Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kwani uwanja huu ni wa majani feki ya rubber kuchanganya na plastic? kama ni yes sioni ubaya wowote kwa nini wasitumie uwanja huu,mbona hapa ,manake jiji letu nalo viwanja vingi vinatakiwa kumwagilia maji kila usiku na uhaba wa maji bongo sijui watawezaje haya na ufukara wa vilabu vyetu mhh sioni matunzo mazuri ya viwanja vya vilabu.manake hata hapa Australia kuna vilabu vingi sana tangu junior mpaka senior utakuta tunapokezana viwanja vyenye nyasi za bandia manake maeneo mengi ya Australia wakati wa summer ni digirii mpaka 40 so majani yote yanakuwa yanjano,kwa hiyo viwanja vya majani feki ni bora sababu wachezaji wasije wakaumia wakati wakifanya mazoezi,kiwanja kikiwa na vipara majani hapa au hapo.uwanja wa taifa ubaki kulindwa na usiguswe kufanyia mazoezi maanake ni uwanja wa kitaifa ambao ucheza mechi za kigeni na sie wanyumbani.
    wacha wanasoka wetu wafanye mazoezi kwenye kiwanja cha maana hapo kwa bibi.kama unataka kulalamika walalamikie viongozi wa vilabu na sio taifa au uongozi wa nchi,hayo sio aibu au vichekesho wala nini ni hali halisi ya nchi yetu ,kama unataka kubadilisha hayo basi wachezaji watoe fees za juu ili vilabu viweze kuweka nyasi bandia kweye vilabu vyao.uwanja huu ni wakila mtanzania na wanahaki ya kufanya mazoezi hapo.

    ReplyDelete
  2. Kwanza nakushukuru sana Anko kwa kuileta mada hii. Kwa kweli wengi inatuuma kuona timu zetu, hata kubwa zinakosa viwanja vya kufanyia mazoezi.
    Lakini mimi binafsi, napenda kuwasukumia lawama watu wote wanaohusika na usimamizi wa ardhi na mipango miji (Land Management and Planning).
    Kuna dalili za wazi kabisa kwamba Tanzania hatuna mamlaka wala taasisi za sekta hiyo. Tukumbuke zamani kidogo, mpaka hata miaka ya 1980, Dar es Salaam hiyo ilikuwa bado na viwanja kibao, ama vya kucheza watoto ama hata vya klabu mbalimbali za watu wazima. Nakumbuka kwa mfano hapo Temeke, maeneo ya karibu na Uwanja wa Taifa kulikuwa na viwanja lukuki na timu kama One Time Fun Club, Temeke Boys, Good Hope FC, African Temeke, Sifa Politan, Opec International, Villas Equador, n.k., lakini leo ukizunguka utakuta vyote vimefanywa gereji za kutengeneza magari. Hivi viwanja na timu zao vilisaidia kutoa wachezaji wenye vipaji kama vile kina Selemani Mkati, Edward Chumila, George Lukas, Peter Nkwera, Salvator Edward n.k.
    Watu wamevamia mpaka vile viwanja vya Jangwani na kuweka parking za magari, sijui siku hizi Villa Squad wanafanya wapi mazoezi!
    Hii inaonyesha ni jinsi gani tusivyoheshimu utaratibu.
    Lazima tuwe na utaratibu wa kujitengea maeneo ya michezo na kujiepusha na tamaa binafsi za kuuza maeneo kwa wafanyabiashara wasiojali maendeleo ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  3. Kwanza shukran Ankal kwa kutuonyesha hii aibu ya mwaka. Kweli inasikitisha kuona Vilabu vyote vya Tanzania havina uwanja. Hata hivyo vilabu vinavyojiita vikubwa vinakosa hata viwanja! Hii kweli hii inatia uchungu sana!! Tatizo mimi naliona ni UTOVU, UBUNIFU na BASI BASI tu kama ulivyosema. Nimesema ubunifu kwa kuwa Viongozi wa Vyama vya Soka na Vilabu hawana upeo mkubwa wa kuona kama hilo ni tatizo kubwa. Utanunuaje Kabati wakati huna hata nguo yani Club sasa zina uwezo wa kumleta kocha toka nje, na kusheheneza wachezaji , so called "Wakulipwa" na kutoa mishahara minene bila kuwa na uwanja wa mazoezi?? Hivi hii ni akili au madudu!! How much kiwanja cha mazoezi kina cost?? Ni ujinga wa viongozi tu kutojua ni nini wanafanya. Pili kama pendekezo: Kwanini wasitumie hao wadhamini kuwajengea viwanja ikiwa kama part ya Mikataba yao. Hivi ndivyo yafanyikavyo uku kwa wenzetu. Mabenki, Makampuni makubwa kama KIlimanjaro Beer wanatakiwa kujenga viwanja au kukurabati viwanja na kuvipa majina yao ya kibiashara kama Vodacom Stadium Soth Africa, Emirates UK, etc. Wanakaa wanawadanganya Watanzania kila siku kwa kugawa mipira na Jersey ambayo haina mahala pa kuchezea unadhani tutafika? Jamani jibu la kutondelea soka la Watanzania tunalo, kuwa hatuna plan, hakuna viwanja vizuri vya Mazoezi. Kama hao wanaojiita wadhamini kwa nini wasidhamni ujenzi wa miundo mbinu kwanza?? Pili ni hali ya kutojali inayotuathili Watanzania. Mtanzania wa leo hajali kama mtanzania wa miaka arobaini ijayo ataishi vipi? Tukianzia katika Viwanja, Barabara na Mitaro. Leo uwanja mpya wa Taifa hauna hata miaka miwili lakini tayari ukoka umeshaanza kukauka na vipara vinaanza kuota!! Kiwanja hakimwagiwi maji hadi Drogba na wenzake watishie kutocheza?? Huu ni upuuzi mtupu, si nasikia mlipelekwa Beijing kusomea matunzo ya Uwanja?? Sasa huko Beijing waliwaambia kuwa msiumwagie uwanja maji mpaka aje Mwanasoka Bora duniani. Huu ni Upuuzi hatuwezi kufikiri kuwa kama hatutatunza hizi mali leo wajukuu wetu watakosa pakujivunia? Na watajiuliza hivi wazee walikuwa wanafanya nini?? MWISHO Serikali inatakiwa isitishe zoezi hili mara moja na kuagiza vilabu kuwa na viwanja vya mazoezi la sivyo timu hazitaruhusiwa kushiriki tuone kama havitapata wadhamini wa kujenga viwanja. Timu zina mabasi ya gharama halafu havina viwanja?? PIA TFF inabidi ipitie upya mikataba na NBM, Vodacom na Kilimanjaro Beer kwani jamaa wananufaika sana kuliko wanachokidhamni. Wajenge viwanja mbona South Africa wanajenga?? Ah hii inasikitisha sana!!

    ReplyDelete
  4. Wakulaumiwa MKAPA Viwanja vya shule ya Uhuru,kajenga shule.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...