Mabalozi mbalimbali wamejitokeza kutoa rambirambi na kuweka saini daftari la maombolezo ya kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa hapa Ubalozi wa Tanzania, London. Ubalozi huu umefungua kitabu hicho leo asubuhi kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2009. Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali waliopo hapa London wamemuelezea Mzee Kawawa kama nguzo muhimu ya historia ya Tanzania na Kiongozi aliyeacha mfano wa unaminifu.
Balozi wa Zimbabwe, Mhe. Gabriel Machinga (Picha ya juu) amesema "Tunashukuru kwamba Mzee Kawawa ameacha historia iliyovuka mipaka ya nchi yake na bara zima la Afrika. Atakumbukwa sana na wengi tunamshukuru kwa kazi aliyoifanya."
Balozi wa Zambia, Profesa Royson Mukwewa akiweka sahihi yake. Yeye alimwelezea Mzee Kawawa kama "Shujaa Mkuu wa Tanzania na Afrika aliyejitolea muhanga kupigania ukombozi wa Bara zima." Alisema njia pekee ya kumuenzi Mzee Kawawa ni kuendeleza yale aliyoyapigania wakati wa uhai wake.
Balozi wa Papua New Guinea, Bi Jean L Kekedo, O.B.E. akiweka sahihi yake. Amesema "Tunatoa pole kwa kifo cha kiongozi huyu mkuu."
Balozi wa Ghana, Profesa Kwaku Danso-Boafo akiweka sahihi na kusema "Afrika imempoteza kiongozi wa kipekee. Bwana Kawawa alikuwa kiongozi aliyetutia hamasa wanasiasa wengi Afrika, wengi wetu tuliingia kwenye siasa kwa kufuata nyayo zake. Alichangia kiasi kikubwa kwa ukombozi wa Afrika."
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio UK, Ndugu Abubakar Faraji akiweka sahihi yake. Kwa majonzi makubwa amesema jina la Simba wa Vita halikuja hivi hivi na kwamba ni kweli Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa sima wa vita vyote vya Tanganyika na baadaye Tanzania, akisimama kidede katika shida na raha zote nchi ilipitia. Na kwamba endapo Mwalimu Nyerere alikuwa wino basi Mzee Kawawa alikuwa kalamu na kwa pamoja waliweza kuiandika historia ya kipekee ya Tanzania ambayo ni kisiwa cha upendo, amani na utulivu kutokana sio tu na busara zao bali pia kwa kuona mbali na kuunganisha matabaka yote.BURIANI SIMBA WA VITA
RASHIDI MFAUME KAWAWA
By Ayoub Mzee
Today the Tanzania community, Diplomats and friends of Tanzania gathered at the Tanzania High Commission to Pay their respect by signing the condolences book that was opened at the High Commission on 3 Stratford Place, London.
By Ayoub Mzee
Today the Tanzania community, Diplomats and friends of Tanzania gathered at the Tanzania High Commission to Pay their respect by signing the condolences book that was opened at the High Commission on 3 Stratford Place, London.
This book will be opened till Friday this week for all to come and sign.
Rashid kawawa who was the first Prime Minister of Tanzania died in the morning of 31 december 2009 in Dar es salaam. A seven- day mourning period has been declared by President Jakaya Kikwete.
The Tanzania community in the diaspora in conjunction with the Tanzania High commission in London will hold a memmorial service for the late on the 9th January 210 at
St Annes Mosque -St Annes Road,
Tottenham ,
London,
N15 5GJ
You are all welcome


Jamani tumelost mtu mmoja wa muhimu sana katika nchi yetu Kawawa mtu wa watu mwenyezi mungu alilaze roho yake salama salmin Amen.
ReplyDeleteJamani hitma saa ngapi?
ReplyDeleteAsalam Alaykum
ReplyDeleteNaomba kusahihisha kwamba huyo anayesaini kwenye picha ni Shabani Kawawa mtoto wa mdogo wake Marehemu Rashid Mfaume Kawawa na sio mjukuu wake.
Yupo mjukuu wake anaitwa Rashid,ila si huyo anayeonekana kwenye picha.
Ningependa kumjulisha huyo anayeuliza hitma saa ngapi,kuwa ni saa 9.
Shukran
Shukran
ukimaliza shuguli za huko london huko uje na bongo kutoa shukrani kwa ndugu jamaa na marafiki zako ndo utakuwa umewakilisha vyema
ReplyDelete