Hi ankal Michuzi,

Ebwana kuna jambo linatusumbua sana watumiaji wa zain lines tulio nje ya
Tanzania, awali kulikuwa hakuna tatizo lolote, ila kama siku nne zilizopita
tunapata shida ku-recharge SIM card zetu, maana hatuwezi kabisa na bado
hatujui tatizo ninini?
Tumejaribu kupiga 100 service line na jibu tunalopata ni kama tulivyozoea mwanzo, yaani kuongeza salio 138*Namba ya kadi then unapiga. Lakini hamna hela inayoongezeka wala kupata sms kuonyesha umefanikiwa kuongeza salio.

Inatupa usumbufu mkubwa kwani wengi wetu, ilikuwa ni njia rahisi kuwasiliana na familia na hata kuwatumia vijisenti kwa njia ya ZAP nk.
Tumejaribu kwenda kwenye ofisi za Zain huko tuliko, ila hatukupata mafanikio maana wametuambia the same thing kama tulipopiga 100.

Tunaomba wahusika wa ZAIN Tz kama kuna tatizo lolote juu ya hilo, tungependa kufahamu, kwani hadi sasa tuna vocha hadi za dola 120 ambazo tumeshindwa kuzitumia kabisa. Tumesha sajili SIM card zetu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Mdau,
Anthony
Khartoum-Sudan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hiyo ni kweli kabisa hata mimi nina week moja hapa DRC nimeshindwa ku-recharge simu yangu mpaka sasa nikitaka kuwasiliana na watu mpaka niombe simu za watu hapa kwa kweli kuna usumbufu mkubwa tunaomba ZEIN wasaidie kwa hilo.

    ReplyDelete
  2. Customer service ya Zain ni mbovu sana, sijui mitandao mingine. Customer service staff wao wako rude, halafu wamekalili namna za kuhudumia wateja, hawafikirii. Ukishamwambia nimefanya hivyo unavyonielekeza na sipati ninachokitaka wanakuwa wakali wanafikiri wewe ni mbumbumbu. Halafu Zain wako very expensive, ni kama wana hidden charges. Mimi ni mteja wa Zain toka 2006, enzi za 0787 lakini wameanza kuni-bore, najaribu namba ile natumia kupokea tu! Akina Twisa na yule bishoo anayeandika andika vtabu na makala magazetini, fanyeni kitu, sio mnakimbilia ma-promosheni na ma-advertisement tu mnasahau huduma bora kwa wateja na kupunguza bei zenu. Tigo wako very cheap, Voda wana cheka time na wateja wao wanafurahi. Fanyeni kitu kama mnajali wateja.

