
Bondia wa Tanzania Rodgers Mtagwa amepoteza pambano muhimu siku ya Jumamosi huko Madisson Square Garden New York la kutafuta mkanda wa ubingwa wa uzani wa Feather wa shirikisho la ngumi la WBA dhidi ya Yuriokis Gamboa wa Cuba.
Pambano hilo ambalo lilihudhuriwa na watanzania kadhaa waishio Marekani na hata Uingereza liliishia katika raundi ya pili baada ya Mtagwa kuangushwa kwa mara ya pili na refa kusimamisha pambano hilo.
Pambano ambalo lilionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya HBO lilitangulia pambano jingine la kugombea taji la WBO katika uzito wa Bantam kati ya Juan Lopez wa Pueto Rico na Steven Luevano wa Carlifornia ambapo Lopez alifanikiwa kumnyang'anya taji hilo Steven Luevano kwa KO raundi ya 7.
Kwa habari zaidi za pambano hilo na picha ungana na www.sundayshomari.blogspot.com
Whater hake
ReplyDeleteKwanzia lini MR. Mero anaitwa Bw. Kwayu?
Yooo!!, if u a hater for any how don't try to provide wrong information kwenye blog ya jamii.
Yes Mr Mero is in New York, and he is a very good guy working for Tanzanian Mission.
I dnt understand why everytime akipostiwa kwenye hii blog anakuwa haandikwi jina au kuandikwa majini yaajabu.