Waombolezaji wakiwa na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Swetu Fundikira, aliyeaga dunia asubuhi ya leo kwa kile kinachosadikiwa ni kutokana na kipigo kutoka kwa watu wanaosemekana ni wanajeshi.
Mwenye bazee la Afrika Magharini ni kaka wa marehemu, Ismail Fundikira, akifuatiwa na Mshama Fundikira ambaye ndio kwanza amewasili toka Tabora.
Hadi sasa haijajulikana atazikwa lini kwani mwili bado upo hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ukisubiri uchunguzi wa kina kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa vile hii ni kesi ya polisi. tutajulishana kinachoendelea kadri habari zitavyopatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Pole sana familia ya Fundikila kwamsiba uliowapata,hao wanajeshi waliotoa roho ya Raia inabidi wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwao kwani wameshazoea tabia ya kupiga Raia marakwamara,wakijiona wao ndio wenyemadalaka yote.hii hali imekuwa ikijirudia marakwamara nahakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao.

    ReplyDelete
  2. inalilahi wa inallah wajinun!haaaaaaaa ina maaana swetu huyu naemjua mimi ndo kafariki dunia au sijaelewa jamani!!mungu ametoa na yeye ndo ametwaa jamani!!namjua huyu kaka jirani yangu ana watoto wa kike 2 jamani au ukoo wao kuna swetu wengi kaka michuzi?poleni ndugu wa marehemu jamaniii duh jamani!

    ReplyDelete
  3. Dah inauma na inasikitisha sana. Nawapa pole sana wafiwa wawe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao. Lakini hao waliompiga si wanatakiwa kuwa ndani hadi hivi sasa au hawajulikani?? tatizo la hawa kina Afande Alufonsi na afande Petero wanajiona muingu they think they are above the law all the time na rigwaride lao!!! washikishwe adabu.
    michuzi na wewe ahsante sana uko mstari wa mbele sana katika masuala ya kijamii iwe furaha (Minuso) au shida (Vifo, ajali nk) ubarikiwe sana. pia uko mbele kutuletea habari zivunjikazo (breaking nyuuuz) sisi tulioko huku ughaibuni na michuzi glob twajiona tuko nyumbani, na bila michuzi glob twajiona tuko mbali na nyumbani. kaza buti mora atakulipa.
    Mdau wa Pajazzz+Titizzz

    ReplyDelete
  4. What a lawless country, and the perpetraitors will be let loose, God have mercy on Tanzania

    ReplyDelete
  5. inalilah...........hivi huyu ni yule jamaa alikua kwenye vidio ya mr paul zuena kama dr ama....

    ReplyDelete
  6. Pole Sana Familia ya Fundikila, inatia huzuni mtu kukatiswa uhahi wake tena na watu ambao walipaswa kuulinda uhahi wake...
    Sijui kama ndiye huyu Swetu ninayemfahamu mimi! Swetu ambaye Marehemu baba yake alikuwa anafanya kazi Posta na Simu Mwanza!Nakumbuka miaka hiyo nilisoma na Swetu mmoja shule ya Msingi Nyanza - Mwanza ila alikuwa mbele yangu (nilikuwa darasa moja na mdogo wake wa kike) na baadaye nimefanya kazi na dada yake mkubwa kwenye Agence moja inayojishughurisha na masuala ya Afya(ambaye pia alisoma na sis wangu Mwanza Sec!)
    Kwa kweli inasikisha sana, nashindwa ata kukubali kuwa hili nalo ni mipango ya Mungu.
    Allah awatie nguvu na moyo wa subira, Insha-allah
    inalilahi wa inallah rajiuun!

    Hussein

    ReplyDelete
  7. Swetu was a nice guy, I knew him personally and he was a great guy, very smart and cool - hiyo lugha wanayosema aliwajibu ya maneno makali mbona ni ya kawaida tu? Ila tunazidi kukosa imani na watu wanaolinda Taifa kwani sio wema kwa raia wa Taifa hili. After his death, and before his death I say May Allah rest his soul in eternal peace. Angalia sasa na ukiritimba wa Police mtu anaanza kuteseka baada ya kufa, badala ya sisi kufikiria kuzika wao wanamalizia uchunguzi.

