Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:
Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden ni hatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi ya laptop na mapochi makwapani mwao.

Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.
Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kisha abiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.
Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.

Mbagala:
Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwa kuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu. Kundi hili hupora fedha, simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwa vipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.

Giraffe Hotel:

Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuacha mali za thamani ndani ya magari yao.
Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunja vioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windows na kuchukua kila wanachoweza.
Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at owners risk.

Posta ya zamani na mpya:

Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogesha magari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili. Watumia daladala wa Posta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoni wakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu. Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaacha ndani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo ya maegesho.

Bonde la Jangwani, Salenda Bridge na Bonde la Kigogo:
Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanya huo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatari zaidi. Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringi hadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama. Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuacha ukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.

Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:

Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi na kupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi. Maeneo haya yametulia sana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakini hayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili na nusu giza likiwa linaingi, maana utakumbwa na dhahama.
Daraja la Mlalakuwa, karibu na makao makuu JKT
Hapa watu wamesema weeeee wamechoka. Yaani watu wanavyoporwa kila siku kijua kikizama inaanza kuaminika kwamba wapiga loba ni askari wa hapo JKT ama wanashirikiana na hao vibaka. Wakazi wanajiuliza iweje sehemu nyeti kama hiyo pawe na vibaka? Wanatokea wapi?

TUTAFIKA kweli?
Afande Kova upooooooooo????

NB: Sehemu ambazo hazijatajwa, ikiwa hata mikoani na visiwani, msaada tutani wadau


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Hizo power windows zinazoibwa zikiachwa kwenye magari ni zipi...sijaelewa hapo? Mimi niko nje huku sipati picha ni nini kinaongelewa hapo maana power window ni kioo cha gari lako ambacho hutumia umeme wa gari kupanda au kushuka, Ni hicho huibwa?

    ReplyDelete
  2. Hongera sana mdau kwa kutuletea dondoo za kiusalama. Kwa kweli umefanya jambo kubwa kuliko hizo isara za usalama na plisi, ingawa wewe huna mgao wowote wa kodi zetu.

    Kamanda Kova, Hawa vibaka inashindikana vipi kuwakomesha?

    ReplyDelete
  3. "USALAMA WA KILA MMOJA NI MUHIMU"

    Huu ujumbe wa huyu mdau unatisha,usalama wa kila binadamu katika nchi yake ni muhimu saana katika maendeleo ya nchi,bila usalama italeta hatari ya wazalendo kuichukuwa sheria mikononi "Jugle Law" kwa mauaji ya kikatili.

    Nakubaliana na mtazamo wa afande Kova kujaribu kuja na "MIPANGILIO" mipya ya kupunguza hili tatizo la vibaka na majambazi si kwa sisi wazalendo pekee hata wageni wanaoitembelea nchi yetu wawe na usalama,bila ya usalama itaharibu sifa za nchi yetu.

    MJ-Denmark

    ReplyDelete
  4. Mdau tunakushukuru sana kwa hizo tips.

    Ni maeneo yanayoeleweka hapa mjini kwa muda mrefu lakini hayajapatiwa ufumbuzi.

    Polisi wetu wanafanya kazi nzuri ila tunawaomba wasiweke mkazi kwenye majambazi pekee wajaribu pia kuangalia jinsi ya kudhibiti vibaka maana nao kero kweli kweli.

    ReplyDelete
  5. Duh!! Kwakweli ni HATARI KUBWAA....ki msingi hakuna palipo na usalama, na jeshi la polisi lina kazi kubwa sana ukizingatia sehemu nyingine zinahofia kuwa washiriki wake wakuu ni askri wa jeshi flani au JKT nk... Zitungwe sheria kuhalalisha umiliki wa silaha nyepesi like bastola kwa raia as a measure for self Defense, haya ni mawazo yangu tu...

    ReplyDelete
  6. POLISI NJAA KALI WANASHIRIKIANA NA VIBAKA KUIBA NA KUGAWANA MALI,NANI ANABISHA?NISHAWAHI KUWA POLISI BUT NILIPOONA MAMBO KIBAO YAKUJIDHALILISHA WITHIN POLICE FORCE I DECIDED TO QUIT.NIKAENDA PCB NAKO HIVYO HIVYO WALARUSHWA WANASHIRIKIANA NA MAOFISA WA PCB KUGAWANA HELA YA RUSHWA,NIKAONA LA KAMA VYOMBO HIVYO NDO VIMEWEKWA KWA AJILI YA KULINDA MASILAHI YA MTANZANIA JE TUTAPONEA WAPI?SERIKALI WALIPENI POLISI NA WAFANYAKAZI WENGINE KAMA AFYA,COURT,PCB NA WENGINEO MISHAHARA MIZURI ILI NJAA ZISIWAFANYE KUTENDA MATENDO MAOVU.
    BY THE WAY KWA SASA NIPO USA HUKU POLISI HATA UKIMPA $ 1M HACHUKUI

    ReplyDelete
  7. ....kwa maana hii hakuna sehemu yenye usalama bongo maana naona kila sehemu imetajwa.watu wanaishije?na je kama sehemu hizi zisizo na usalama zinatambulika,kwa nini polisi na dola kwa ujumla hailifanyii swala hili kazi?au ndo kusema dola imekufa kabisa,maana najua dola yetu inalega,ila sikuwa naimagine kwa kiasi kikubwa hivi.je,wageni wakituambia kuwa nchi yetu si ya amani tutabisha.....?

