Kundi la Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali akiwemo mdau John Nditi (shoto chini ) pamoja na Nickson Mkilanya wa Star TV na Redio Free Afrka wakijiandaa kupanda kiberenge kuelekea kilometa zaidi ya 10 toka mjini Kilosa , njia ya reli ya kati kulekea eneo liliposombwa na maji darala la reli katika Mto Mkondoa , usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira , Dk Batilda Burian , ( kulia) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu , Omary Chambo ( kati kati) na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo ( kushoto) wakitafakari hali halisi ya uharibifu wa mazingira na athari za mafuriko yaliyowakuba wakazi zaidi ya 24,000 wa mjini Kilosa kuanzia Desemba 26, mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo ( kushoto) akipita orodha ya vifaa vya misaada ya dawa za binadamu na mingine iliyotolewa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Regencyu ya Dar es Salaam ( hayupo pichani) iliyowasilishwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kilosa ikiwa ni kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea mjini Kilosa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana.

wananchi wa Kilosa wakibeba misaada kupeleka kwa waathirika wenzao wa mafuriko hayo
wananchi wakivuka mto mkondoa
daraja la reli ya kati iliyokumbwa na madhara ya mafuriko hayo
sehemu ya uharibifu huo

daraja likiwa limebomoka kwa mafuriko










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. serikali yetu ina kichwa kigumu sana kama ingekubaliana na ashauri wa wananchi kuhusu lile tuta yasingetukuta haya, tatizo blaa, blaa, nyingi,nina machungu na kwetu kilosa

    ReplyDelete
  2. ....kuna business opportunities nyingi sana Tanzania!!

    Haya madaraja ya enzi za enzi yanatakiwa kurekebishwa tusiwe tunaisingizia mvua wakati ni uzembe wetu kuweka miundombinu yetu sawa.

    Nawapa pole wahanga wa mafuriko!!

    ReplyDelete
  3. mradi wa kudumu wamedizaini kwa mvua ya miaka 10, wachina bwana!

    ReplyDelete
  4. nimependa sana hiyo mandhari

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi,

    Huu ni uzembe. Ripoti ipo chuo kikuu tangu sijazaliwa!

    Flood control, Mkondoa river system
    hydrological records
    by U. Riise


    Published in 1970, University of Dar es Salaam, Bureau of Resource Assessment and Land Use Planning (Dar es Salaam)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...