Shikamoo bro Michuzi,
Kwanza kabisa shukrani tele kwa kutufikishia habari kwa njia ya blogu yako. Ubarikiwe na uzidishiwe sana tena sana. Nimevutiwa sana na makala iliyoandikwa na mdau John Mashaka.
Nimevutiwa sana na nimeona nichangie mdahalo huo kwa kujaribu kuelezea mfumo wa soko la nyumba wa marekani (kwa kifupi na urahisi...very simplified kwahiyo kuna detail nyingi ambazo sijaweka) na kujaribu kuonyesha kwamba upo tofauti sana na mfumo wa soko la nyumba na ardhi Tanzania.
Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba ule wa Marekani ulikuwa unategemea zaidi mauzo na manunuzi kwa njia ya madeni wakati Tanzania kwa uzoefu wangu mdogo ni kwamba watu wengi wanafanya manunuzi kwa cash zaidi (Kaa alivyoeleza Bw. Mashaka kwamba kuna mtu alitoa mamilioni meeengi tu kwenye buti la gari na kulipa).
Mimi argument yangu ni kuwa si rahisi kwa uchumi wa Tanzania kutetereka kwa kutegemea soko la nyumba Tanzania. Sababu kubwa niliyonayo ni kuwa transaction nyingi zinafanyika kwa cash na sio mikopo.

Basi kwakuwa Ndg. Mashaka ameiita makala yake "...Mdahalo.." basi na mimi naomba nichangie kwa maelezo haya hapa chini. Nitafurahi sana kama yatapata nafasi na kukubalika machoni pako.

