Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete akiwa pamoja na viongozi wakuu wa umoja Pembeni kulia Yupo katibu wa umoja na Mh Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi Ali Shauri Haji.na kwa upande wa kushoto ni Mwenyekiti na Waziri wa fedha.
Baadhi ya viongozi katika picha ya pamoja wakiwa wanajiaandaa kwa kumpokea Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr Jakaya Mrisho Kikwete katika moja ya safari yake ya kikazi nchini Misri.
Wa mwanzo kutoka kulia ni Nd. Juma Abdulrahman(Mshauri)anayemfatia ni Katibu Mkuu na Mwenyekiti Nd. Majaliwa wapili kutoka kushoto ni mshika fedha Mwalimu Haji na Nd. Mukhtar Idd Mgodoka.
TANZANIA STUDENT UNION (TSU)
UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WASOMAO NCHINI MISRI.
Umoja huu wa Wanafunzi wa Tanzania nchini Misri ulianzishwa rasmi
tarehe 18-12-1964 na kupata usajili tarehe 30-10-1966 chini ya kifungu
cha sheria ya Misri nambari 32 cha Mwaka 1964, na nambari ya usajili ni 111, na Mpaka hivi sasa umoja una wanachama walio hai 76
ambao wapo katika mikoa miwili tofauti - Mkoa wa Alexandaria ambapo kuna tawi la umoja huu na kuna Wanachama 14 na Wanachama waliobaki wapo (62) Mkoa wa Cairo ambapo ndio makao makuu ya Umoja huu.

Wana umoja hao ni wanafunzi ambao wanasoma katika vitivo mbalimbali vya chuo kikuu cha Al-Azhar na Chuo kikuu cha Cairo University na vitivo hivyo ni:-
kitivo cha sheria za kimataifa,
kitivo cha sheria ya uislam,kitivo cha thiologia,
kitivo cha malezi na Ualimu,
kitivo cha Sayansi na Jamii,
kitivo cha teknologia ya Sayansi, habari na mawasiliano,
kitivo cha uandishi wa habari,
kitivo cha historia na ustaarabu,
kitivo cha biashara,
kitivo cha Lugha ya kiarabu na
Kitivo cha Lugha na Ukalimani.

MADHUMUNI YA UMOJA.
Kuleta umoja kati ya wanafunzi wote wa Tanzania nchini Misri.
Kumsaidia kila mwanachama mwenye matatizo kulingana na uwezo wa Umoja.
Kukuza uhusiano na vyama vingine vya wanafunzi nchini Misri na Dunia nzima.
KAMATI KUU YA TSU 2009-2010.
Umoja huu kwa mujibu wa muongozo wa katiba yetu huwa tunakuwa na uchaguzi kwa kila mwaka ajili kuweka uongozi mpya ambao utaendesha kurudumu katika kuletea maendeleo Umoja na Kwa Mwaka huu wa 2009-2010 Viongozi Majina yao ni kama ifuatayo:-
1.Majaliwa Mussa Shabaan Mwenyekiti.
2.Ghalib Nassor Monero Katibu Mkuu.
3.Dau Silima Ali Katibu Jamii.
4.Maulid Mpwani Naibu Katibu Jamii.
5.Swalehe Juma Mdungu Katibu Mwenezi.
6.Mashi Yussuf Mashi Katibu Michezo.
7.Juma Addrahman Mshauri.
8.Omar Juma Mangilile Mshauri
9.Mukhtari Idd Mgodoka Mshauri.

UHUSIANO WA UMOJA NA UBALOZI.
Umoja wetu unapata ushirikiano mzuri sana kutoka kwa Mlezi wa Umoja Mh. Balozi Alli Haji Shauri na Maofisa wote ubalozini kwa ujumla katika kutatua baadhi ya matatizo yanayotukumba au kukabiliana nayo katika Safari yetu hii ya Utafutaji wa Nondozazz.
Tunashukuru sana kwa ushirikiano wao.
Kwa Maelezo Zaidi Wasiliana na:-
Katibu Mkuu.
+20109152841
KWA NIABA YA UMOJA
KATIBU MKUU,
GHALIB NASSOR MONERO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...