    Pereira, Dar es Salaam

    ReplyDelete
  8. Big blow in Town, I say another big blow after Kim's death, Swetu was a nice guy, very smart and cool, I knew him personally and he proved to be a good person to society, one of the great guys in town. We know our people that's why we do posting these kinda comments.

    Lugha chafu? What is it? Tunasikia lugha chafu nyingi tu, even the soldiers use their own abusive languages, hii sasa tutaanza kuiogopa nchi yetu, and what now? The Police are delaying the funeral for investigation purposes, our man is gone and we want him to rest, how could you delay his funeral, you killed him and now you torture him, come-on.

    After his death, and before his funeral I pray that our man be rested in eternal peace and Allah forgives him.

    Pereira, Dar es Salaam

    ReplyDelete
  9. askari wanaotakiwa kutulinda ndio wanaotuua na kutubambikizia kesi

    siku zitadundwa mitaani wee ngoja!!

    ReplyDelete
  10. Natoa Pole kwa wafiwa wote.

    Hii inanikumbusha jambo moja ambalo nililisikia tangu zamani kuwa cheo ni dhamana. Hawa wameua bila kujua, nafikiri walitaka kumpiga awajue wao ni nani, kuonyesha ukuu wao. Kwa sasa watakuwa wanajuta pia kwani hata wakiachiwa damu ya marehemu itamlilia mungu naye atawaadhibu.


    Ushauri si kwa wanajeshi tu, kwa wote tusipende kuchukua maamuzi ya haraka hasa kuhusu kupigana ni hatari.

    ReplyDelete
  11. Wanajeshi wmezidi kujidai sana wakati wanajulikana kwa kupenda dezo.... Hata mimi kuna wakati walitaka kuniletea ubabe lakini nikajifanya mjinga ili kuwe na tofauti (sikushindana nao). Sheria kali ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wen
    gine

    ReplyDelete
  12. hata kama alitoa lugha chafu ndo mumtoe roho?? kwanza hiyo ni njia yenu ya kipuuzi ya kujitetea kwa vile hayupo keshafariki nyinyi wajeshi ni mabingwa wa kuvunja sheria mnajiona wababe sana hasa mkiwa mmevaa hiyo migwanda yenu mnajiona mungu watu ovyo sana elimu ndogooo inabidi kabla hamjaanza jeshi muwe mmemaliza hata form six manake mna ununda wa hali ya juu kama hao mgambo wa jiji ni mambumbumbu kazi kunyanyasa watu na elimu zao wakati nyie ni maziro tuu inaboa saana tunaomba mungu mfungwe maisha wauaji wakubwa

    ReplyDelete
  13. yani natamani watu waanzishe maandamano ya hiari hadi ikulu ili raisi afungue macho ajue jeshi lake lakulinda nchi na raia linavyonyanyasa wananchi utadhani watu wako iraq!!

    ReplyDelete
  14. Unajua baadhi ya hawa wanajeshi wanajiona wapo juu ya sheria.Kisa ni kwamba ajira yao ipo kwa minajili ya maslahi ya kulinda taifa.Basi hapo wanajiona niuntouchable.Mmoja wao akishambuliwa na mwanachi(haswa vibaka ambao hawachagui mtu) ,basi wao watakuja kuwaadhibu watu woote waliosika na wasiohusika(macho man priciple)katika mazingira ambayo tukio lilitokea.Lakini wao wanapouuwa raia au kutumia nguvu za ziada bila ya sababu za kimsingi wanajiona kama vile ni haki yao.Hii inasababishwa na udhaifu wa vyombo vya dola vinavyopaswa kushugulikia situation kama hizi(weakness in martial law court implementation kwa malimbukeni kama haya).Hata Kama wao ni wababe, ni upumbavu na ulevi wa kimamlaka unaowapelekea hawa malimbukeni kujichukulia sheria mikononi kisa? eti ni wanajeshi.Tatizo ndugu zangu kilio chetu ni kama cha samaki no body listens(the question is,for how long will they kill our brothers and sisters and no body says something about it?).Some of us might not feel it because it didnt happen to our close memmber of familly but guess what?one day it will come to you!!.Who feels it,knows it.Trust me!!!.Something has to be done to discipline these fools.