Nimeguswa sana na jinsi ambavyo Ndg. John Mashaka amelinganisha kutetereka kwa uchumi wa dunia hivi karibuni na uwezekano wa kitu cha jinsi hiyohiyo kutokea Tanzania.
Sababu kubwa uliyoitaja inayoweza kusababisha kumomonyoka kwa uchumi wetu wa madafu ni
1. kuna watu wachache wanaoshikilia ardhi pamoja na nyumba
2. Madalali wanaopanga bei "kiholela"
Ni kweli kabisa kwamba sababu, hususani ya kwanza inalingana na kushabihiana kabisa na sababu kuu iliyosababisha uchumi wa dunia haswa kupitia USA na UAE kuporomoka.
Hata hivyo kuna tofauti kubwa sana kati mfumo wa soko la nyumba nchini marekania na huku kwetu wamatumbi na wapogolo. Mfumo wa marekani uliosababisha kuporomoka kwa uchumi wa dunia:
1. Madalali waliuza nyumba kwa wananchi kwa njia ya mikopo (Makubaliano ni kwamba mnunuzi atalipa kidogokidogo kila mwezi. Mnunuzi atakaposhindwa kulipa, basi nyumba inakuwa ya dalali. Hii ndio wanaita "default" kwa lugha ya kigeni)
2. Madalali wakaenda kuuza haya madeni kwa Mabenki na wawekezaji matajiri wachache(ambao wao sasa wataendelea kulipwa na wale wanunuzi katika kipengele 1. Wanunuzi wakishindwa kulipa, nyumba zinakuwa mali ya Benki au mwekezaji anayemdai mnunuzi).
Mabenki na wawekezaji wakavutiwa sana na mpangilio huu na wakazidi kununua madeni mengi zaidi hali wakiamini kabisa(ingawa kimakosa) kuwa thamani ya nyumba siku zote inaongezeka na hivyo hata watu wakishindwa kulipa basi watabakiwa na nyumba ambazo zina thamani ya juu na wataweza kuziuza kwa bei ya juu vilevile na kupata faida sana.
Kawaida, kuna vigezo ambavyo mtu lazima avifikie ili aweze kuuziwa nyumba kwa mkopo (lazima waweze kuthibitisha kuwa mnunuzi ataweza kulipa deni). Vigezo ni kama kuwa na kipato stable n.k. Madalali baada ya kuona kuwa huu mfumo unamfaidisha kila mtu, basi wakaanza kupunguza vigezo vya mtu kupewa nyumba kwa mkopo, ili waweze kuuza nyumba nyingi zaidi (watengeneze faida kubwa zaidi). Kwa vile bado waliamini kuwa thamani za nyumba zitazidi kuongezeka milele na milele.
Kilichotokea ni kwamba wakauza nyumba nyingi sana kwa watu ambao kwa vigezo vya mwanzo vya ununuaji wa nyumba kwa mkopo, wasingeweza kununua. Matokeo yake watu wengi sana wakashindwa kulipa, na hivyo waka-default. basi kulingana na mfumo ulivyo, nyumba hizi zikawa za mabenki pamoja na wale wajasiriamali matajiri.
Matokeo ya watu wengi kudefult: Kukawa na nyumba nyingi sana kwenye soko la nyumba. Hii ikasababisha supply ikawa ni kubwa mno ukilinganisha na demand katika soko la nyumba (kumbuka watu ambao wangenunua ndio hao hao wamesha default, hawana ankara). Kama kawaida, Supply ikiwa kubwa kuliko demand, bei zinaporomoka. Basi bei za nyumba zikaporomoka, na kufanya thamani za nyumba kushuka chini mno.
Basi kushuka kwa thamani ya nyumba (ambayo mabenki na wawekezaji waliamini kuwa itapanda milele na milele amina) kukashusha thamani ya hisa za makampuni mbalimbali ambayo yalikuwa yamewekeza kupitia wale wawekezaji mabenki, ambao kwa kifupi sasa wanamiliki mayumba meeeengi ambayo thamani yake imeporomoka.
Hivyo basi kwa vile nyumba hizo zilikuwa ni msingi wa kuthamanishwa kwa mabenki na wawekezaji, basi thamani zao pia zikashuka mnoooo. Basi na watu wa kawaida waliokuwa wamewekeza kwenye hisa za mabenki, na wawekezaji hao, Hisa zao zikashuka thamani saaaaana tu(kumbuka wawekezaji wengine ni hao hao waliokuwa wanunuzi hapo mwanzoni).
Maelezo hayo marefu yanaweka bayana kuwa mfumo huo ni tofauti sana na Tanzania ambapo kama mwandishi wa makala hii alivyosema, watu wanalipa cash. Na kwa kweli uchumi wa Tanzania (kwa watu wengi ambao ni wananchi wa kawaida) unategemea zaidi mfumo wa kulipa kwa cash na sio kwa mikopo.
Hivyo basi suala la madalali wetu hapa Tanzania kupanga bei kiholela, sio rahisi kuporomosha uchumi kwa staili ambayo uchumi wa dunia uliweweseka maana kwa hakika mfumo wa ununuzi kwa mikopo ni asilimia ndogo kuliko ule wa njia ya cash.
Ikiwa itatokea kweli kwamba bei zitazidi kupanda tu bila kuwa na mapumziko, basi hakika wanunuzi watabaki wachache wenye nazo, hivyo kusababisha supply kuwa kubwa kuliko demand. lakini kwa vile mfumo wetu unahusisha zaidi malipo kwa cash, basi suala la watu kudefault madeni yao kiasi cha kusababisha uyumbaji wa uchumi sio tishio kubwa kiasi hicho.
Hata hivyo suala la upangaji wa bei za nyumba na viwanja kiholela linabaki tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka sana!
Ni mimi Mdau wa Libeneke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. mmhh ila wee mdau kiboko kishwahili simple na nimekuelewa mwezangu asante,,,
    john mashaka nimeshindwa kiinglishi kwakweli

    ReplyDelete
  2. wewe mtu usipoelewa uschangie maada ya MASHAKA, kwa kifupi umelopoka tu hakuna lolote la maana ulilo ongea. Yeye MASHAKA ali base zaidi kwa watu wa chini katika argument yake. Kimtazamo wake anaona bei ya nyumba si sawa na hali halisi ya maisha ya mtanzani kufuatia na jinsi uchumi wa Tanzania ulivyo.

    lakini wewe umekua uki support upandaji wa bei za nyumba kiholela, je umewafikilia watu masikini wa tanzania ambao wengi wao hadi leo hii bado wanaishi kwenye nyumba za Miti na udongo?

