Kaka michuzi
naomba sana msaada wako kwani huko niendako sina mwenyeji Nataraji kufika mji huo wa Malaga, Spain nikitokea Dar es salaam siku ya Jumanne tarehe 27/01/2010 asubuhi lakini kwa bahati mbaya sina mwenyeji japo nimeshafanya booking ya hostel.
Natarajia kuwepo hapo kwa miezi 4 Naomba kama kuna mtanzania yeyote katika mji huu tuwasiliane ili niweze kupata mwenyeji kwani hata lugha (kihispania) nayo nayo ni tabu.
Tunaweza kuwasiliana kwa email osicstz@yahoo.com au simu no 0715 462281 lakini baadaya ya kuondoka Tanzania jamaa yangu mwenye namba 0784 297783 ataweza kutumika kutuunganisha.
Natanguliza shukrani
Mdau Emmanuel

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. We mtoto hebu tulia.Natumaini kiingereza chako ni kizuri tu nikilinganisha na kile wachokizungumza waspanish.Ukiweza kuongea kingereza huwezipata shida sehemu yeyote duniani.Utafika Spain salama kabisa na utaondoka salama.Utapata wenyeji wa kispanish na maisha utayaona poa sana,hata huo muda wa miezi mnne utaona kama siku mbili.Nirahisi sana kupotea Dar hata kama unaongea kiswahili cha kizaramo maana miji yetu haina sreet address wala zipcode.Wachina wamejaa Marekani na hawajiu kuongea kingereza lakini mwendo mdundo.Ukirudi Bongo tueleze mambo yalikuwaje.Seat back and ejoy your flight.

    ReplyDelete
  2. Hola! como estas???

    ReplyDelete
  3. kalale hotel wewe mwenyeji wa ninii unafikiriaa unaendaa shinyanga ulaya hiyo fala weweee eti mwenyeji ili ukalalee bure wabongo bwana msione kichaka mnataka kunya

    ReplyDelete
  4. mimi naishi hapa spain mwaka wa sita,na sitakikukaribisha watu wa namna hiyo..
    kama wewe unakuja kwenye mkutano si mnapewa ruzuku tumieni hizo,
    ila inabidi ujue kuma huku ni aghali kidogo,labda kwa wanigeria unaweza ukapata nafuu kidogo

    ReplyDelete
  5. Watanzania ovyoooo. Huyu jamaa amekosa nini mpaka ashambuliwe hivyo. Ameomba kama kuna mtanzania eneo analokwenda basi ajitokeze kuwa mwenyeji wake. Na hajasema kwamba anaomba mahala pa kulala wala kula, tatizo liko wapi. Kama hutaki kumsaidia kaa kimya, siyo kuporomosha mineno inayotia kichefuchefu hapa.
    Mdau wewe nenda zako Malaga na achana na hilo wazo la kutafuta mTZ huko. Wengine maisha yao magumu huko ulaya, wanafikiri kila mtu anashida kama wao.
    Niliwahi kukutana na wabongo London wakiongea kiswahili. Nilipowasalimia kwa kiswahili, ghafla wakajifanya wanaongea kiingereza na kujifanya si waswahili tena. Goddamn!

    ReplyDelete
  6. wala usiwe na wasi wasi ndugu yangu, kwanza kuwatafuta wabongo nje huko ni kutafuta matatizo tu wala usijisumbe kabisa. Kila siku hapa tunasikia kuna vyama vya watanzania huko nje, una maana huko Spain hakuna hicho chama au jumuiya? Sie sijui tukoje tuko tofuuti sana na mataifa mengine.

    Kama ni shida ya kuongea na watu, tuliza boli utapata watu kutoka Afika kibao wa kuongea nao, mimi niliona upweke mwanzoni nilipoenda mji mmoja nje, lakini mara moja nikapata marafiki kutoka Angola, Msumbiji, Jamaica, Madagascar, Mauritius, na tukaishi kama familia moja kwa mwaka mzima, tukipika na kula pamoja kila tukipatana nafasi, rangi zetu zilituunganisha.

    Kwa hiyo usitumie pesa zako nyumbani kwa mambo mengine ukitegemea kupata mteremko kwa wabongo, beba pesa zako ukiweza hata akiba beba ili uishi zako comfortable, Wabongo wenyewe watakutafuta utakapokaribia kuondoka, uwabebee mizigo ya kupeleka kwa jamaa zao na wewe uwalie jiwe usikubali.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 11:48 hasira za nini kaka??mbona sie tukija bongo hamtukaribishi majumbani kwenu kwa kuogopa sijui aibu kazi yenu kututafuta kwenye mabaa na kubeep simu tu.Hii Ulaya kaka tumeshawashtua wabongo wanaokuja kwenye tu short courses wanataka ulalo wa bure ili wasave hivo vi dollars.
    Mdau mwingine inawezekana ulikutana na sisi maanake huwa tunabadilisha channel tukiona wabongo wanataka urafiki kwa kiswahili chao....ndio hio.
    mdau wa north london

    ReplyDelete
  8. ndugu yangu naungana na mdau mmoja hapo juu katoa mawazo safi kabisa mimi nipo hapa marekani ukweli ni kuwa ulaya na marekani kama mtu umesoma shule na unajua english nzuri huwezi kupotea kabisa huku kwani kila nyumba ina namba kila mtaa una jina kila kituo cha basi kina maelezo ya kutosha kwa msafiri tena huku kama ni mara yako ya kwanza kufika ni bora kama una ulizia tafuta police ndiyo mtu mzuri wa kuuliza ok

    ReplyDelete
  9. Te te te ..hata mie naona wewe kaka unakiherehere sanaaa, kwanini unakwenda huko Spain kama huna mwenyeji?? Na kama unaenda kikazi au kishule ina maana utakuwa umejiandaa vya kutosha sio? kama hujajiandaa unataka kupewa vya kupewa bure bure na kusihiii utulize makanyagio yako kwenu utokako, sio kusumbua watu hapa..niko Spain lakini sorry sitaki kukukaribisha kwangu mtu hata sikujui kisa ni mtanzania tu?? Tulia wacha kisebu sebu...Asante sana.