    ReplyDelete
  15. Kwa kweli acha sheria ichukue mkondo wake hawa jamaa wamezidi misifa na hii ndio iwe fundisho kwa wengine, waone faida ya kujitia mihasira sasa wananyea kopo na bado damu ya huyu kitukuu wa chifu itawaandama na kuwasakakma vizazi vyao vyote. Du!!

    ReplyDelete
  16. KIFO HIKI NI MATOKEO YA WATU KUKOSA KUHESHIMIANA KATIKA JAMII YA WATANZANIA.

    KULINGANA NA HABARI ZILIZOTOLEWA MPAKA SASA INAONEKANA HAPA KULITOKEA KUTOKUHESHIANA AMBAKO KULIZAA KUONYESHANA UBABE NA HATIMA YAKE NDIO HII.

    WAHENGA WALISEMA HESHIMA NI KITU CHA BURE.

    KWA SASA HILI JAMBO LIKO KWENYE VYOMBO VYA DOLA, TUSUBIRI TUONE LITAISHIA WAPI.

    USHAURI WA BURE KWA WADUA.
    JAMANI TUJIADHARI NA MAMBO YA MAGOVI. WALA USIJARIBU HATA KUMPIGA MTU KOFI. NA WAKATI MWINGINE UKIMYA NI JIBU ZURI SANA.

    ReplyDelete
  17. I hardly know Mr swetu,but I was in the same secondary school with his daughter Misuka.

    My sincere condolences to Misuka,Syalo and whole of your family,by your looks and behaviours connotates the kindness and all the good things about your late daddy.

    The justice must be saved to all those so called wanajshi who did such the evil thing.

    Poleni sana.
    William Jackson

    ReplyDelete
  18. WEWEW KAKA UNAYESEMA KUTOHESHIMIANA, JE, ULIKUWEPO? JE, USHAWAHI KUKUTANA NA HAO MAASKARI IWE POLISI AU JESHI USIKU NA UKAONA JINSI WANAVYONYANYASA RAIA HADI UWAPE KITU KIDOGO? NINA UHAKIKA BADO NA NDIO MANA NA WEWE UNAONGEA TU KITU USICHOFAHAM.. HATA KAMA MTU AKIKUTUKANA, HUNA MAMLAKA YA KUMPIGA TENA MBAYA ZAIDI KUMCHANGIA FOUR PPL vs ONE? COME ON,,!!
    KAKA MICHUZI, HAWA MAASKARI WETU, KUPIGA WAKE ZAO NI WAO, UHUNI WAO, UBABE WAO,KUCHINJA WAKE ZAO WAO, YANI KILA KITU NI WAO, INATAKIWA HUYU MHESHIMIWA DAVIS MWAMUNYANGE AONGEE NA WANAE NA KUWAKANYA KWASABABU KUSEMA UKWELI HAPA TUNAKOELEKEA SIO KWEMA, UKISIKIA VITA BTN WANAJESHI NA RAIA NDIO TUNAKOELEKEA SASA.. KWANI HATA RAIA NAO WATACHOKA KUONEWA BILA KOSA. HII NINAONGELEA MAJESHI YOTE, POLISI NA HAO WANAJESHI IWE JKT, AU JWTZ.. HAO WAUAJI WANAPASWA WAADHIBIWE VIKALI, HAKUNA CHA INSANITY HAPO WALA NINI, THAT WAS A PLANNED KILL COZ WALIMTOA KINONDONI HADI KUMBURUZA KOTE HUKO NA KUMPIGA NA NIA YAO NI KUUA TU,AMBAYO FINALLY WAMEFANIKIWA..
    R.I.P SWETU

    ReplyDelete
  19. HAO WANAJESHI WALIKUWA KWENYE JARIBIO LA KIVITA.NA HILO NI TATIZO LA TAIFA KUWAFUNDISHA WATU MAFUNZO YA KIVITA HALAFU HAWAWAPATII SEHEM YA KUJIPIMA NGUVU.SASA WAMEKUTANA NA RAIA MWEMA WAMEMFANYIA MAJARIBIO YAO.TUNAELEKEA WAPI I DONT KNOW

    ReplyDelete
  20. poleni wafiwa.
    kama sikosei adhabu ya kuuwa ni kunyongwa naomba wawanyonge mapema wasituyeyushe

    ReplyDelete
  21. Poleni sana ndugu zangu na marafiki zangu wa siku nyingi. Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi. Adamu fundikira naomba tuwasiliane kwa kupitia mtandao ili nipate contact zako. Michael.