    ReplyDelete
  8. Sehemu nyingine nje ya Dar ambayo ni hatari ni River Road jijini Nairobi, ikifika jioni unaweza banwa na watu ukakoswa msaada hapo! uwe mwangalifu sana ukiwa maeneo hayo.

    ReplyDelete
  9. Hongera sana uliyetufahamisha haya, na unafahamu umuhimu wa matumizi ya blog ya JAMII. NINAUHAKUKA KUNA MAENEO MENGI TU TUELEZE TAFADHALI.

    ReplyDelete
  10. kuanzia cococ beach hadi kwenye yale magorofa yanayobomlewa karibu na sea cliff hotel kuna vibaka wa kufa mtu kuanzia saa kuni na mbili watembea kwa miguu wapiga tizi wanakoma ukipata pancha ndo utajiuliza why?? kwa nini??/

    ReplyDelete
  11. MI naona ianzishwe sheria mwizi akikamatwa akatwe katwe vidole vyote.

    ReplyDelete
  12. jamani tumeisha halafu tunasema Tanzania kuna amani amani itoke wapi kwa mambo kama haya? Tafadhali Michuzi tunaomba upelekee taarifa hii tena na tena makao makuu ya polisi. Tusaidie baba yangu.

    ReplyDelete
  13. Kaka usisahau eneo la darajani kutokea Kamata hadi mataa ya Chang'ombe ni hatari tupu, maana Keko kuna camp kabisa za vibaka ambao hilo ndio eneo lao la kazi.

    ReplyDelete
  14. JK angetumia muda wa kukutana na wachezaji wa kigeni, kutembelea vituo vya police kuona utendaji wao

    ReplyDelete
  15. Maeneo ya bonde la kinondoni mkwajuni pia sio salama ukipata pancha tembea nayo, kuna vibaka wanaoshambulia kwa makundi na kuchukua mpaka viatu.

    ReplyDelete
  16. ukweli nakubaliana na wadau, kuhusu usalama wa hayo maeneo, ila kuna sehemu ambazo ni za hatari zaidi na ambazo watu wanaenda zaidi lakini hazijatajwa....

    1. BEACH COMBER HOTEL
    -Hii ni hatari sana nafikiri kuliko hotel zote mjini... katika wiki moja zinaweza vunjwa gari tatu kioo, halafu majibu ya utawala ni hayo hayo kuwa wao hawahusiki na ulinzi wa gari na mali yako. Na walinzi wanao wapo hapo hapo wanayaangalia magari. kama wezi si wao ni nini?
    -Agalizo: mnaotupeleka ktk vikao sehemu hii muangalie hilo au sehemu ingine salama zaidi.

    2.MLIMANI CITY:
    -Hapa napo ni balaa zaidi, maana hapa wanaiba na gari lote sio kwamba wanavunja kioo tuu, wanatupa vikadi vyao na pia ukivigeuza nyuma pia wameviandika "hawahusiki na ulinzi wa gari wala mali yako" si ndio wezi wenyewe hawa.

    -ANGALIZO KWA KOVA
    -Jee waajiriwa ktk haya makampuni wanafanyiwa screening ya kutosha? isije ikawa majambazi ndio wanaajiriwa huko? tusipoangalia tutajikuta tuna generation ya majambazi ambao wote ni walinzi hapa mjini.

    -Ukweli ni kwamba hawa walinzi huwa ndio wanawapigia simu hao wezi waje, pale wao wanapochungulia wakaona kuna kitu ktk gari cha thamani. na wakati wanavunja yeye ndio anawaangalizia usalama

    Michuzi naomba uliweke mwanzo hili......

    JESHI LA POLISI LINASHINDWA....TUMIA TAALUM YAKO YA UPASHAJI HABARI KUITAHADHARISHA JAMII.

    Mimi ni MHANGA wa hayo matukio..."mara tatu"

    ReplyDelete
  17. Mdau wa kwanza,wanazoiba ni zile power window switch.Ni kero kubwa huku asikwambie mtu,njoo likizo yakukute.