    ReplyDelete
  3. @Mon Jan 25, 01:39:00 PM
    umemlisha panya dawa yake, hawa wadandiaji wanapotosha sana umma. Mashaka kafanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika makala yake, lakini panya linakuja kutafuna kila kitu, na kukiharibu

    ReplyDelete
  4. Hongera Mzee;
    Wakina mashaka wanaangalia uchumi wa west bila kutafautisha

    Simply; kule uchumi umeporomoka kwa sababu wamiliki wa nyumba walishindwa kulipa madeni

    Hapa watu wanalipa kwa cash, kama economy itashuka watakao umia ni just watu wachache sio overall econoy

    Anae elewa economy atasuport argument yako, isipokuwa wale wachache wanaofuata upepe watabaki na mgando uleule wa mawazo, Mashaka is our presider 2010, For what?

    ReplyDelete
  5. mtu anaweza kununua nyumba kwako cash,utajuaje labda hio hela kakopa benki?watu wengi wanakopeshwa hela za kununua nyumba na benki,vilevile hata ukitoa mil.300 kununua nyumba leo, demand ikiwa ndogo kuliko supply si thamni itashuka?sio lazima iwe uchumi wa nchi hata individual lazima wawe makini,usije kununua nyumba mil.300 baada ya miaka 3 thamani yake ni mil.50,ndicho kilichotokea huko usa,uk etc

    ReplyDelete
  6. Mashaka ni mtu anayetaka mambo nje ya uwezo wake.

    Alikwenda Bagamoyo kwenye hotel za high class akauziwa soda $5 kaja kwa Michuzi kulalamika.

    Kenda kwenye soko huria la ardhi, kapigwa bao na wenye hela anakuja tena hapa kulia lia.

    Yeye alidhani milioni 80 ni hela nyingi sana hakuna wa kumpita.

    Grow up man.

    Kama umeamua kurudi Bongo jifunze mambo yanavyokwenda Bongo, sio unataka mambo ya Bongo yawe kama ya Marekani.

    Alikuja hapa akadai uchumi wa Marekani umetetereka hivyo uchumi wa Bongo nao utateterka ... akatoka kapa.

    Uchumi wetu umekua. Data ziko benki kuu pale.

    Leo anakuza mambo out of proportions anadai eti kwa kuwa kapigwa bao kiwanja cha Bunju, basi uchumi wetu utatetereka, na eti waliompiga bao ni watu hatari kwa usalama wa taifa.

    Jeeez man! Grow up.

    ReplyDelete
  7. asante mdau wa libeneke kwa twisheni nzuri uliyotupatia in this rejoinder to Mashaka's dictum. Hizi bei holela za nyumba zitaporomosha uchumi wetu kwa kupandisha inflation, na hivyo thamani ya shilingi kuporomoka. Vile vile tofauti kati ya kipato kati ya wenye nacho na walalahoi itazidi kupanuka kwani ni wachache watakua wanamiliki ardhi na other means of production.
    nawasilisha,

    Mwakasungula (PhD, Univ of California - Berkeley)

    ReplyDelete
  8. Nashukuru sana kwa maelezo haya. Yako 'clear' kabisa, na nimeweza kuelewa kwa lugha raisi kabisa kuhusu mporomoko wa bei za nyumba huko marekani; unafaa kuwa mwalimu. Nimependa vilevile approach yako ya kuingia katika huu mdahalo. Baadhi ya wasomaji naona wanataka kupeleka mambo tofauti kwa kutazama zaidi mtu, na siyo fact. Ndipo hizi blog comments zinaanza kuchosha na kupoteza muelekeo. Let's keep the discussion going.

    ReplyDelete
  9. Mdau nashukuru kwa kuchangia na kwakutumia kiswahili, hongera sana, lakini naungana kabisa na baadhi ya watu kuwa hujaelewa nini Mashaka anaelezea, ilinilazimu nirudie kusoma makala ya Mashaka na naona hujamuelewa, na pia Mashaka nadhani aweke mada kwa kiswahili itakuwa nzuri sana!

