Ubalozi wa Tanzania nchini UAE ulifungua kitabu cha maombolezo ya kifo cha Simba wa Vita Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa tarehe 5 na 6 Januari, 2010, Ubalozini, Abu Dhabi. Waliokuja kutia saini kitabu hicho ni pamoja na Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE, Mabalozi, wawakilishi wa Mabalozi na wadau wengine. Pichani juu mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje nchini UAE, Balozi Saeed Hamdan Al Naqbi, akitia saini kitabu cha maombolezo huku Kaimu Balozi, Bw. Athumani W. Beleko na Afisa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Zaigal wakishuhudia.
Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje akimpa mkono wa pole Kaimu Balozi, Bw. Athumani W. Beleko baada ya kusaini kitabu
Balozi wa Nigeria, Mhe. Bashir Yoguda, akitia saini kitabu cha maombolezo.
Balozi wa South Africa, Mhe. Abba Omar, akitia saini kitabu cha maombolezo huku Kaimu Balozi, Bw. Athumani Beleko akishuhudia.
Balozi wa Senegal, Mhe. Abdourahmme Diof, akitia saini kitabu cha maombolezo 



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...