    ReplyDelete
  18. Anthony Luvanda (MC)January 08, 2010

    Asante Mdau Kwa Tips,

    Mimi ni kati ya wahanga wa eneo Salender Bridge. Nilishuka kujisaidia haja ndogo usiku wa saa 4 nikavamiwa na vibaka wawili wakiwa na kisu na rungu kubwa, uzuri nilikua fiti 'kijudo' nikawtoa knock-out, otherwise it could have been so worse.

    ReplyDelete
  19. mdau umesahau millenium towers,zile parking pale chini ni hatari mno,ndani ya nusu saa wanakomba kila kitu na cha kushangaza kuna walinzi.mi nilikombewa na kumuuliza mlinzi anasema hajui.pabaya mno!

    ReplyDelete
  20. Bradha Michuzi,

    Ongezea hapo kwenye hiyo list ya orodha - BONDE LA MKWAJUNI lile lililoko katikati ya Kanisa katoliki Magomeni mpaka kituo cha Basi cha Mkwajuni.

    Napo pia saa za usiku watu wachukue tahadhari

    ReplyDelete
  21. .......Mdau wa kwanza, unakaa nje hujui power window? Acha hizo, jamma kajitahidi kutueleza kwa makini kadri awezavyo,
    Au mliambiwa kukaa nje kazi yenu ni kukosoa walio bongo tu?. Njo bongo uliwe, kama unajidai hujui kiswahili.
    Bro Michu, Ondoa hiyo comment ya kwanza iwe ya mwisho, huyo jamma hana shukrani na maelezo ya mdau.

    ReplyDelete
  22. LOL...ni Dar es salaam yote imechafuka. hakuna pa kupita. kama kule ocean road nako kuna wzi basi Dar ya kuhama tu. Beach la maTX lilikua poa sana pale Ocean road...Bongo tambarare....
    Mwee lakini nichicheme kitu hata tunakoishi siku hizi na hii recession vibaka wapo.

    ReplyDelete
  23. MTEREMKO WA MAGEREZA UKONGA.
    Ukipata panchali hapa wewe sepa tu ukisimama basi ni balaa kwani kuna vijana wahuni wanategeshea hapa na kama kuna chunusi vile huwa haipiti siku gari halijadondoka hapa,likidondoka ndio furaha ya kunguru!!

    ReplyDelete
  24. mmesahau njia ya tandale uzuri watu wanavamia magari wakiwa na mapanga upora kila kitu

    ReplyDelete
  25. Kaka pale kwenye daraja la Mtoni kwa azziz ali, kuelekea mbagala(treni inapopita juu)mida ya usiku utasikia tu kitu kimerushwa kwenye gari,mostly jiwe,ukisimama umekwisha,utasombewa kila kitu. unatakiwa uende kwa kasi hadi maeneo ya njiapanda ya kijichi labda ndo usimame. Mi ishanitokea hiyo,jiwe lilirushwa, sijui lilipotokea hadi bodi ya gari ikabonyea!
    Be carefull na maeneo hayo pia!

    ReplyDelete
  26. Jamani eee!! kwa kifupi ni kwamba kwa Dar hakuna sehemu yoyote ambayo ni salama tena,ni kuchukua tahadhari tu,hao wakuvunja vioo kwenye parking siku hizi nao wanakuja na gari wanapaki ubavuni kwako wanafanya kweli,ukitokea kabla wanawasha gari wanatimua.Hapa dawa ni kukamata nakujichukulia sheria mkononi tu.

    ReplyDelete
  27. magomeni kwenye mataa, kuna watu wamevaa vizuri tu unakuta wako 2 lakini anakuja 1 kwenye dirisha la kushoto anakuambia umepata pancha, ukiwa unashangaa yule mwingine anatokea dirishani kwano na kama umevaa hereni au mkufu wa gold anachukua au kama umesahau dirisha la gari wazi na kuna kitu kama laptop anachukua haijalishi saa ngapi tena huwa wanategeshea mchana wakati wa joto siunajua siyo magari yote AC zinafanya kazi? Mie niliibiwa mkufu wangu wee acha tuu!!

    ReplyDelete
  28. Maeneo korofi zaidi yanajulikana,ni kwanini Polisi wasichukue hatua kuwanasa hawa vibaka?ni rahisi tu,wasuke mitego ya kushitukiza mara kwa mara.Au sio kazi yao? (Wakishanaswa makatwe vidole)

    ReplyDelete
  29. mnazi mmoja kwenye yale mataa kuelekea air port funga vioo saa zote asubuhi mchana jioni full stop vibaka wa pale wanajidai wanavuka barabara mara chwii washalamba kitu kwenye gari yani jiji la dar limekuwa na vibaka kila mahali kama nairobi ni wakora kila kona

    ReplyDelete
  30. michuzi tafadhali hii ikiwa kama blog ya jamii tuwekee kurasa special humu ndani ili wadau woote ulimwenguni wa blogu hii tuweke saini kumkumbuka simba wa vita

    ReplyDelete
  31. Maeneo ya kigamboni ferry akipita mzungu lazima alizwe simu au vipochi wanavyo wekea passport zao.