    ReplyDelete
  10. Mdau asante kwa maelezo mazuri na fasaha. Sijui kama nitakuwa nje ya mada, lakini tungweza kuongeza kuwa mfumo wetu wa manunuzi kwa cash umekuwa mojawapo ya chachu ya ufisadi. maana watu wanapenda kumiliki nyumba na vitu vingine vya anasa lakini hawezi kusubiri hadi waweke akiba ya miaka 30 kufikisha pesa za kununua nyumba. badala yake wanafisadi! hata walw wanaopata mikopo ya benki riba ni kubwa mno na kipindi wanachopewa kurejesha ni kifupi mno. bado inakuwa kama ni mfumo huo huo wa taslimu. matokeo yake kitakachporomosho uchumi wa tanzania sio soko la nyumba bali ni UFISADI.

    ReplyDelete
  11. Wajameni naomba kuulizeni, Dr Shayo amekufa au bado yupo maana haya ndo maeneo tungetegemea kumsikia. I meant kufa kifikira siyo kimwili ndugu wadau wa libeneke.

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  12. Mkuu,

    Ahsante kwa mada nzuri ila nina mashaka na wazo lako la kusema nyumba nyingi Tanzania zinanunuliwa kwa pesa taslim (Cash).

    Hebu angalie zile Apartments zilivyoporomoshwa Jijini, kweli zile zimejengwa kwa Cash??

    Na yale mahekalu kule Masaki na O'bay nayo yamejengwa kwa Cash??

    Hili naona unapotoka mkuu.

    Alichosema Mashaka kiko makini kabisa...soko la nyumba na arthi Tanzania ni PUTO linalosubiri mwiba lipasuke. Dalili zipo kila mahali...mwenye macho na aone.

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  13. mdau asante sana kwa kueleza uchumi wa marekani kwa urahisi ambao sijapata kuona! for the first time nimeelewa hii ishu vizuri sana ingawa naiona kila siku kwenye tv hapa kwa kaka obama. Kama wewe sio mwalimu naomba ufikirie kuwa mwalimu, mimi naomba sasa unieleweshe mambo ya stock kama hivi manake nayo yananipiga chenga na nina hamu sana kuelewa.
    grasuj@gmail.com,
    ntasukuru.

    ReplyDelete
  14. Wanaotaka kujua hali ya Dr Shayo ni kuwa taarifa za uhakika zilizotufikia leo ni kuwa kijana huyo kaamua kurudi Nyumbani Rasmi, kujenga Taifa. Vyanzo vyetu hivyo vinasema kuwa ameamua kutimiza ile ahadi yake aliyotoa miezi kadhaa.

    Kwa kweli mimi binafsi nimefurahishwa na kitendo hicho cha kikakamavu anachokionyesha Dr Shayo.

    Nilipomsikiliza Radio Ujerumani hivi majuzi nilijua tuu, kweli jamaa kaamua kurudi kuja kusaidiana na watanzania wenzake kujenga Taifa.

    Kama anania ya Ubunge ni mapema sana kujua, lakini akiamua kujikita huko moshi vijijini, atawatoa nje akina Lyatonga Mrema, Kimaro Aloyce na wengineo ambao wanataka kutumia bahasha za Khaki.

    Hadi sasa mchango wake, ni njenzo tosha ya kupewa Kura 2010

    Waswahili walisema "ukiona kobe kainamisha kichwa anatunga sheria"

    Hivyo, ninavyomuelewa Dr Shayo is working on something, Let us wait.

    ReplyDelete
  15. NAONA MNAROPOKA TU, WALA MSICHANGANYE MASWALA YA NYUMBA YA U.S.A. NA TANZANIA. TANZANIA SI BIASHARA RASMI YA UUZAJI WA NYUMBA NI KAMA VILE MTU ANAKWENDA SOKONI KUNUNUA NYANYA, U.S.A PROPERTY BUSINESS NI RASMI NA INATAMBULIKA NA VYOMBO HUSIKI SI TANZANIA WATU WANAUZIANA NYUMBA KIHOLELA HATA KODI HAWALIPI, IS OFFICIALY KNOW INDUSTRY IN TANZANIA SO NI VITU VIWILI TOFAUTI KUVILINGANISHA.

