la kuwa Waraka umepitwa na wakati huo ni mjadala mwingine. Lakini huyu mtumishi wa umma ni yupi? Nauliza hili swali kwa sababu baadhi ya watu wamekuwa wakiamini mtu yeyote afanyaye kazi serikali ni mtumishi wa umma.

Kwa maana ya sheria na kanuni mtumishi wa umma (Public Civil Servant) ni Kuanzia Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Makamishna, Maafisa mbalimbali hadi mhudumu wa ofisi iwe Serikali Kuu au TAMISEMI.
Lakini pia lipo kundi la watumishi katika kundi la wanasiasa ambao hawana sifa ya watumishi wa umma na hawa wanayo masharti yao tofauti. Hawa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri,Wabunge, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Kwa hiyo wale wanaodai kuwa mbona wapo mawaziri ambao ni watumishi wa umma lakini ni viongozi wa siasa kama akina Chiligati na Mkuchika na wengineo. Hao huo Waraka hauwahusu. Ndiyo maana wako baadhi yao walikuwa wameajiriwa serikalini ilibidi wajiuzulu huko ili wachukue nafasi zao za kisiasa.

Wale wanaodai kuwa Waraka ule alioutumia Ghasia umepitwa na wakati labda wanayo hoja. Kwa mfano mtumishi wa umma ambaye ni mwanachama wa CHADEMA atawezaje kutii kipengere kinachohusika sharti na kutunza siri za serikali, Serikali za mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma(confidentiality/secrecy).
Huyu katika hali halisi hawezi kwa vile atavujisha tu siri. Ndiyo maana haishangazi unaposikia mtu kama Dr Slaa anatamba kuwa yeye siri za serikali anapelekewa. Japokuwa iko sheria ya Official Secrecy Act utekelezaji wake umekuwa haufanyiki.

Nakaribisha mjadala wa suala hili.
ADILI na NDUGUZE
Soma tamko la serikali juu ya Profesa Baregu
Soma wadau wanasemaje juu ya hiyo ishu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. DAS(disrict administrative escretary), daktari wa wilaya, mhandisi wa wilaya, afisa elimu wa wilaya, wafanyakazi wote wa serikali hawatakiwi kuhudhuria mikutano ya kisiasa.

    Mfano waziri akitembelea wilaya fulani na kuitisha mkutano wa hadhara kuona kama sera za chama tawala zimefanikiwa jimboni, watumishi wa serikali waliotajwa hapo juu hawatakiwi kuhudhuria mkutano huo kwa mujibu wa waraka huo wa utumishi.

    Ila waziri anaweza kutembelea ofisi za serikali na idara hizo jimboni kujadiliana na watumishi juu ya mafanikio, mapungufu au changamoto mpya.

    Hivyo kwa tafsiri hiyo, kukiwepo mkutano wa hadhara wa kisiasa, mtumishi wa serikali haruhusiwe kuhudhuria, kuhoji mbele ya kadamnasi ya mkutano wowote wa kisiasa.

    Naamini watumishi wanaweza kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Lakini mtumishi wa serikali kushiriki kikamilifu kuandaa mkutano wa kisiasa mfano ziara ya waziri jimboni ni makosa kufuatana na waraka huo.

    Hivyo kutokana na sakata la Prof. Baregu, tutaona mabadiliko makubwa kwa idara kuu ya utumishi serikalini kuwabana watumishi wote wa umma, kutoandaa, kushiriki, kuhamashisha, kusaidia mikutano ya kisiasa iwe ya ndani au ya hadhara.

    Kiongozi wa kisiasa akitaka kujua ufanisi wa sera, basi awafuate watumishi wa serikali ktk maeneo yao ya kazi kama shule, hospitali, idara za kilimo. idara ya umwagiliaji n.k na sio kuwaita katika mikutano ya kisiasa ili watumishi wapande jukwaani kujieleza.