    ReplyDelete
  22. Mgana Fundikira wamempoteza Swetu. The only way to get them relieved is for justice to be done. Nina maana hii kesi upelelezi umeshakamilika, kwani kwa kitendo cha askari hao aka "maiti" kama wanavyoitwa na makonda cha wao pia kushitaki kuwa aliwafanyia fujo ni dhahiri wanakiri kuwa walimpiga wao kwa kuwa aliwachokoza.

    ReplyDelete
  23. I hate them wanajeshi hawa! sijui wakoje? who do they think they are? hivi kwanini wasipelekwe kabul kwenye vita jamani? miguvu yao wanaitumia kwa raia ambao ni unarmed! to be honest with every body,hawa watu if left bila kuhukumiwa kifungo, hii nchi itakuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe..namaanisha mjeshi vs raia...hapo ndio kikwete na viongozi wenzie watajua kama raia inafika mahali wanachoka na kuwa sugu! hatujasahau ya zombe na wenzie dhidi ya raia wa madini, ditopile dhidi ya dreva wa dala dala, kuna mwingine kaua raia last year kisa mpira, i remember the one mr christopher, a chagga boy was also killed kipindi cha mipira ya mashindano flani ya africa i think kwenye ealry 90's or late 80's....kina marehemu mine chomba, baba shah....yaani list ni ndefu na utashangaa hakuna hata mjeshi mmoja amewahi kuchukuliwa hatua zaidi ya zombe na ditopile ambao waliwekwa ndani kiasi and then they were freed! shame on u tanzania for allowing ur citizens suffer because of cowards police/wanajeshi! hivi umoja wa mataifa huwa wanapata hizi taarifa? MICHUZI fanya hima taarifa hizi zifike kwa watu wa UN uone jinsi serikali itakavyokuwa serious on this! poleni watoto na mke wa marehemu, Mungu atawafuta machozi yenu siku moja, ur enemies will flee with shame. God will fight for u on this, trust him.

    ReplyDelete
  24. Tunaposhuhudia hawa ndugu zetu wanajeshi ambao ndiyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ndani ya mipaka yetu sisi raia wa kawaida tunapoteza matumaini.

    Matumaini yetu yanazidi kupotea hasa tunapoendelea kushuhudia mfululizo wa matukio ya uonevu wa wazi ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya hawa wanajeshi wetu. Hii inaweza kuwa inasababishwa na pengine viongozi wa juu wa jeshi kutochukua hatua stahiki ili kukomesha uonevu huu na kuwafanya askari hao kujifunza adabu.

    Tunafahamu kwamba wengi wa wanajeshi wetu elimu yao ni duni mno na pengine kwa vile wengi wao wamekuwa wakipata ajira hiyo kwa mtindo wa kujuana pale wanapokuwa wamevaa makombati yao wanadhani wako juu ya sheria na kwamba hii nchi ni yao pekee yao. Kama ni frustration za maisha wanayoishi huko jeshini ndizo zinawafanya kukosa adabu wajue kuwa haat huku uraiani kuna wengi wenye frustration tena kuliko hata za kwao.

    Wanashindwa kutambua kwamba hata wao wanalitumikia taifa kama ambavyo watu wengine kama walimu, madaktari, wamachinga, wabunge, mawaziri, wakulima n.k wanavyolitumikia taifa na kwamba hakuna anaetakiwa kujiona kwamba yeye ndiye mwenye nchi.

    Ni ulimbukeni tu.Kwanza maisha huko jeshini kwa sehemu kubwa wengi yamwashinda. Pia wengi wao tunawajua ni wavuta bangi,

    Utaona askari mwenyewe kakondeana na hata macho yake yamejaa matongoto lakini kwa vile kavaa makombati basi atajifanya mbabe kumbe ushamba tu.nendeni shule mkajifunze ustaarabu. Bahati mbaya sana ni wanajeshi wachache mno wenye ufahamu wa vitu kama hivi vya akina Michuzi ambao watasoma hizi comments kwani kama nilivyosema hapo awali wengi wao ni mbumbumbuuuuuu kabisa! Ovyoooooo! Mngesoma sijui ingekuwaje.

