Kaka Jamaa wamefurahi sana kwa kuwafunga jamaa wenzao 4-0 siri ya mafaanikio ya huyu Mmisri kupiga soka kama hivi naona itakuwa vyema sana baada ya kuchukua kombe tuieleze japo kwa ufupi ili nasi timu yetu ya Bongo ifike Japo Kombe la Dunia miaka Ijao.
Ahsante Mdau Cairo
Ijumaa Njema.
habari kamili nenda BBC sport


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Tatizo la Wachezaji wetu wanacheza mpira bila Passion. Kinachowapa ushindi Wamisri ni Passion waliyonayo juu ya nchi yao. Hata wenzetu Wakenya wana Passion kubwa kuliko sisi. Kenya hawajui mpira kama ssi lakini wanafika mbali kwa kuwa wanacheza kwa Passion. Kumbuka enzi za wakina Athumani Juma Chama, Zamoyoni Mogella, Haidari Abeid, Charles Boniface Mkwasa. Lakini siku hizi tunacheza tuu ili mradi mpira unazunguka zunguka uwanjani. Fuatilia mechi ya leo kati ya Algeria na Egypt ndio utaona ni nini maana ya kuvaa jezi ya Taifa.

    ReplyDelete
  2. Kumbe Taifa Stars tuko juu. Kufungwa kwetu 5 na Misri haikumaanisha hatujui mpira. Wale wa Algeria waliomfunga Drogba wamelazwa 4? Si mchezo, kiwango chetu kioko juu.

    ReplyDelete
  3. POA SANA. MISRI WANATISHA

    ReplyDelete
  4. Ankali ki ukweli jana nimekasirika sana sio kwa misri kushinda bali kwa maamuzi mabovu ya refa wa mechi ya jana,hivi kwanini marefa wetu wa kiafrika wanatumia sana hasira kutoa maamuzi rather than busara???unawezaje kutoa Red card in the first half of the critical match kama ya misri Vs Algeria....hebu ona ule upigaji wa penati yaani its very dispointing to see the referee makes the algeria team frustrated...Kweli maamuzi kama haya ya kujinga huwa namkumbuka sana Sir perrugi Collina maana he is smart and he always think before making a decision in the football match...Misri walipania kushinda na refa aliamua kuwapa ushindi na kwa staili hii tuna safari ndefu kuweza kufikia ubora wa soka la kimataifa.

    All in all CAF wana kazi kubwa ya kufanya michuano yetu kuwa na ubora ili tuweze kuwa impress hata hao wanaosema soka letu la Africa lipo chini na lina mizengwe sana.

    ReplyDelete
  5. watanzania kukwenda kombe la dunia ama african cup si leo wala kesho kwani. watanzania wanao zaliwa nje za nchi generation hiyo ndo hita leta matunda tz kwneye sport adi kiserekali kwani upwewao ni kama wa wazungu. watanzania wa sasa ni wabinafsi sana na wachawi .
    mtazamo wangu tu
    mdau Afghanistan

    ReplyDelete
  6. mimi sikuielewa ile penalty iliowapa ushindi Misri,,,nifahamishwe vizuri

    ila kazi ipo,mirsi vs ghana na sie wengi weusi tii yani tutachukia saaaana tu misri ikishinda,,,wale sio waafrika jamani ni waarabu ithink wangekuwa kama western sahara sijui ile jimbo na moroco

    ee mola tujalie ngozi nyesui kushinda

    ReplyDelete
  7. Wewe unaye mlaumu refa pambano la misri na algeria ulikuwa umelala? refa ana makosa gani? au ukuona mechi kati ya asernal na barca fainali ulaya kombe uwanjani na kipa akatolewa dk za mwanzo tu? acha ushabiki na malalamiko yasiyo na tija refa amechezesha vizuri sana na tena alikuwa na huruma sana vinginevyo algeria wangecheza watatu tu. soma mpira algeria iliingia na hasira na kukamia, misri ni watu wazima waliingia wakiwa wametulia na kujua kilicho wapeleka angola!

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza ingawa nakubaliana nawe kwa point ya kuwa na passion, sikubaliani nawe kuwa wakenya hawajui mpira kama sisi ila wanafika mbali kwa sababu ya passion.

    bila ya ujuzi wa kucheza passion pekee haikufikishi mahali. tafuta wenzako wenye passion na nchi na mshuke uwanjani kama hamtochakazwa mabao 100 kama hamjui kucheza mpira.

    kusema wakenya hawajui mpira zaidi ya sisi sio tu kuwadhihaki wakenya bali pia ni kujidhalilisha kwa kujifika vilemba vya ukoka.

    Angalia katika time hiyo ya wachezaji uliowataja kenya ilibeba mara ngapi kombe la challenge (sasa linaitwaje sijui)na tanzania ilibeba mara ngapi? Tanzania bara au zanzibar zimefika mara ngapi katika fainali hizo wakati wa kipindi hicho?

    wakenya hawakupa mafanikio hayo bila ya kujuwa kucheza mpira.

    ReplyDelete
  9. Hawa jamaa wanaosifia Misri hapo juu kweli mpira hamuujui!kwa maamuzi ya jana unaweza kusema Misri kashinda au kabebwa kwenda fainali?nina sababu 3 kubwa za kuwapeni mjue ya kwamba waamuzi wa Afrika ni bogus kabisa
    1.angalia kadi ya kwanza alompatia yule mchezaji wa kwanza wa Algeria,haikuwa halali kabisa!
    2.ile faul aliwapa Misri na kumpatia jamaa kadi ya pili ya njano na hatimae nyekundu ni ujinga mtupu maamuzi gani yale?
    3.Angalia upigaji wa penati kweli mwamuzi alikuwa makini,mtu anakwenda anatishia then anapiga mpira penati ya wapi hiyo au hii ina apply CAF na si FIFA?Na ni maalum kwa MISRI tu!
    CAF lazima waangalie upya hawa waamuzi wao,tusifurahie ushindi wa Misri kwasababu tu tunaipenda MISRI,ndo maana wameshindwa hata kwenda Sauzi kwa World Cup.Anaejua mpira lazima ataniunga mkono,huwezi kufurahia ushindi wakati mpinzani wako amekuwa frastuated(changanywa kisaikolojia) na mwamuzi!