    ReplyDelete
  3. Mi nilikua mteja wa celtel tangu 2004 kipindi cha 0748 hadi 0784 290... nikahama nao kuja Zain hadi 2009 july niliposafiri, nimerudi january 4 naingiza line yangu kwenye simu ili nikasajiri ikaniambia sim registration failed. Nikaenda Zain pale opp na sayansi kijitonyama wakaniambia namba yako inatumika na mtu mwingine na ipo active tangu dec 12,2009.Kwa maana kuna mtu amenivua tayari. Nilibaki hoi maana kila nikihoji uhalali wa wao kumpa namba mtu mwingine wakati ile ni kama bank account wao walibaki kushikilia msimamo wao na kudai ati kama hujaitumia line kwa siku 90 wanaifuta kana kwamba laini hiyo ni mpya umeweka hela mara moja na hujaitumia tena hadi kipindi hicho. Sasa nikawauliza kwenye ile pakeji yangu yenye pin na PUK pamoja na kitabu cha maelekezo mbona sijaona hayo maelezo? na kwanini wafanye hivyo hali ukishaweka salio kwenye simu ilikua ikiniambia kwamba itaexpire baada ya takribani mwaka mmoja iweje wao ndani ya siku tisini wampe mtu mwigine namba yangu? na watu wengi nikikutana nao wananiambia we mbona unamwachia simu mtu mwingine si tunakupigia anapokea mtu mwingine tena kama ni za kibiashara anadai anauwezo wa kuwapa hizo huduma. Nabaki kusikitika na kuwaambia nitawapa namba yangu nyingine maana hawa Zain wamempa mtu namba yangu ileile hali kuna code nyingi kama 0787,0786,0785,0783,0782,0684 kwa nini wampe yangu yenye 0784?
    Yaani hadi sa hivi sijajua nifanye nini maana namba hii nimeiweka sehemu nyingi muhimu ikiwa kama anuani yangu na sasa anatumia mtu mwigine
    Kitu kimoja nilichowauliza nikawaambia je kwa mfano ingekua simu yenye ile namba ingekua imeibiwa baada ya muhusika kuuawa na majambazi na na ikawa imechukuliwa ile namba na polisi kama kkizibiti cha kusaidia katika upelelezi. Halafu ndugu wa huyo mtu aliyeuwawa baada ya muda kupita wakaipiga ile namba wakakuta inaita, kisha wakawataarifu polisi huyu mteja wenu mpya si ataenda gerezani? hata kama mtamtetea kwamba sie lakini si atakuwa ametabishwa sana kutokana na taratibu zenu hizo mbovu? walishindwa kunijibu kabisa.
    Wamenisikitisha sana hawa jamaa wa Zain.
    george10080@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. una haki kabisa ya kulalamika ndugu mteja,

    ila usichokifaham ni kuwa, kuna wakati kunakuwa kuna technical issue ambayo inaitaji muda ili kurekebisha tatizo,

    kwa mfano kwa sasa, tatizo limeshatatuliwa, kutokana na juhudi ya pande zote mbili ndugu,

    chukua vocha ya sudan na ujaribu kuiweka kwenye simu,itakubali,

    kwa weye mteja wa congo D'
    sina imani kama unayoyasema ni sahihi, kwani hii watuw a DRC wanaweza kuweka vocha vizuri kabisa ndugu.


    msichofaham ni kuwa zain inajitahidi sana kufuatilia matatizo ya wateja pindi linapotokea,

    ReplyDelete
  5. Mdau aliyesema Zain Customer care zero hajakosea. Unaweza hata ukaona hilo jibu alilotoa huyo Anonymous Mon Jan 11, 12:30:00 ambaye naamini ni mtu kutoka Zain. Kwanza hata kutoa samahani kwa usumbufu kwa wateja wa Sudan hakuna.Pili anakuwa defensive na kujaribu kuonyesha ujinga wa mteja, angeweza tu kusema " tatizo lilikuwa linashughuliwa na sasa limetatuliwa", sio kuanza kusema usichokifaham sijui nini. Tatu anamuignore huyo mteja wa DRC, ni kama anamuita muongo , angeweza kusema tutalichunguza tatizo au amuombe namba yake ili waweze kuwasiliana naye kujua tatizo lake vizuri. ZERO CUSTOMER CARE. Mwisho anatuambia "TUSICHOKIFAM NI KUWA ZAIN INAJITAHIDI SANA KUFUATILIA MATATIZO YA WATEJA", wateja gan hao iwapo sisi ndio wateja na tunalalamika hapa na unatuignore?
    Dharau na nyodo za kitoto!Acheni hizo!

    ReplyDelete
  6. ivi nyie kwani sisi tuna mitandao basi bongo??ushuzi mtupu tena hao zain ndo wapuuzi wakubwa
    niliapa kutonunua line ya zain kwakweli

    wizi mtupu

    ReplyDelete
  7. Mimi ni mteja wa DRC mpaka sasa naandika leo tarehe 11/01/2010 sijaweza kuingiza airtime kwenye simu yangu. Nashangaa huyo mtu aliyejibu kwamba hamna problem ana maana gani. Kwa kweli hii inaudhi sana tena sana. Ninapoleta tatizo langu badala ya kuchunguza ili kusaidia wateja wako unakataa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...