Bwana Michuzi

Nashukuru kwa kunipa nafasi niwapongeze Wabunge wazalendo, kutokana na maamuzi yao ya kuamua kung’atuka wakati bado wana uwezo wa kufanya kazi. Kitendo cha Mhe Keenja kutangaza kutogombea Ubunge tena jimbo laUbungo ni cha Kizalendo na kinachoonyesha ukomavu wa kisiasa na uelewa halisi wa Matatizo ya Watanzania.
Kama Tanzania tungekuwa na akina Keenja, Mzindakaya , Pius Ng'wandu na wabunge wengine walioamua kuachia madaraka kwa uhuru wao, Tanzania isingekuwa na viongozi wanaojipenda kama tulionao leo.

Mheshimiwa Keenja, anaacha historia nzuri sana katika siasa za Tanzania, ikikumbukwa kazi aliyoifanya ya kuisafisha Jiji la Dar baada ya Halmashauri kufutiliwa mbali na Sumaye.
Mhe Keenja ameweka maslahi ya taifa mbele kwa kutambua kuwa Dodoma imefika wakati tupeleke mawazo mapya yenye uwezo wa kuchambua na kutatua matatizo ya wananchi.

Katika Bunge lijalo tunahitaji Wabunge wenye uchungu na nchi na rasilimali zake. Tunahitaji tubadilishe utamaduni wa kuongea nje ya bunge na kunyamaza ndani ya bunge. Wazee walioko bungeni ni wazee wenye busara sana. Ni Wazazi wetu ambao wameitumikia nchi yetu kwa
mioyo yao ya Upendo.
Wabunge wengine walipata ajali ama walifariki wakitoka kuwasikiliza wananchi. Yote haya tunayatambua sisi kama vijana, na hatupingi wala hatukatai hata kama wataamua kuuendelea kuwa Bungeni mpaka miaka 100 ijayo. Lakini ninachopenda kuwaaasa ni kitu kimoja, kwanini tuwe watoto wao halafu wasituamini kama tunaweza kuwa wasaidizi wao pale wakapozidiwa nguvu katika shughuli zao.
Muda umefika Wazee wetu watuamini sisi vijana. Sio busara kwa Kijana wa Kiafrika kusimama kwenye Jukwaa kuwashambulia hawa Wazee wetu ambao hata kama tungesema tuwalipe dhahabu na almasi hazitalingana na thamani ya utumishi walioonyesha kwa wananchi.

Utamaduni wa kuacha madaraka kwa hiyari ni heshima kubwa sana katika Jamii, Muangalieni Rais Mandela, kama Mandela angeamua kubadilisha Katiba ili aweze kugombea Uraisi kwa miaka 27 sawa na miaka aliyokaa jela, mimi kama mwafrika ningekuwa wa kwanza kukubali.
Lakini Mzee wetu aliona kuwa Urais haukuwa shida, bali shida ilikuwa ni kasi ya kuwaunganisha Waafrika kusini kuwa Taifa moja baada ya miaka nenda rudi ya Ubaguzi. Kuna wazee wengi sana ambao tunahitaji kuwasikia siku zijazo wakifuata nyayo za akina Keenja.
Kama kijana wa Kiafrika ninafikiri wakati umefika tuwatambue Wabunge walioamua kuachia madaraka kwa hiyari yao, tuwawekee "Red Carpet' tuwaimbie wimbo wa Taifa, tuwashukuru kwa Utumishi wao, ili kukuza utamaduni wa kustaafu kwa hiyari.