    ReplyDelete
  10. Siri ya Tanzania kuwa na mafanikio ya kisoka Afrika na ulimwenguni, ni kuwa na ligi kuu ambayo itakuwa ina ushindani mkubwa kiasi cha kutoa uwezekano wa kupata wachezaji bora wa ndani ya Tanzania.

    Baada ya hapo tunachukua Challenge Cup ya Afrika Mashariki ngazi ya klabu na Taifa. Tukitoka hapo tunaenda CAF na CAN. Tukifanikiwa kukubalika kuwa ni wakali wa kikanda (Afrika Mashariki) na barani Afrika, basi hata world Cup tutazuka.

    Lakini ikiwa mpira wetu ni Simba na Yanga tu kwenye ligi au kombe la Tusker, basi tuishie kuangalia wenzetu ktk TV wakifanya vitu vyao.

    Tizama ligi za Misri, Tunisia, Nigeria zinavyozalisha wachezaji kibao wa kimataifa, hiyo ndio siri kuu, ambayo hata Maximo ana irudia kila siku, lakini watanzania tunataka short-cut.

    Mdau
    Rocky

    ReplyDelete
  11. Mimi isu iko kwa wachambuzi wetu wa mpira wa tanzania kama mliangalia comment za jamaa wa bongo wao walibaki kumuona refa kama mungu wa mpira kwa hawa wapinzani wawili, mimi yangu ni haya nanukuu mmoja wa wachambuzi wetu "KIPA WA AGERIA ANIANZA YEYE KWANZA KUTOKA GOLINI KWA HIYO KOSA SI KWA MPIGAJI WA MISRI KUTISHA KWANZA KABLA YA KUPIGA MPIRA NA KUANDIKA BAO LA KWANZA" mimi ninavyojua ni na ilivyo katika sheria za mpira wa miguu "KIPA ANAPOTOKA KWENYE LINE YA LANGO LAKE KABLA YA MPIGAJI KUPIGA MPIRA IWE KIPA ALIFUNGwA AU AKUFUNGWA NA MPIGAJI ANAPOTISHA KUPIGA MPIRA THEN AKAUPIGA BAADA YA KIPA KU MOVE KWENYE LANGO IWE AMEFUNGwA AU HAJAFUNGA PENALTY HIYO NI LAZIMA IRUDIWE KWA UPANDE WOWOTE ULE" sasa hapa sielewi hawa wachambuzi wa kibongo huwa wanafuatilia mechi za kimataifa au la na mfano huu mmnaweza kukumbuka mchezaji FRANK LAMPAD wa CHELSEA ya ENGLAND ambaye alipiga penalty 3 ambazo zote ZILIZAMA WAVUNI lakini ZIKAKATALIWA kutokana na MAKOSA YAFUATAYO penult ya kwanza kipa alitoka kwenye line kabla ya mpira kupigwa, PENALT YA PILI LAMPARD ALIPIGA KABLA YA FILIMBI KUPULIZWA NA YA TATU LAMPAD ALITISHA KABLA sasa sijui hawa wachambuzi wanafuatilia mipira ya kimataifa ua wao Vi......!!!

    ReplyDelete
  12. Kweli weye Mdau Rocky unafaa kuishia humu humu kwenye blogu. Hivi, hiyo ligi kuu yenye ushindani inatengenezwaje? Hebu tueleze. Unafanyaje uwe na ligi yenye ushindani? Unajua umeongea pumba tupu ila sijui kama unajua. Hujasema kitu. Hao Nigeria na Misri walifanyaje halafu kukawa na hiyo ligi? Pili, ingawa Maximo ameshasema mengi lakini hajawahi kusema kitu kama hiki.

    Michuzi endelea kuwapa watu kama hawa nafasi, hawawezi kusikilizwa popote duniani.

    ReplyDelete
  13. wana sir alex wao hawa wa misri kwani huyu kocha tangu nikiwa mtoto namwonaga na misri.

    ReplyDelete
  14. The Pharaohs 5 Taifa Stars 1

    The Pharaohs 4 Algeria 0.

    Halafu mnadai eti Maximo hajafanya kitu. Algeria waliweka kambi ya kuwatosha maana walijua wanakabiliwa na CAN na WC lakini wametandikwa 4. Sisi tumeweka kambi ya siku mbili tatu tukapigwa 5-1 watu wakadai Maximo hafai. Misri hawakufika walipo kwa miaka mitatu. Kutegemea Maximo atufikishe hapo kwa miaka mitatu au minne ilikuwa ni kumtaka ubaya tu.
    Wachezaji wa stars hawana passion...kocha wa Ivory Coast alikuwa na mawazo tofauti baada ya mechi na sisi. Hata kocha wa Ghana walipokuja kucheza nasi alikuwa na mawazo tofauti.

    ReplyDelete
  15. jamani walichofanywa waalgeria ni sahihi kabisa.....waalgeria natural wanahasira kwabahatimbaya ama nzuri wameshindwa kukontroll hasira yao.na chamoto wamekiona 4 mtungi...mi nimefurahi...sasahiv kunaukimya wahali ya juu mitaani...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...