    ReplyDelete
  16. Mdau nashukuru kwa kutumia lugha nyepesi kuelezea mambo ya mogeji, kweli umenifumbua macho, japo sikuweza kuona kama unamjibu mashaka hoja zake za ufisadi wa bongo. Shule uliyotoa hapo imenitoa matongotongo kujua bubble kupasuka ndo kitu gani. KAKA MASUPU NAONA UPITISHE MADA YA KWAMBA LIBENEKE LIENDELEZWE KIMATUMBI, VINGINEVYO NAANZA KUTOA MADA ZANGU ZA KICHAGA HAPA...aika meku, waai!

    ReplyDelete
  17. Mkuu wa wilaya wa naniihii naomba niwasilishe hoja, natamani sana hoja hii itoke mbele ya umma ili waweze kuelewa kuwa kuna umuhimu wa kusoma na kuelewa maada ya msingi kabla ya kuruka na kuanza kutoa uchambuzi usiokuwa na uchambuzi yakinifu.

    1. Bwana Mashaka katika hoja yake ametoa hoja zaidi ya moja nazo ni hizi zifuatazo
    a. Kutokuwa na taasisi za kuratibu bei za nyumba na viwanja tanazania kunasababisha Madalali kuendesha soko, hili katika muda fulani itafikia mwananchi wa kawaida kwa kiwango chetu cha GDP kushindwa kumudu kuishi mijini ama hata kuchangia shughuli za maendeleo maana hawataweza kumudu gharama hizi katika maeneo yenye viwanda, mashule, mahospitali na ofisi nyingine za kijamii.
    b. Naomba nitumie kingereza kwenye hili nalo ni Development of a vicious circle of corruption. Tujiulize mtu wa kawaida atapata wapi milioni 120 kwenda kununua kiwanja ama nyumba, hii itapelekea kila mtanzania asiye na uwezo kutamani siku moja kuingia madarakani ama kushirikiana na fisadi ili aweze kuiba na kupokea rushwa ili na yeye aweze kuwa na nyumba mjini, hili ni tatizo kubwa mnooooooo, na yeyote anayesema halioni pole zake.
    c. Soko la marekani kimaendeleo lipo katika hatua ya juu sana lakini kutokana na utandawazi nchi za dunia ya tatu huwa zina Leap frog life stages na kujikuta hazifuati hatua zile zile zilizopitiwa na dunia ya kwanza.In Tanzania majority ya appartments na maghorofa makubwa yamejengwa kwa mikopo ya Bank, na ukiangalia justification ya mikopo hiyo kwenye business plan za hawa developers ni kuwa soko lita kuwaa kwa kiwango kikubwa. Swali lipo ni wapi tofauti yetu kimsingi na yaliyowakuta wamarekani. Kumbuka kuwa hawa developers wanachukua mabilioni ya mikopo, hivyo ili fedha yetu iendelee kuwa na thamani hizi hela walizochukua zinatakiwa ziingie kwenye mzunguko, wakishindwa kupangisha ama kuuza ina maana hizo hela zimenasa hukohuko, bank walizokopa itabidi wawanyang'anye hizo nyumba ama wajaribu kuzipangisha wenyewe, je hatujarudi kwenye lile lile la demand and supply, kama haitoshi Bank kuu watahitaji kuongeza mzunguko ambao utasababisha devaluation of currency, inflation nakadhalika.

    Kiufupi ili nchi iweze kuendelea ni lazima kuwa na Taasisi ambazo zinasimamia na kuratibu shuguli mbalimbali za kimaendeleo, tuna case studies nyingi sana zinazotueleza kuwa hii ndoto ya soko huria bila regulator ni ndoto ya mwenda wazimu. Na kama nimemwelewa Mashaka vizuri hili ni moja ya jambo ambalo anataka kuamsha changa moto, na sidhani nia yake ilikuwa ni kutaka kuonyesha kuwa yeye na uzoefu na Ulaya ama marekani kama wachangiaji wengine walivyodiriki kumhukumu. Tumeonna jinsi gani vyombo kama EWURA, SUMATRA, FAIR COMPETITION imebidi viundwe hii yote inatufundisha kuwa si rahisi kwenye nchi zetu hizi kuwaachia watu uhuru uliozidi wa kuamua bei na level of standards za soko, kuwa masomo mengi tu duniani jamani, tusome kidogo.