    ReplyDelete
  25. JAMANI TULIE KWA IMANI HUKU TUKIMUOMBEA MAREHEMU KHERI KWA MAULANA,LAKINI MASIKIO YETU NA SHAUKU YETU NI KWENYE VYOMBO VYA SHERIA MAANA NCHI YETU INA U MIMI FULANI NAMJUA FULANI KWA TAARIFA TULIZOZIPATA WALIOMPIGA MAREHEMU WALIKUWA WANNE MBONA WALIOKO KOROKORONI NI WAWILI SI AJABU HAO WAWILI WAKO NJE YA NCHI NA WAMEKIMBIZWA NA KINA FULANI HAYA WANASHERIA KAZI KWENU THIS TIME WANYONGE TUKO MAKINI HATUKUBALI NG'O SWETU WETU AMEKWENDA NA HAKI ITATENDEKA KAKA SETU ULALE KWA AMANI.

    ReplyDelete
  26. Poleni sana ndugu,jamaa, marafiki na watanzania kwa jumla, kwa kumpoteza mtanzania mwenzetu.
    Habari inasikitisha sana. Everybody has a right to live no matter what, amekutukana..amefanya nini..
    Wanajeshi wanne mnamshangia mtu mmoja. Kama si aibu na dhambi ni nini.
    Hata kama wanajeshi walikuwa wawili, why u all fight with one guy?
    I know many pple jeshini ni wale walioshindwa shule so they just got to use their weapons and kuchukua sheria mkononi as if wapo juu ya sheria. They cannot use their brains to solve a problem.(I repeat their brains to solve a problem) {many Heads, yenye brain but they dont know how to go about a single problem} I remember some years ago, i was going to school at shabaan robert sec. school..awa watu wakawa wamepark gari mbili mbele yangu, because it was in the morning nawai geti lisifungwe& some other citizen wanawai makazini mwao, we decided kupita kwenye njia kidogo cha pembeni. it was a problem, they pulled us over and they started provoking. It seems jeshi lina haki ya kufanya kitu ambacho normal citizen utakula kichapo.
    Tanzania nchi yangu but kurudi majaliwa, hata nikirudi my licence to defend myself itakuwa kiunono. Mana that's the way to live in Tanzania ubabe kwenda mbele. Sijui tutabadilika lini.
    May God bless the country and the people.
    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. amen
    Damu ya mtu haiondoki bure Mungu uwa analipa hapa hapa duniani. It's very sad! Wanajeshi wanaitaji mafunzo ya ki-akili pia. Not kujua kuonea tu!! cha kushangaza wanne mnamchangia one guy!! dah!! Mungu atalipa!!

    Mtanzania,
    U S A..

    ReplyDelete
  27. mshama mkala na familia yote ya fundikila poleni sana mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na mpendwa wenu lakini hawa wanajeshi waliomfanyia vibaya hakikisheni wanapanda kizimbani hii nchi imekwisha jamani inatia uchungu sana michuzi tunashukuru sana kwa kazi yako mungu akupe maisha marefu na afya njema

    ReplyDelete
  28. mshama mkala na familia yote ya fundikila poleni sana kwa msiba mkubwa wa ndugu yenu mwenyezi mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu inasikitisha sana michuzi mungu akupe afya njema na maisha marefu kwa kazi yako iliyo tukuka tunaomba anzisha kitabu watu tuchange pesa kuakikisha awa majambazi wanafika mahakamani please RIP SWETU

    ReplyDelete
  29. POLENI WANA FAMILIA KWA HUU MSIBA.

    THESE KILLERD SHOULD FACE PUBLIC EXECUTION AT MNAZI MOJA!! HUU NI UTOVU WA NIDHAMU ULIO KITHIRI.MIFANO INAANZIA KWENYE KUTUKANA WATU WA CHINI KWENYE ATM.

    ReplyDelete
  30. WATANZANIA nendeni hapa mjionee wenyewe huu unyama!!!

    WWW.GLOBALPUBLISHERSTZ.COM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...