    ReplyDelete
  10. Jamani wadau kama hamwezi kumsaidia huyu ndugu kuna haja gani ya kumtukana? Yeye hajasema kuwa nashida ya mahali pa kufikia alichosema hapa ni swala la mawasiliano "lugha" naimani alikuwa analenga maelekezo ya kawaida tu... sasa watu ni kutoa maneno machafu tu dhidi yake. Ndugu yangu hii ni kawaida kwa watu wengi walio nje wako tayari ku" pretend" kuwa wao si waswahili ili usije ukawauliza chochote utadhani una lengo la kuomba kwao. Kinacho shangaza wakiwasiliana na ndugu zao huku wanajionyesha kuwa wana mafanikio saaaana nenda kule kama utawaona.

    ReplyDelete
  11. Bwana mdogo usihangaike kutafuta wenyeji utapata usumbufu tu wa bure.

    Usifadhaike, wewe jichanganye tu na hata hao wazungu au jamaa kutoka Afrika. Mwanzoni inakuwa ngumu kidogo lakini baadaye utazoea.

    Ni vizuri ujifunze na culture nyingine uone wakoje siyo utanzania tu.

    ReplyDelete
  12. Mdau unayetaka kuja Spain, jaribu kutumia akili kidogo halafu omba kusaidiwa.

    1. Katika Internet unaweza kupata hoteli na kujua mahali wabongo wanapokutana hapa.

    2. Unaweza kuona bei tofauti za mahoteli katika kila mji.

    3. Unaweza kupata ramani ya lugha yoyote na ya mji wowote wa Spain ili usipotee.

    4. Hata kama ukikwama, kila eapoti na kona ya mji ina wafanyakazi wanaowasaidia watalii kupata mahoteli na ramani ya mji.

    5. Ulaya sio Afrika. Undugu hamna. Siku hizi story za kutofoana macho hamna. Kama huna fedha za kutosha, ujue kuwa si rahisi kupata msaada kutoka kwa wenzako.

    Safari njema.
    Amigo en Madrid

    ReplyDelete
  13. mweh. mjomba uku unakuja ulaya si songea. njoo kamili hata kama tukijuana utarifi wetu ni nje tu sitakukaribisha nyumbani kwangu ku lala.

    ReplyDelete
  14. mweee wee msafiri pole kwa mitusi hii,,,
    ila achana na izo za kutaka mwenyeji wee fanya linalokupeleka rudi bongo,watu wehu majuu na hawana utu wema walio wengi mwisho wakubebeshe cocaines ufie uko

    ila kuna watu wanajidaiii eti ukiwa nje,khaaa ulimbukeni huu?sasa mnavotukana apa ndo nn

    ReplyDelete
  15. ukifika tu nenda kwenye madisco ya wafrica utawabamba tu huko weeengi jamani eeh huyu ndugu anataka tu kampani na mtoko wa hapa na pale akiwa na wazawa sio kuwa ati anatafuta mahali pa kushukia acheni hizooooooo ni company tuuuu ebo!!

    ReplyDelete
  16. hola njoo kwangu basi chumba na choo bila msosi bei Euro 50 per night au unasemaje

    ReplyDelete
  17. Mijitu mengine Bwana kama huwezi kutoa wazo husituandikie matapishi yako hapa. Mtu ameomba kukutana na mwenyeji na sio kwamba anaomba mahali pa kulala ama chakula. Kitu cha kwanza amekwambia kuwa ameisha fanya bukingi ya hosteli. Halfu watu muwe mnakumbuka mlikotoka. Wewe ulipofika hapo mara ya kwanza ulipokelewa na watu wakakupa kila kitu. Sasa mtu ametanguliza kuomba kama kuna mwenyeji huko anakoenda, nyie umkaanza kutoa matapishi. Watanzania mnatia kinyaa pale mtu anapouliza kitu kwa busara na lugha nyororo. Inabidi tujifunza namna ya kujibu swali kutokana na kitu kilichoulizwa. Kama hunaona huwezi kujibu kistahiri basi unyamaze, make sio lazima tuone utumbo wa majibu yako hapa. Hii ni seheme ya habari ambayo tumewekewa kwa ajili ya kusaidiana pale inapowezekana, sio kutoleana matosi kama wengine wanavyofanya. Make inatia kichefuchefu sana. Kaka usiwe na wasiwasi utakuwa sawa.

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  18. hahahah!! mdau 0606huna lolote, i wonder if at all you r in spain.

    ReplyDelete
  19. mdau 0606 you must be nut, i wonder if at all uko spain coz you dont sound like one

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...