Zaidi ya yote napenda kuwaongea na vijana wenzangu, kuwa zile siasa za kuwaita Vijana Taifa la Kesho ziondolewe, kwasababu taifa ni vijana na Watoto. Sisi ndio tutakaokwenda vitani, sisi ndio tunaojenga mabarabara na kulima. Kwanini wazee wasituamini kuwa tunaweza pia kuongoza?.
Nitachukua Likizo kwa ajili yako wewe kijana mwenzangu, nitakuja kukusaidia kupiga Kampeni utakapoamua kugombea kiti chochote kile ili mradi umeonesha hari ya kuitumia nchi yako. Ninapoongea na Vijana ninaongea na Issa Michuzi na Vijana wote wa Kitanzania. Matabaka tunayojenga ya kuwaita wenzetu watoto wa vigogo na walalahoi inatugawa zaidi kuliko kutuunganisha. Haijalishi umetoka Mkoa gani, au wazazi wako wanafanya nini, jitokeze tukupeleke Dodoma ukaitumie Taifa letu.
Vijana wengi wanadai siasa za Tanzania ni hatari lakini Martin Luther King alisema "The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort and convenience, but where he stands at times of challenge and controversy,.... I submit to you that if a man hasn't discovered something he will die for, he isn't fit to live"
Kwa maneno haya namkumbuka Mh Amina Chifupa, ambaye alijitoa mhanga kupambana kwa ajili ya Taifa la Vijana. Mimi na wewe tuna kazi ya kufanya ambalo ni kulitumia taifa letu. Kwa wale mnaoishi nje ya nchi yetu, nafikiri wote ni mashahidi kwa jinsi vijana na raia wa maitaifa hayo wanavyozipenda nchi zao, lakini ukisoma historia yao utakuta kuna kitu kinawachowafanya wazipende nchi zao. Mwalimu Nyerere alisema "Freedom to many means immediate betterment, as if by magic.
Unless I can meet at least some of these aspirations, my support will wane and
my head will roll just as surely as the tickbird follows the rhino.”

Nguvu na maarifa tunayo, Nia na malengo ya kutumikia taifa letu tunayo. Tusimame kama watoto wa baba mmoja tulijenge taifa letu. Tutafute suluhisho ya matatizo ya wazazi na kusimamia wadogo zetu tukitambua kuwa wanakua na kutuangalia tunakoelekea.
Sote ni Watanzania kwanza halafu unafuata U-CCM na U-pinzani. Kama tutaweka Utanzania mbele, tukafanya kazi kwa bidii, tukawa na uchungu na nchi yetu, tukagawana Rasilimani ya Nchi kwa uwiano sawa, tutazidi kupendana na kuendelea Kulijenga Taifa la Watanzania lililo imara lenye kukaribisha wageni kuja kushuluhisha migogoro ya mataifa yao kwetu.

Aksanteni sana
Mungu Ibariki Tanzania
Kuja WP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. US-Blogger)
    wee kuja unaumwa. what the hell in the world are you talking about? bwana nenda kwa Dr. Shayo ukapate Darasa kabla ya kuruka kwenye hizi anga za watu, You are a dead rat. if you fail seek help from other experts

    Dr.US Blogger
    Alumni, Oxford Univesrity
    Economics Dept.

    ReplyDelete
  2. SIMBAULANGAJanuary 23, 2010

    HUU NDIYO UZALENDO......!
    The law to allow Tanzanians to hold dual citizenship should finally be enacted by the end of the year, Foreign Affairs and International Co-operation minister Bernard Membe said yesterday.

    Speaking in Dar e s Salaam at an International Organisation for Migration (IOM) meeting, Mr Membe said research conducted on the proposal had established that the new law would not harm the country.

    "The government is regretting locking out Tanzanians overseas during the 49 years of our Independence, while some African countries have been granting dual citizenship to their people," Mr Membe said.

    Tanzanians living abroad will receive the news with jubilation, as they have for many years campaigned for the introduction of such a law to enable them to belong to both their host countries and their motherland.

    Many have complained that lack of such a law disadvantages them, as it denies them opportunities they could access if they were citizens of the countries where they work.

    Yesterday, Mr Membe explained that the issue had taken many years to conclude because the ministry did not wish to "rush such a sensitive issue". He added: "We decided to conduct a thorough research before introducing this law, which deals with the basic rights of a person."

    The research had enabled the government to establish that dual citizenship "is not bad, as some people were trying to depict it".

    ReplyDelete
  3. kuja mbona haueleweki huko kila sehemu? shida yako ni nini ushabiki? kama unatak kuwa kada wa CCM basi tafuta mdahmini siyo kuropoka...pole sana subiri wabeba boxi waamke

    ReplyDelete
  4. HUYU KUJA ANAMPONDAGA YOHANA MASHAKA HUKU ANAJARIBU KUMUIGA KWENYE UANDISHI WAKE UCHWara. KAZA BUTI WP KUJA

    ReplyDelete
  5. ina maana waosha vinywa wako majuu tuuu manake sie ndo tumelala saa hii na wengine ndo kumekucha acheni hizooo hata huko waosha mouth kibaoooo nyoo

    ReplyDelete
  6. Mimi ninaona huyu jamaa ana haki ya kuandika kwani anajaribu kueleza mawazo yake. si lazima tukubariane naye lakini ni vizuri kutumia lugha nzuri ili kukataa au kukubari mawazo yake. Swala la wawakirishi wetu kama wabunge ambao wametumikia wana nchi kwa muda mrefu hawana budi kung'atuka endapo watako penda kufanya hivyo. Performance yao inakuwa judged na wana nchi katika majimbo yao.

