
Sio tutoe tuu msaada wa mashuka, bali tuwatandikie kabisa’ ndivyo wanavyoonekana kufanya maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma, PSPF wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga (wa kwanza Kulia), Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bw. Ali Kiwenge, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE, Godfrey Ngonyani WA PSPF na Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd, Bi. Mary Haule (Kulia) akisubiri atandikiwe. PSPF, imekabidhi taasisi hiyo mashuka 250 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 4 kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.





Habari na Picha na Pashal Mayala
Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma, PSPF, unaendeshwa kwa mafanikio makubwa, yanayopelekea kuzidi kutoa mafao bora kwa wanachama wake, ikiwemo mikopo ya kujenga au kununua nyumba kwa wastaafu waliobakisha miaka 5 kabla ya kustaafu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga, mashuka 550 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 8 kwa Hospitali za Temeke na Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd zote za jijini Dar es Salaan, kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.
Bibi Mmanga amesema, mafanikio hayo makubwa ya PSPF, yanatokana na juhudi zinazofanywa na uongozi na wafanyakazi kwa ujumla, ambapo mfuko huo unapata faida kubwa katika vitegauchumi vyake mbalimbali, vinavyo zalisha faida kubwa hivyo kuboresha mafao ya wanachama wake na ziada kutumika kwenye kutoa huduma za jamii vikiwemo vifaa na vifaa tiba kwa mahospitali.
Naye Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bw. Ali Kiwenge, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE, amesema, zaidi ya kutoa mafao ya uzeeni, mfuko huo wa PSPF unatoa mafao ya ulemavu, mafao ya warithi, mafao ya wategemezi na msaada wa mazishi. Sambamba na mafao hayo , mfuko huo pia unatoa mikopo ya ujenzi au ununuzi wa nyumba kwa wanachama wake waliobakiza miaka 5 kabla ya kustaafu.
Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Temeke, Dr. Aisha Mahita, aliushukuru mfuko huo kwa msaada wake wa shuka hizo 300 ambao amesema utasaidia sana kupunguza nakisi ya mahitaji halisi. Hata hivyo, alisema hospitali hiyo bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawa, vitanda, majengo na vifaa tiba kufuatia ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa na hospitali hiyo, hivyo ametoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa PSPF.
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd, Bi. Mary Haule, amesema hospitali hiyo ambayo ndio pekee ya rufaa za ugonjwa wa saratani hapa nchini, inakabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa, hali inayopelekea kuongezeka kwa mahitaji ya miundo mbinu, wafanyakazi, madawa na vifaa tiba ili kukidhi mahitaji halisi.
Mfuko huo wa PSPF ulioanzishwa mwaka 1999, unaendelea na kampeni yake maalum kuzisaidia hospitali mbalimbali nchi nzima kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, mafanikio ya miaka 10 tangu kuwepo kwake. Kesho PSPF itatoa msaada hospitali ya Temeke na keshokutwa, Hospitali ya Ilala.
Hii habari inatupunguza machungu yamajeraha tuliyoyapata katika vita ya RICHMOND,BOT,EPA na nyengine nyingi ila makovu yataendelea kubaki mwilini,nimfano mzuri wakuigwa na sekta nyingine zikiwemo za serikali,kama itaendelea namna hii basi malalamiko hayatokuwepo kutoka kwa wananchi,Big UP PSPF,kip it up.
ReplyDeleteHongera Dr.Asha kwa kuwa Mkurugenzi mapema! Lakini unawakumbuka Dr Jella Noordin na Mh.Mkama Constantino waliokupatia nafasi ya kusoma Ukraine na kukupokea na kukulea huko wakati ulipofika kuanza masomo yako ktk mji wa Kharkov kabla hujahamia Odesssa Medical University. Inabidi uwakumbuke sana maana wasingekuwa wao basi labda hata usingeweza kupata nafasi ya kwenda kusoma Ukraine. Kwa sasa Dr.Jella yupo Bongo waweza ukamtafuta na kumsalimia kwani ni mtu aliyechangia sana ktk kufanikiwa kwako kupata elimu hiyo.
ReplyDeleteMh.Mkama bado yuko Europe.