    ReplyDelete
  32. Mdau umesahau Ofisi za posta...ambapo vifurushi na barua zinafunguliwa na kuibwa

    Uwanja wa ndege.........ambapo masanduku na bidhaa nyingine zinadokolewa ama kuibwa zooooooooooooote


    Ndio inaitwa BONGO wizi aka Usanii kila mahali

    ReplyDelete
  33. njaa imezidi bongo wafanyaje? wakati mafisadi wanakula raha zao ,waacheni na wao wajipatie riziki kwa njia wanayoijiwa waaaaaaa

    ReplyDelete
  34. kimara kwetu hakuna vibaka ni mwendo wa majambazi kila kukicha vya moto nje nje huku tumeshazoea

    ReplyDelete
  35. Asante kwa kutupa taarifa. Kwakuongezea, sikuhizi hata huku uwanja wa Taifa kumeharibika kuna vibaka ile mbaya hasa siku ambazo kuna mpira ndo usiseme. Jamaa wanatembea kama kikundi wakitokea uwanjani ukiwaona kwa mbali tafuta jinsi ya kujihami kwani hawatakuachia na chochote ulichonacho halali yao. Eneo baya zaidi nikutoka Uwanja wa zamani (shamba la bibi) hadi keko.

    ReplyDelete
  36. mmesahau tabata relini (maeneo ya ami) pale ni noma ukiwa kwenye daladala na hata ukiteremka

    ReplyDelete
  37. Bila kutafutwa njia mpya ya kutengeneza ajira halali (rasmi na si rasmi), haya mambo hayataisha:
    Kodi ya kichwa irudishwe
    Vitambulisho vya uraia viwepo, kuonyesha kazi ya kila mtu.
    Polisi waongezwe na wawezeshwe.
    Polisi wawe wa kisasa (teknolojia.
    JKT iwe lazima kama zamani,kwa kila kidato cha nne.
    Kuwe na udiktekta kidogo kuhakikisha watu wanakuwa wawajibikaji.

    Hii ni kwa kuwa sisi tunaishi kienyeji sana, kila kitu kinaenda kienyeji na watu hawaogopi tena chochote.

    ReplyDelete
  38. Mimi nasikitika sana sisi binadamu hali ngumu ya nchi tunaumizana wenyewe kwa wenyewe.Kwa sababu hao vibaka wakiiba wanauza mitaani kwa bei poa na sisi wenyewe tunanunua ndiyo maana vibaka hawataisha lakini tukiwa na msimamo mmoja na kuhakikisha mtu anakuuzia kifaa chochote hakina risiti hakiko kwenye kasha lake usinunue na kama inawezekana ni kumripoti mtu kama huyo.Tukiendelea kununua vitu mitaai kwa sababu bei ni poa basi tutaendelea kuibiwa na jeshi la polisi liko tu linaangalia nchi inaendelea kuwa chafu kwa sababu wanaouuumia ni walala hoi.

    ReplyDelete
  39. NA KIKWETE KWENYE HOTUBA YAKE YA MWAKA MPYA ALISEMA KUNA USALAMA, USALAMA GANI? KWA VILE WAO HAWAIBIWI? SAID MWEMA EBU FUATILIA HILI SISI RAIA WA KAWAIDA, WALALA HOI TUNATESEKA, NA WEWE MICHUZI KAMA MWANDISHI WA HABARI MNATAKIWA KUFUATILIA HILI NA KWENDA KUMHOJI SAID MWEMA ATOWE MAELEZO KWA SISI WANANCHI PLEASE TAKE IT SERIOUS MAN!!

    ReplyDelete
  40. Kaka Michu pole na shukuli za kazi nyingi mkulima. Naomba uiposti hizi site ili wamatumbi waweze kuziangalia na kujua hali gani inayoendelea duniani na jinsi gani tunaweza kuepuka kwa sasa kwani tusipokuwa makini haya mambo yameshaanza kuingia kwetu taratibu kwa wakubwa kupewa misaada isiyokuwa na masharti ikiwa ni mojawapo ya mitego yao. Kwa leo sina mengi ila nitawapasha habari nyeti ili tuwe makini,tuangali kwa macho matatu na kusikia kwa masikio matatu.Ila nawasia je manajua kuwa kuna mpango wa kupungusa idadi ya watu duniani kwa kutumia vyakula vyenye sumu na chanjo ambazo zitakuwa na side effect in a long run?Be alert,aware watch out people. Site zenyewe ni WWW.Infragard.com,WWW.Bilderberg.com, WWW.Projectbluebeam.com or you can check on the yutube.com.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...