    Ahsante.

    ReplyDelete
  7. magreth Lucus ( Canada)January 23, 2010

    We Kuja, acha kudandia vitu ambavyo huwiwezi. aliokuambia umtafute dr shayo akupe shule anakutakia mema kabisaa. Dr shayo, Mashaka John na January makamba wako mbali sana na michango yao sio lazima wawe wabunge.
    Ninaamini taifa linawatambua, na itafikia kipindi michango yao itapewa kipaumbile

    ReplyDelete
  8. @magreth Lucus ( Canada)
    huyu kuja hawezi kulinganishwa na Dr. Shayo, John Mashaka au January, kwanza aliyoyaandika hayaeleweki. Wale ni wataalamamu na wasomi wenye upeo wa hali ya juu

    ReplyDelete
  9. kuja, mshikaji nitafute. tumesoma pamoja na kumaliza shule pamoja pale community college alabama mwaka jana. vipi issues haule@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. Kuja kumbuka kuwa hao wazee unaowasema waliingia madarakani wakiwa vijana kama wewe lakini sijui ni kitu gani tunachoweza kujivunia kutoka kwao? ndio maisha bora yamepatikana lakini kwa kikundi kidogo cha watanzania wateule. asilimia 90 ya watanzania wanaishi kwa kudra ya muumba (ikiwa ni pamoja na mvua zake!). ujana au uzee si hoja, hoja ni kuwa na viongozi wenye dira. kama ni kutaka kwenda dodoma au kwingineko (iwe ni kwa tiketi ya ccm au ccj) aende dodoma akiwa anajua anakwenda kulitafutia nini taifa. kwa mfano, ukiwauliza waliopo sasa hivi, vijana kwa wazee, kwa nini wako dodoma utashangaa majibu yao kama sio kukutumbulia mimacho!!!

    ReplyDelete
  11. Jamani ndugu zangu ni yale yale, siku zote tukombele kupondana, kama mtu alichosema ni kibaya si umkosoe , mbona tunamshambulia sana ndugu yetu hayo ni mawazo yake na ya kwako ni yapi?
    Yangu ni haya: ndugu Kuja umeongea vizuri sana hasa ukizingatia kuwa katika bara zima la Afrika ni viongozi wachache wanaachia madaraka kama Kaenja. Hilo lazima tulijue na tulifanyie kazi, pili mchango wa vijana katika kujenga nchi pia ndivyo inavyotakiwa kuwa, ila nadhani suala ambalo umesahau ni kuwa kwenye katiba yetu kuna umri unaotakiwa-labda tuanzie hapo halafu tuendelee na vigezo vingine. Na maanisha lazima katiba yetu iwe wazi katika nyanja zote mbili ya umri wa kustaafu na umri wa kugombea viti mbalimbali.
    Na mwisho ni suala la vyama mimi kinachoniumiza ni kuona wagombea wale wale kila mwaka , hivi hakuna watu wengine wanoweza shika nafasi zao. Angalia USA, France, UK, Ghana, mtu anagombea mara moja akishindwa basi anamwachia mwingine. Nadhani ni mifano ya kuigwa. Dr Shayo, Mashaka na wengineyo siyo kigezo cha kupima mawezo ya wengine. sote ni watanzania na mawazo yetu ni ya muhimu hata hatukubaliani katika masula fulani fulani kulingana na mtazamo wa kila mmoja wetu. Swali langu ni, je watanzania wanahitaji nini ili wapige hatua mbele zaidi na kwa kasi?

    ReplyDelete
  12. Hata sikutaka kuchangia huu ujinga lakini anyways... Kosa lililofanyika hapa ni mwandishi kujitaja jina. Watu wengi wanaakili fupi kama kuku. Ukitaja jina wanaacha habari nzima na hoja zote zilizoandikwa na kuanza malumbano ya kum-discuss mwandishi. Forget about who wrote the msg and discuss the issues and ideas put forth

    Huyo kijana either jina lake ni kuja au kwenda ametumia uhuru wake kuongea mawazo yake. Tumpongeze au kumkosoa kwa hoja bila kujali who he is. Thats what it means to make the needs of our republic paramount above any personal or group interests.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...