Nakutakia kazi njema.
Mwanachuo mwenzako.
Go Dr. Asha! Madaktari wote Africa wanapaswa kushukuriwa maana mazingira yao ya kazi ni magumu sana; kwa sisi tuliobahatika kutoka nje ya nchi na kulinganisha hali za vitendea kazi mahospitalini huwa najiuliza how did we survive? Mungu awabariki waganga (madaktari na wauguzi) Africa nzima.
ReplyDeleteHongereni watoaji na wapokeaji wa hayo mashuka.Lamuhimu kwa ndugu zangu wapokeaji ni utunzaji wake, yasije yakaishiya kwenye mikono ya wasiowaaminifu,kuanzia kwa wafanyakazi,wagonjwa na hata watu wengine wabaya.Kwa uelewa wangu kumekuwa na utolewaji wamisaada ya marakwamara kwenye hospitali zetu,lakini misaada hii wakati mwingine imekuwa ikiishia kwenye mikono isiyo miaminifu.
ReplyDeletemdau Jan 17, 11:48pm umeniacha hoi kwa ushauri unaompa Dr Asha, inaelekea ulikuwa umempania sana nafikiri hajalipa fadhila kwa hao uliowataja au we ni mmoja wa hao watu. there was no need for all the unnecessary information. Get a life. Huyu dada simjui lakini sidhani kama amefurahi kumwanika hivyo kwenye globu to me ni kama hujasoma vile though you claim to have been with her in Ukrane for studies.
ReplyDeleteDk. Asha hongera kwa kazi, kama kuwatafuta hao wanaoelezwa walikusaidia hilo si hoja, kwani shule ulianza kusaidiwa na wengi tangu primary, secondary na chuo, kama fadhila utawalipa wangapi. Kikubwa kazi buti watumikie Watanzania vilivyo.
ReplyDeleteKweli huyo mshamba hapo juu ana njaa kali. Yanakuhusu nini wewe? Kama una wivu panda ukazibe! Mtoto huyo kaajaliwa mtasema mtachoka anapeta tuu, ni ubongi wake ndiyo ukiomfanya akafika hapo na siyo mtu yeyeote aliyempokea airport au kumfadhili. Kama wewe ni mwanachuo mwenzako then elimu haikukusaidia maana unaact kama watu wasioenda shule na hawana ustaarabu. Find a way to deliver the message kwa mtu privately at the end of the day WHO CARES ABOUT WHO DID WHAT? BE CIVILISED NA KUACHA USHAMBA WA KUWAUMBUA WATU NA UZUSHI. KAKA ISSA NAOMBA USIIBANIE HII PLS. Dr. Asha achana na wenye wivu kazi yako tunaijua nakusubiri kukuona utakapokuja states soooooooon! Huyo anaedai kuwa ni mwanachuo mwenzako siajabu bado anarudia madarasa na hata hiyo degree hajaipata!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMdau Jan 18,06:43:00 PM unaonekana ni mshamba ambaye hujaenda shule na huko USA ulienda kimaajabu kwa ajili ya kubeba maboksi.Angalia ulichoandika ni utumbo mtupu,kwani mtu alipotoa maoni yake ndiyo kwa upande wako ni wivu huo. Utaendelea kubeba maboksi mpaka kesho na siku hizi US siyo deal na kusema kuwa unamsubili kumpokea US atakapokuja huo ni ushamba wa hali ya juu.Kaka Michuzi bandika hiyo aone huyo mbeba maboksi.
ReplyDeleteMy dear mshamba ni mshamba tuu. Njoo USA nikuajiri, si kila mtanzania aliye USA anabeba box! . Na sina haja ya kuyaandika yote haya in public kama mshamba mwenzio hapo juu anayetaka kumvunjia hadhi mwenzake kisa wivu! Kama una ubavu si unajua cheo cha DR Asha? na ofisi yake kwa nini usimtumie barua ya kumweleza hayo uliyoyaandika hapa kwenye mtandao? Kubali yaishe huu si ustaarabu na elimu wewe hukuipata. Kwa bahati mbaya BOX sijui linabebwaje labda wewe unipe experience yako kama unajua.
ReplyDelete