Sensei Alfred Malekia akiwaelekeza watoto nini cha kufanya. Sensei Malekia, ambaye ni kiongozi wa dojo (shule ya karake) ya Tanzania Goju Ryu Karate-Do inayotumia mtindo wa Jundo Kan-Kuroobi Kai (badala ya Jundo Kan Shibu) ya Okinawa, Japan, inaendeleza libeneke la sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu katika ukumbi wa shule ya msingi ya Zanaki kila siku jioni. Leo hii wanafunzi watano wametunukiwa mikanda myeusi shahada ya kwanza na wawili wametunukiwa mikanda ya kahawia katika sherehe fupi zilizofanyika hapo dojo usiku huu. Sensei Malekia amesisitiza umuhimu wa vijana na watoto kujiunga na mazoezi hayo ambayo humlea mwanafunzi kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika jamii.
watoto wakicheza kata ya kwanza ya Goju Ryu
Francis Kabika Sizya anaachana na mkanda wa kahawia na kuvalishwa mweusi baada ya kufuzu
Said Seleman Saleh akivishwa mkanda wa kahawia na kuachana na wa kijani baada ya kufuzu
Sensei Mbezi akimvisha Gaston Peter Minja mkanda wa kahawia
Sensei Rashidi Almasi akimtunuku Nicolaus Melkior Kalambo mkanda mweusi
Omary Emily Gregory akivalishwa mkanda mweusi
wahitimu ya mkanda mweuzi wakicheza kata
wahitimu wa mkanda mweuzi wakijifua na 'mae geri katika squatting position'
vingunge wa dojo la zanaki hivi sasa
wahitimu wa mikanda myeusi na kahawia wakipozi na viongozi wa dojo
wahitimu wa mikanda myeusi katika posi na viongozi wa dojo












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Safi sana

    hongereni wahitimu

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Sensei Edgar KalibotiJanuary 05, 2010

    Ni habari za kufurahisha nawapa kheri za mwaka mpya pamoja na hongera nyingi kwa masensei na masempai pamoja na wanafunzi wote hapo Zanaki Dojo! Endeleeni na moyo huo wa mazoezi na pia kuzeni dhamira ya ushirikiano na kuzidi kuendeleza sanaa aliyotuachia marehemu Sensei Bomani Hapo nchini!

    Sensei Edgar Kaliboti

    ReplyDelete
  3. Hongereni naona sasa wazee tumeamua kwenda na karate ili tujilinde

    Ole wenu majambazi

    ReplyDelete
  4. ImpokocheleJanuary 05, 2010

    Du nimefurahi sana, yaani ni suala la uwezo tu mngefungua matawi kila kona nchini.

    Huko Musoma kulikuwa na vijana wengi wazuri waliokuwa wakiendeleza ma-Dojo kwa technique hii ya Goju Ryu kama vile 'Sensei' Sele ku-mcha aliyehamia Dar na kuanzisha Wu-shu group na ngoma za utamaduni wetu na zaidi ya wote Mwalimu wa Walimu, bingwa mploe asiye na majigambo down to earth tallented individual 'Sensei' Abdallah Mkamba ambaye kwa kweli alistahili pengine kuwa na mkanda mweusi lakini Chuo chake hakikuendelea kutokana na ukosefu wa ushauri wa kitaalamu na fedha.

    Mola awajalie sana Selemani na Abdallah maana kwa kutufundisha sisi enzi hizo tuliweza kuwa watu wenye nidhami sana katika jamii na pia kutotishwa na ubabe wowote tukawa huru kutembea, kwenda shule, kwenda Naseems Villa bila uoga wa kuvamiwa, kupigwa wala kunyangánywa madaftari, mandazi wala wapenzi wetu bila kosa, mchezo mchavu uliokuwa umeenea.

    Hizi zilikuwa enzi za wababe mfano akina Juma Manero, Kakaa, Reny, Kenny n.k

    ReplyDelete
  5. napenda kujua shule hii ya dojo inapatikana wapi ili nimpeleke mtoto wangu, maana anapenda sana mchezo huu. Please help.

    ReplyDelete
  6. Ebwana mimi sina wa kumsifia mtu yoyote yule kwani michezo ni michezo kama mtakuwa wabunifu zaidi mnatakiwa kuanza kucheza muvi kwani za ukweli hiyo itawasaidia sana kiuchumi na kukuza uchumu wa nchi yetu tanzania,

    kwani miaka inazidi kwenda industry ya muvi za kitanzania bado inachemka kwani hata mastaa wao hawajui hata kuruka sarakasi kama jet lee na wengineo, na siyo lazima muwe kama jet lee, lakini mkifanya kwa muda mrefu mnaweza mkamfika hata kumzidi jet lee.

    kuna vijana kibao wapo wanauza vocha kitaani hawastaili kuwa pale,kama nyinyi wanajudo sijui nini mnaweza mkawapa mzuka nao wakajumuika na nyinyi, na kuanza hata kushindana kimuvi na mataifa mengine kama hollywoods. Mimi naomba taasisi kama hizo zijiwekee system itayokuwa inashirikia na shirikisho la sanaa tanzania, hata masponsor wajitokeze kuwasaidia vile ni hayo tuu nawatakieni kheri na fanaka ya mwaka mpya. Big ups mkazane na mjirekodi tuanze kununua movi zenu jamani na zisiwe na pumba nyingi..

    Huu ujumbe usichukuliwe ni kuwaponda watu flani wa maisha flani, ni maoni yangu tuu na nawataka watu tujikwamue kwenye huu umaskini tunaojiendekeza nao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...