    Mdau
    Mtumishi Makini wa Umma.

    ReplyDelete
  2. ADILI NA NDUGUZEJanuary 16, 2010

    Ndiyo maana nikasema kuanzia Katibu Mkuu Kiongozi hadi mhudumu wa ofisi. Kwa hiyo DAS na hao uliowataja wako ndani ya range hiyo.

    Ni kweli hawatakiwi kuhudhuria mikutano ya kisiasa kama unahusu masuala ya siasa. Ila kama unahusu utekelezaji wa Ilani ya CCM itabidi wahudhurie siyo kwa maana ya kushiriki bali kwa maana ya kuchangia kwenye agenda ya Ilani.Kwa vile wao ndio vehicles of implementing hiyo Ilani. Wanahudhuria kwa madhumuni ya kutoa ufafanuzi pale wanapotakiwa kufanya hivyo. Ikimalizika na yeye anatoka nje ya kikao.

    ReplyDelete
  3. tanzania ni nchi ya ajabu sana,hasa pale swala husika linapo husu mtu aliye nje ya system(nje ya serikali na chama chake kwa pamoja).
    hapa zitatautwa sheria na vipengele vya kuhakikisha mtu huyo anabanwa na kuwajibishwa kisheria na waraka etc.lakini ikifikia wakati serikali ndiyo inapaswa kujibu/kuwajibika mbele ya wananchi wake bila kujali itikadi zao,hapo zitatafutwa sababu zote za kukwepa na sheria zitasemwa zimepitwa na wakati,na ushahidi uan tafutwa,ect.
    naomba niulize swali langu hapa:
    serikali inaruhusu watumishi wa umma kuhudhuria vikao vya vyama vyao lakini wasitoe opinion zao,sasa nini maana ya kuhudhuria kikao?nikukaa na kusikiliza tu then kuondoka?hii si ndiyo beaurocrassy?
    2.ccm chama tawala,na serikali yake vimekuwa vikiwatumia watoto walio na umri chini ya miaka 18 katika siasa na kuwavisha sare za chama badala ya bendera ya taifa,wakiwaita chipukizi. sasa hebu tuseme ukweli,tukiingia katika sheria za nchi na haki za watoto duniani huu sio ukiukwaji? je kama ni uvunjwaji wa haki nani anapaswa kushughulikiwa ktk hili?
    kwanini wasifundishwe uraia na sio kuingizwa ktk makundi ya kisiasa wakiwa chini ya umri usiowaruhusu kushiriki siasa?
    hebu tuache kufunika macho na kutafuta tu vipengele kwa ajili ya kuvitumia kwa faida fulanifulani za watu fulani walio katika nyadhifa fulani kudhoofisha wengine hadi kuathiri pia sehemu nyeti kama elimu.
    mimi siko katika siasa maana si mwanachama wa chama chochote wala sihitaji kuwa,lakini napenda kuyaangalia mambo kwa mtizamo wa kimaendeleo maana siasa za afrika ni uchuro mtupu kwa faida za wachache waliotayari hata kupiganisha watoto wadogo ktk vita na chuki wasizo zijua chanzo chake.
    mungu ibariki afrika,mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  4. Bongo bana kila kukicha ni masakata ya kijinga wakati wenzetu wanasonga mbele!Oh sijui nyumba ya gavana,hapa ngeleja na madudu yake,pale sijui Ghasia kamkomoa Baregu kwa niaba ya CCM,kule sijui nini? na mengineyo meengi, yaani sijui tukoje?
    Baregu atapata kazi ughaibuni kwa vile wanamjua alichonacho kichwani.
    Sasa hapo kakomolewa nani?
    Halafu JK anawashawishi wataalamu wa kibongo wenye kazi zao nzuri nje ati warudi kwenye huu utumbo!
    Ama kweli bongo tambarare!!

