Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dr. Meshack Shimwela, (Kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma , Bibi Hawa Mmanga (Kushoto), maa baada ya hospitai yake kupokea msaada wa shuka 300 na foronya zake, zenye thamai ya Shilingi milioni 5. Katikati ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bibi Edna Mangesho, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana. PSPF, imekabidhi Hospitali hiyo mashuka 300 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bibi Edna Mangesho, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana (Kushoto) akikabidhi shuka kwa Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dr. Meshack Shimwela, (Kulia) , huku wauguzi Grace Mtweve na Itima Francis wa hospitali hiyo wakishuhudia, katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo mwishoni mwa wiki. PSPF, imekabidhi taasisi hiyo mashuka 300 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga (Kushoto), na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bibi Edna Mangesho, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana na Kushoto wakitandika kitanda cha wagonjwa Hospitali ya Amana mwishoni mwa wiki. PSPF, imekabidhi taasisi hiyo mashuka 300 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga (Kushoto), na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bibi Edna Mangesho, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana na Kushoto wakitandika kitanda cha wagonjwa Hospitali ya Amana mwishoni mwa wiki.
Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dr. Meshack Shimwela, (Kulia) akiwatembeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma , Bibi Hawa Mmanga (Kushoto), na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bibi Edna Mangesho, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana (Katikati), kujionea hali halisi ya matatizo ya Hospitali ya Ilala.PSPF, imekabidhi taasisi hiyo mashuka 300 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.
Hospitali ya Amana yahitaji msaada
Hospitali ya Amana iliyoko wilaya ya Ilala, inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba, licha ya kuwepo vyumba viwili vya upasuaji, zoezi la upasuaji hufanyika kwa kupokezana baadhi ya vifaa toka chumba kimoja, hadi kingine, kufuatia uhaba wa vifaa hivyo.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ilala, Dr. Meshack Shimwela, wakati akipokea msaada wa mashuka 300 na foronya zake, zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma, PSPF, kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.
Dr. Shimwela, ametolea mfano kuwepo kwa mashine moja tuu ya usingizi, ( Anaesthesia machine) wakati hospitali hiyo, inavyo vyumba viwili vya upasuaji, hali inayolazimisha upasuaji ufanyike kwa kuhamisha mashine toka chumba kimoja hadi kingine, wakati ilitakiwa kila chumba cha upasuaji kuwa na vifaa vyake vinavyojitosheleza.

Akizungumzia matatizo mengine makubwa ya hospitali hiyo ni uchakavu wa majengo kwenye wodi na huku hazina slingi bodi, hali inayoongeza mateso kwa wagojwa wao wakati wa jua kali, hivyo kuifanya hospitali hiyo kuongeza mizigo kwa wagojwa wakati hospitali panatakiwa kuwa mahali pa faraja.

Dr. Shimwela amesema hospitali hiyo ambayo huzalisha mpaka wajawazito 100 kwa siku, inacho kifaa kimoja tuu cha kutengeneza hewa ya Oksijeni kwa watoto wachanga wenye matatizo ya kuanza kupumua, hali ambayo inahatarisha usalama inapotokea wanapozaliwa watoto wenye matatizo hayo zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga, alisema Mfuko wake utajikita zaidi katika misaada ya kijamii kwa mahospitali ya umma, hivyo kilio cha Hospitali ya Ilala, kimesikika, japo hukutoa ahadi yoyote kuhusu kilio hicho, alisema kimepokelewa na atakifikisha kunakohusika.
Bibi Mmanga, huku akiwa ameandamana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bibi Ednana Magesho, , ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana, Ofisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Fatma Elhady na Godfrey Ngonyani, walijitolea kufanya kazi ya huduma kwa wagonjwa kutandikia shuka mpya kwenye baadhi ya vitanda.