    Naandaa mchakato wa kuchambua soko la nyumba marekani na sababu zilizopelekea prime lending crisis.
    ASANTE, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  18. mashaka wakati mwingine andaa mada yako kwa kimatumbi ili kila mmoja aweze kukuelewa na kuchangia mawazo yake.

    ReplyDelete
  19. Bei za nyumba zitastabilize pale hela za EPA zitakapoisha kwenye mzunguko full stop.

    ReplyDelete
  20. Nakubaliana na uhuru wa kuchangia mawazo kwenye blogu hii ya jamii, lakini kwa hili mdau unapotosha umma kwa kujibu hoja ya Mashaka bila kutafiti. Kuuza nyumba au kiwanja au kupangisha kwa bei kubwa(tena kwa dola) kuna athali kubwa kiuchumi kwa Tanzania. Fikilia ni dola kiasi gani zinatoka nje ya soko na hivyo Benki kuu inabidi iteketeze hazina yake ili kufidia, kwani si zote zinarudi nyingine zinapita njia za panya na kutoroshwa nje ila mdau hufikirii hii hasara kwa Taifa.
    Kitu kingine ni kuporomosha thamani ya shilingi kwani mfumuko huu wa bei za viwanja na nyumba kusababisha kujaza hela kwenye mzunguko bila kuwa na thamani halisi ya bidhaa hizo za nyumba.Mfumuko wa bei huo huathiri sekta nyingine za uzalishaji kwa kuchochea mfumuko wa bei huko na kuathiri uchumi wa Tanzania.
    Achilia mbali uchumi wa mtu mmojammoja ambao huathirika kutokana na sehemu kubwa la pato lake kuelekezwa kwenye kufidia gharama za nyumba. Uchumi wa nchi huendelezwa pia na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Sasa kama uchumi wa watu unaathirika kutokana na bei hizi za kionevu ni wazi nguvu ya uzalishaji inaathirika kadhalika uchumi wa Taifa
    Sasa hivi huko wanaposema watu ati kimara,Tabata,mbezi ni gharama nafuu.Hivi kupangisha nyumba nzima kati ya TSh.180,000 hadi Tsh. 300,000. ni gharama nafuu?

    ReplyDelete
  21. Kwa anayesema bei ziko juu na tuwafikirie masikini. Nawakumbusha kwamba hivyo ndivyo soko huria linavyofanya kazi. Kwenye soko huria humlazimishi mtu kuuza kwa bei unayotaka wewe. Anauza kwa bei yake akikosa mteja atashusha. Na vile vile humlazimishi mtu kununua kwa bei unayotaka yeye. Ananunua kwa bei yake akikosa atapanda dau au atatafuta mbadala rahisi.

    Kwa nini usijenge wewe hizo nyumba za bei rahisi? Tena wewe ukiukata na kuanza kujenga nyumba zako ndio utakuwa wa kwanza kutaka bei za juu. Kwa sababu huna unalaumu.

    Mlivyoambiwa mnaachana na ujamaa na kuenda kwenye ubepari mkashangilia. Sasa mnaonja chungu yake mnapiga kelele. Mnapenda faida zake, hasara zake zikija mnakuwa wakali.

    Hizo bubbles na bursts ndio njia za soko huria kurekebisha bei pale zinapokuwa juu sana au chini sana. Hazikwepeki. Kama hamzipendi rudini kwenye ujamaa.

    Badala ya kulalama, njia rahisi ya kuwakomoa hao wanaoweka bei juu ni kwa wewe kutengeneza nyumba za bei rahisi zaidi. Hakika wateja wote watakuja kwako, including hao masikini unaowaonea huruma. Na hao jamaa watalazimika kushusha bei zao.

    Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.

    Kama huwezi kushindana na soko huria limekushinda, angalia jinsi ya kurudisha ujamaa. Huo ndio mkombozi wako.

    ReplyDelete
  22. Hivi mbona watu wanapoongelea maswala ya nyumba Tanzania wanaangalia sana Dar? Mbona Dar ni sehemu ndogo tu ya wakazi Tanzania na hata bei ya nyumba ukienda Mbeya au Mwanza ni tofauti na Dar. Na ndivyo bei za viwanja...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...