    ReplyDelete
  5. Kung'ang'ania ajira ya umma ama serikali wakati umefikia muda wa kustaafu ni kujidhalilisha kwa Profesa na hata kwa Wasomi wanaotishia kufanya maandamo eti kuishurutisha serikali kumpa ajira! Ujasiriamali sio tu kwa wafanya biashara ndogo ndogo; hata kwa wasomi! Tusijidhalilishe. Wasomi wastaafu waanzishe vituo vya kusaidia mikakati ya maendeleo wakiwa huru zaidi. Mbona akina Profesa Wangwe na wengine wenzake wanaendelea vizuri tu. Hizi akili tegemezi kutoka kwa watu tunaowaona wasomi ni aibu kubwa kwa Chuo Kikuu na nchi yetu! Ningekeuwa Beregu ningekuwa wa kwanza kuiunga mkono serikali kwa msimamo wake! Wasomi amkeni! Dunia imebadilika! Ujamaa haupo tena!

    ReplyDelete
  6. MIE SIJAELWEA SAKATA LA BAREGU. MBONA GHARIB BILALI ALIYEGOMBANIA NA NA RAIS KARUME KUPITIA CCM MWAKA 2005 NI MJUMBE WA CCM.NA ANAENDELEA KAMA KAWA KUTOA LECTURE UDOM

    ReplyDelete
  7. Hapa shida si Baregu wala walaka.Shida ni kwamba hiyo sheria inawahusu wapinzani tu? Nimesoma kwa makini sana mjibuji wa hoja amabye bila shaka hakusoma na kujibu hoja zote zilizo tolewa na wanajamii.
    1.Ni meya wa meogoro ni mwana ccm na mhadhiri SUA
    1. Mkuu wa chuo cha ushirika moshi ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na wengineo wengi tu
    Sasa je hao hajavunja sheria na waraka? Tafadhali mdau jibu hoja fanya nalysis kwa haki usijibu kisiasa siasa.
    Pili kama unasema ni kwa ajili ya security hizo ni security zipi unazozisemea na je kwa nini tusiwambie watanzania kuwa tuna mfumo wa chama kimoja kwa ajili ya usalama na siri za nchi kuliko kuwahadaa kwa kusema nchi yetu ni democracy?
    Binafsi sitaki kuamini uongo unaotoa kwa kutumia waraka na sheria za utumishi ambazo zinalalia upande mmoja.
    Sasa kwa mtazamo wako tunaenda wapi kama si kufanya kila mtu aogope kuunga mkono itikadi anazoona zinafaa? naoma usinijibu kisiasa mimi si mwanasiasa na sitegemei kuingia kwenye siasa za bongo za majungu na unafiki
    Mdau SK

    ReplyDelete
  8. Kinachawashinda Serikali ni kwenye kila mfano wanaotumia kuna mifano mingine minne ambayo inawasuta. Time will tell, maana sio kazi kuonyesha hypocrisy ya serikali.

    Kinachonitia wasiwasi zaidi ni jinsi tunavyozungumzia elimu ya juu kuwa muhimu halafu tuja ignore kabisa recommendation ya wale wahusika wenyewe chuoni wanaosema kwamba Prof. Baregu kichwa chake bado kinahitajika.

    Tunasema vijana wengine waache, hivi kweli leo hii mtu na akili zake anadiriki kutamka swala la vijana waachiwe kwenye mambo ya elimu ya juu. Kweli waziri wetu katembea nje ya nchi kwenye vyuo vya elimu ya juu kuona vibabu vyao vinavyotukuzwa. Ufundishaji sio kama kazi yako ya uwaziri. The fact kwamba waziri haoni tofauti inaonyesha jinsi kazi kubwa tuliyonayo.

    ReplyDelete
  9. Mimi nasema kama mdau mmoja alivyosema pale juu mimi najiandaa kabisa nipate ajira yangu huku nilipo kimasomo kwa sababu serikali yatu TZ inaonekana kuwachukia wasomi ambao wengisaidia sana.