Mfuko huo wa PSPF ulioanzishwa mwaka 1999, unaendelea na kampeni yake maalum kuzisaidia hospitali mbalimbali nchi nzima kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, mafanikio ya miaka 10 tangu kuwepo kwake. Kesho PSPF itatoa msaada hospitali ya Temeke na keshokutwa, Hospitali ya Ilala.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Majina 156 ya watendaji mafisadi kukabidhiwa Rais Kikwete

    Mkutano wa maombi ya shukrani kati ya viongozi wa dini wa Tanzania na Israel, umemalizika kwa kuazimia kumpa Rais Jakaya Kikwete, majina 156 ya watendaji mafisadi serikalini ambao wanashirikiana na mafisadi papa kudhoofisha uchumi wa nchi hivyo kuzuia jitihada zake za kuwaletea wananchi maisha bora.

    Katika taarifa iliyotolewa jana na Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentecoste, ilisema watendaji hao wametajwa kujikita katika vitendo vya ushirikina ili kulinda vyeo vyao serikalini na bungeni.

    Ilitaja baadhi ya mawaziri waliotajwa kuwa mzigo na kushindwa kabisa kwenda na ari mpya na kasi mpya ya kazi ni pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu wake, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Utawala Bora, Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Waziri wa Ardhi, Waziri wa Maliasili na Utalii, akiwemo kigogo mmoja wa Ikulu (majina yanahifadhiwa),.

    Taarifa hiyo iliongeza kuwa viongozi wa dini wamechoshwa kuwaombea viongozi kama hao ambao wanatumia wizara na ofisi za umma kama vijiwe vya kujilimbikizia mali, mambo ambayo utawala wa awamu ya tatu ulioongozwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, uliyakumbatia kwa kupora ardhi za wananchi mgodi wa Kiwira.

    Ilisema serikali ya Mkapa iliwaacha maelfu ya Watanzania wakihangaika bila ajira na ndiyo sababu viongozi wa dini wanamlinganisha Mkapa na baba aliyewaibia watoto wake mchuzi wa mboga.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika orodha ya viongozi wabadhirifu wamo wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wabunge na baadhi ya vigogo.

    Ilisema watu hao wamezigeuza taasisi za umma kama mali zao huku wakimpa kisogo Rais Kikwete kwa kutaka kuizamisha serikali yake katika matope.

    Aidha, taarifa hiyo ilisema viongozi hao wa dini, Sheikh Ramadhani Ali kutoka Kanda ya Magharibi na wageni kutoka Zambia, Askofu John Ngambi waliitaka serikali ya awamu ya nne kurudisha mashamba ya Kapunga yaliyoko Mbarali mkoani Mbeya kwa wakulima wa kawaida.

    Ilisema serikali isiendelee kumkumbatia mwekezaji ambaye ameshindwa kuliendeleza shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 5,500.

    Askofu Ngambi na Sheikh Ramadhani ambao ni wataalamu wa kilimo waliefundishwa kwenye vyuo vya Israel wamemwomba Rais Kikwete kuwagawia mashamba wananchi kwa usimamizi wa mtaalamu wa kilimo katika Wizara ya Kilimo, kazi ambayo itaajiri mamilioni ya Watanzania ambao kwa sasa wanashinda vijiweni kwa kukosa ardhi ambayo kimsingi iliporwa na utawala wa Mkapa.

    Taarifa hiyo ilisema mkutano huo pia ulimwombea maombi maalum, Rais Jakaya Kikwete na mke wake, Salma huku viongozi wa Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, John Mwakipesile, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Gama, Meya wa Jiji la Mbeya, Atanasi Kapunga wameshitakiwa kwa Rais Kikwete kwa kushindwa kuhudhuria maombi hayo licha ya kupewa mwaliko na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Pentecoste Evangelistic Church.

    Ilisema mkutano huo uliwakutanisha watu 4,000 wakiwemo maaskofu, wachungaji, mapadre, mashehe, wainjilisti na wazee wacha Mungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...