    Angalia nchi jirani wanavyo thamini michango ya wasomi wao na hata kuwalipa mishahara mizuri lakini Tanzania inaona wasomi ni maadui wa CCM, kama CCM watafanya vizuri mambo yao kwa uwazi hakuna mtu anashida nao isipokuwa wanaendelea kufikiri watanzania wote ni mbwiga tu hatujui lolote.

    CCM wanafikiri wamemkomesha Prof Baregu lakini wanasahau, huyu Baregu kasoma PhD na Dr. condoreza rice, na anatambulika sana duniani kuliko huyu CD waziri wetu.

    Baregu akitaka kazi tena yenye mshahara zaidi ya aliokuwa anapata UDSM anapata mara moja, sasa sijui ghasia na........yake watapata nini.

    ReplyDelete
  10. Ooooh!!!??? Mungu Ibariki Tanzania.
    Ndio maana Prof. Baregu anasisitiza katiba ya nchi hii ibadilishwe. Ina mapungufu mengi tu kama hayo ya kunyanyasana. Kama nchi yetu ni ya vyama vingi wananchi tofauti na ccm wafanye nini kwenye nchi yao. Kinachofanyika akijitokeza mpinzani mahiri mwenye kuelewa maana ya upinzani wanatafuta jinsi ya kumnyima nguvu. Bila ya kuwa na wapinzani tutasemaje nchi yetu ina vyama vya upinzani. Tukubali kuwa tunalazimishwa nchi yetu ni chama kimoja kutokana na katiba waliyojitungia. Wakati watu wenye uelewa wakisema ibadilishe wanatafutiwa sababu za kuwadhoofisha.
    Muhimu hapa KATIBA IBADLISHWE ili kuwe na misingi ya DEMOCRASIA sahihi.
    Anyway TIME WILL TELL.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  11. Mie naishangaa sirikali! Pale SUA kuna Mheshimiwa mmoja yeye ni Profwesa na ni diwani kupitia chama tawala na kwakupitia tiketi hiyo ya udiwani wa ccm amefanikiwa kuwa meya. Na bado anaendeleza libeneke SUA.
    My qn kwa Ghasia why do we have double standards? Muwajibisheni Profwesa Ishengoma basi haraka achague CCM au SUA.

    ReplyDelete
  12. Naishangaa sana serikali ya TZ. Mie sielewi kama tutaweza kujiondosha katika lindi hili la ujinga maana unategemea hata kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji kuwa waziri iliuwezekuuona ubabaishaji huu.
    pale SUA yupo mh. Profwesa Ishengoma yeye ni diwani wa ccm na meya wa manispaa ya morogoro na bado anaendeleza libeneke pale SUA bila hata shida. Yeye hajakiuka sheria za utumishi kwakuwa ni ccm.
    Ghasia why the hell do you havedouble standards? Let Ishengoma be held responsible as well. Kwanini hiyo sheria iwe kali kwa walionje ya ccm tu???
    Hatukatai the fact kwamba baregu amekiuka sheria tunachopinga ni namna kunavyokuwa na matabaka inapokuja suala la kuwawajibisha wakosaji.

    ReplyDelete
  13. Kinachonishangaza mimi, ni kwamba pamoja na ukweli wote huu Hawa Ghasia bado kakaa kimya kama vile hajafuka. Bob Marley "You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time" na Akasema katika wimbo mwingine " Time will tell" Pia mashujaa wa Majimaji Chief Songea Kabla ya kuuawa na wajerumani alisema "Nyie mwatuua sisi katika nchi yetu lakini watoto na wajukuu wetu watapambana na nyie hadi muondoke" So akina Hawa Ghasia na wenzake wasome alama za nyakati.

    ReplyDelete
  14. Obama- KikwetelizedJanuary 17, 2010

    Hili jambo limefanya niandike yafuatayo.

    Mimi ni mwana CCM na familia yetu wote ni wana CCM (damu-damu) lakini nimesikitishwa sana na majibu yanayotolewa hapa juu ya kilichotokea kwa Prof. Mwesiga.

    1. Sishabikii Wastaafu kuendelea na kazi za mikataba kama hakuna sababu yeyote. Lakini pale ambapo tuna upungufu wa Wanataaluma kama huyu Prof. na AKATAKIWA NA MAMLAKA HUSIKA (rejea mapendekezo toka Mlimani penyewe) hakuna kosa kumuongezea mkataba. Mbona tuna watu kibao waliofikisha umri wa kustaafu lakini wanaendelea kututibu kama Madaktari, wanaendelea kututawala kama Wakuu wa Wilaya/Mikoa na wengine kuongoza Wizara kama Mawaziri n.k

    Hivyo si kwamba ni yeye anangángánia bali anaombwa kusaidia na ombi linatolewa na jamii ya Wasomi wenyewe.


    2. Kuhusu suala la waraka huo wa utumishi wa umma. Yeyote mwenye upeo wa kuangalia mambo kwa undani na anayejali utawala wa sheria atajiuliza kuwa, je ni wapi panasema kuwa 'mtumishi wa umma akikiuka moja au zaidi ya maadili apaswayo basi asubiriwe mpaka pale anapoweza kukataliwa kuongezewa mkataba wa ajira au kutopewa nafasi fulani anayoomba?

    Ninachosema hapa ni kuwa, endapo Prof. katika kutekeleza wajibu wake kama mtumishi wa umma kwa wakati wowote alionekana ama kutotimiza wajibu wake kwa sababu ya siasa au kutofuata maadili ya kazi yake au kutokuwa mwaminifu au kutokuwa msiri n.k kwa nini HAKUCHUKULIWA HATUA WAKATI HUO?

    Halafu tuwe makini sana kupata tafsiri mwanana inayomaanishwa katika kila kipengele cha waraka huo.
    Mfano mimi kama mtumishi wa umma nikigundua kuwa mtumishi wa umma mwenzangu (haijalishi mdogo au mkubwa kiasi gani) ni mbadhilifu wa mali ya umma au anasababisha kutuongezea umaskini, maradhi au ujinga katika ngazi yeyote ya serikali na nikatoa taarifa ya wazi panapohusika. Je hapo nitakuwa mwaminifu au si mwaminifu kwa Serikali yangu?

    Mh. Waziri kwa heshima zote, suala hili linatuletea kiza ambayo si ya lazima katika Serikali yetu makini chini ya CCM. Kama hatukumchukulia hatua wakati amevunja maadili hatuna haja ya kumsuburia kwenye kurenew mkataba maana tutakuwa na hoja hafifu.
    Pili, hekima wakati fulani inatufunza kuwa hakika kwa matukio kama haya, maana hapa ndipo mtu anapandishwa umaarufu wake kisiasa kitu ambacho si kusudio letu. Tukumbuke Mwl. alipotuambia kuwa muacheni wamsukume Mh.Mrema hata kama wanataka kumbeba, leo Mh. Mrema yuko wapi kisisasa?

    Bila aibu napenda kutamka wazi kuwa hata umaarufu wa Mh. Zitto ulinyanyuka exponentially kuliko kiwango chake alichostahili wakati amesimamishwa uamuzi ambao kwa kweli Bunge liliteleza.


    Kama ni katika taaluma yake ya kuzalisha Wasomi wenye upeo tunamkubali, lakini kama ni katika majukwaa ya kisiasa, mbona tupo wana CCM kibao tena vijana wasomi ambao tuko tayari kumtoa jasho na yeye akatukubali bila kucheza faulo yeyote maana Uprofesa haumaanishi kuwa ni kuwa bingwa au kubobea katika njanja zote bila mipaka!

    ReplyDelete
  15. ADILI NA NDUGUZEJanuary 17, 2010

    Ndugu Makimu na wenzio. Exactly huo Waraka pia unatakiwa kumbana Profesa Ishengoma na wengineo ambao wapo kwenye udiwani lakini bado wameajiriwa. Lakini je una hakika kuwa Ishengoma bado yuko kwenye payroll ya SUA? Una hakika kweli? Ila namjua diwani mmoja wa Ilala ambaye ni secretary wa Wizara ya Elimu mpaka sasa. Kinachotakiwa ni Hawa Ghasia na wataalamu wake wafanye audit ili kufahamu kama waraka huo unatekelezwa.

    Hoja yangu iko palepale Waraka hata kama umepitwa na wakati ni lazima uzingatiwe. Of course kama ubatilishwe basi serikali yenyewe itajua na hiyo ni mada nyingine.

    ReplyDelete
  16. Tatizo hapa ni Prof Baregu wala sio Waraka.

    Serikali haitaki wasomi wajihusishe na siasa wakati huo huo wanakubali kuwakodishia mabasi wanafunzi wa Mlimani kwenda Diamond Jubulee kuhudhuria mkutano wa CCM.

    Kwa nini CCM inaogopa kivuli chake namna hii???

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  17. MTU YOYOTE YULE ANATAKIWA KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI, KWANI SERIKALI NI WATU WOTE SI YA CHAMA TAWALA TU, NDO MAANA NCHI ZA WENZETU KAMA MTU AMEVUJISHA SIRI ZA SERIKALI NA IKITHIBITISHWA HIVYO UFIKISHWA MAHAKAMANI, NIMEONA HIVYO U.S.A. CANADA NA U.K. WATU WAKIFIKISHWA MAHAKANI KWA KUTOWA SIRI ZA SERIKALI HADHARANI BILA KIBALI SO SWALA LA KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI SI SWALA LA CHAMA TAWALA TU NI SWALA LETU SOTE, KUNA TARATIBU ZA KUFWATA KULALAMIKIA SIRI HUSIKA KAMA INAENDA KINYUME NA HAKI ZA MSINGI ZA BINADAMU, VIKO VYOMBO VYA SHERIA. SO WAZIRI YUKO SAWA KABISA KWA HILO

    ReplyDelete
  18. THE government decision not to renew the contract of Prof Mwesiga Baregu to lecture at the University of Dar es Salaam, is raising quite unnecessary debate.

    Employment contracts are the preserve of employees and employers and are maintained with mutual consent. The contracts clearly stipulate that renewal must be agreed upon by both parties.

    Neither the employer nor the employee can be forced to renew a contract and no third party has the right to impose the terms of a contract between employer and employee.

    Like all contracts of employment, Prof Baregu’s contract is, therefore, exclusive to him and his employer.

    Nobody, least of all the University of Dar es Salaam Academic Staff Association, should thus usurp advocacy for renewal of the contract.

    But, for the sake of argument, even if UDASA or any one else were to take up the case of government’s decline to renew Prof Baregu’s contract, they should examine the facts and avoid politicizing it.

    The Minister of State in the President’s Office (Public Service Management), Ms Hawa Ghasia, has clearly explained that the outspoken don, who is now an elected member of the Chadema Central Committee, retired from the university when he clocked 55 years of age, ten years ago.

    He apparently opted for the voluntary retirement under the law, to look for greener pastures in Zimbabwe. What Prof Baregu’s self-appointed advocates don’t tell you is that he returned home after a fouryear stint and has since lectured at the ‘Hill’ for five years on short contracts, the last of which expired in 2008.

    Clearly, this reflects appreciation of Prof Baregu’s teaching skills by the government, which was his employer. It is important to note that the don is a retiree and the five years extension of contract was purely discretionary.

    That discretion could be applied further, but as pointed out by Ms Ghasia, Prof Baregu’s acceptance of a leadership position in a political party, now bars him from employment in the public service under standing regulations.

    Of course, that is far from saying Prof Baregu cannot take up employment in a privately owned university and there are many in need of the special skills he possesses.

    Alternatively, even the best lecturers have to retire effectively one day and the most recent example is Prof Issa Shivji. Isitoshe kung'ang'ania madaraka ni moja ya dalili za kutokuwepo kwa succession plan kwa vijana wa kurithi kazi zetu na hao maProf wa UD walikuwa wanoko kwa kufelisha watu ili wasije kuchukua nafasi zao..wakati umefika wazee wapumzike..kuna vijana wasomi wengi tu!!
    It is entirely upon Prof Baregu to determine his way forward.

    ReplyDelete
  19. akili ni nywele kila mtu ana zake..

    so mnazijua KIASI cha nywele za kila mhusika hapa?

    mshanisoma

    ReplyDelete
  20. we Anony wa 09:37 hujui tofauti kati ya siri za serikali na Scandal, so usikurupuke tu, hivi unadhani kwa mfano kusema kwamba rada mbovu zimenunuliwa jeshini ni siri? hizo ni scandal ambazo lazima zijulikane na kutafitiwa, ndo maana kuna ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali. KAMA HUJUI JUST KEEP U MOUTH WATERFUL!

    ReplyDelete
  21. Kwa ufupi kabisa waraka huu wa utumishi wa umma, unatakiwa kuwabana watumishi wote wa umma kutoonekana wakiwa pamoja na wanasiasa wakati wa saa za kiofisi za ofisi ya umma.

    Sasa ni kufuatilia kwa ukaribu na kuona hatuwaoni watumishi hawa wa umma ktk mikusanyiko, mikutano, kampeni, wakiwa na sare, alama za kutambulisha chama chochote cha siasa kikiwemo chama tawala.

    Mdau
    Waraka

    ReplyDelete
  22. Kwa maelezo ya watu hapo juu na jinsi waraka huo unavyotumika kuwabagua watumishi wa serikali kulingana na vyama vyao ni wazi kuwa tafsiri halisi ya waraka huo ni kuwa "MTUMISHI WA SERIKALI HARUHUSIWI KUFANYA SHUGHULI ZA KISIASA ZA CHAMA KINGINE ISIPOKUWA CCM"

    ReplyDelete
  23. Waraka unaozungumziwa hauwahusu madiwani. Tafadharini tujitahidi kusoma na kuelewa siyo kufuata tu mkumbo. Wanaotaja jina la Prof. Ishengoma wanachemsha kwa hilo. Yeye kama diwani na meya hivyo vipengere havimuhusu.
    Hata kama tu wanachama wa vyama mbali mbali, tujaribu kuondoa hisia zetu na tuweke maoni kufuatana na kanuni na taratibu za ajira serikali. Mambo ya kusema Hawa Ghasia ndiye kakataa kuongeza mkataba wa Baregu huyo ni utoto. Hayo ni maamuzi ya serikali, na Mama ni msimiaji wa sera ktk wizara husika.

    ReplyDelete
  24. mdau 10:09, hapo mzee Arap Moi angesema kuwa'
    " Serikali ndiyo munyama gani?

    Ondoa hapa upupu yako. Musimamizi ya sera akitelesa lazima watu wamwambiye arekebise na siyo kusukumia serikali. Kwa nini yeye hakuchukuliya hatua Bereku wakati nakosea? Hii si uungwana! "

    ReplyDelete
  25. CCM wanaogopa kuwa kuendelea kumlipa Prof. Baregu mshahara wake wa Uprof pale UDSM atakuwa anawachagia CHADEMA pesa za kampeni na kuwawezesha kufanya operation zao za kuing'oa CCM. Mkakati wao ni kuwa-sufforcate wapinzani kiuchumi ili washindwe kujitangaza. Haya mengine yote ni janja ya nyani tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...