Marehemu Swetu Fundikira ambaye alifariki jana asubuhi kwa kinachosadikiwa majeraha makubwa yaliyotokana na kipigo Ijumaa usiku jijini Dar
Juu na chini ni baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa baba wa marehemu,
kinondoni karibu na mahakama ya kinondoni


Habari ambazo tumezipata sasa hivi kuhusu msiba wa marehemu, Swetu Fundikira zinasema kuwa mazishi yake yatafanyika kesho katika makaburi ya Mwananyamala jijini Dar saa tisa alasiri.

Hii ni baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa hospitali ya Taifa, Muhimbili kwa kuwashirikisha ndugu wa marehemu pamoja na maofisa wa jeshi la Polisi ili kujua chanjo cha kifo chake, kwa mujibu kaka wa marehemu Ismail Fundikira.

Aidha Ismaili amewashukuru wadau wote waliojitokeza tangu mwanzo wa msiba mpaka sasa pamoja na wadau wa klabu ya michezo ya Mango Garden ambayo Marehemu alikuwa nahodha wa timu hiyo kwa kutoa mchango wa hali na mali katika msiba huo.

"Napenda unifikishie salamu zangu za dhati kwa wale wote waliofika kutufariji tangu mwanzo wa msiba.Waandishi wa habari nao wamekuwa wakifika hapa nyumbani na wamekuwa wakitusaidia katika kutoa taarifa za msiba wa mpendwa wetu", alisema Ismail ambaye ni afisa mwandamizi Swissport.

Marehemu ameacha watoto wawili ambao ni Misuka na Syalo ambao wako Ulaya wakisoma katika vyuo vikuu vya huko.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, Jeshi hilo linawashikilia askari wawili wa Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), Sajenti Rhoda Robert na Koplo Ali Ngumbe wakazi wa Lugalo kwa tuhuma za kmpiga na kumsababisha kifo marehemu Swetu Fundikira.
Hata hivyo kumekuweopo na minong'ono ya kuhoji ni kwa nini watuhumiwa wabaki wawili na sio wanne kama walivyokutwa na askari wa kituo kidogo cha Salender baada ya kutonywa na dereva wa teksi siku ya tukio.
Vile vile rafiki wa marehemu Swetu waliyekuwa naye, na ambaye alikimbia kwenda kuomba msaada baada ya kuzidiwa nguvu na watu wanne, amesema idadi ya washambuliaji wao ilikuwa watu wanne, akiwemo mwanamke mmoja.
Tunaendelea kufuatilia kitendawili hiki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Eti wanachunguza chanzo.Mtu kapigwa hadi kufa halafu unakuja kusema wanachunguza chanzo.Hii ni First Degree Murder Case. 2000 consecutive life sentence in prison iwe fundisho kwa wajinga wengine wanaotumia Uniform za JWTZ kuonea raia.

    ReplyDelete
  2. POLENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA FAMILIA YA FUNDIKIRA.Kaka Michuzi kweli hicho kitendawili!! ila hapo kwakweli hao askari wachukuliwe sheria ili iwe fundisho kwa wengine manake wamezidi na sidhani kama ni mara ya kwanza kutokea kwa tukio kama hilo(hao askari kuwapiga wananchi),aya leo wamesababisha kifo kweli tunaenda wapi sasa jamani?!!?
    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.AMIN
    Rabia

    ReplyDelete
  3. R.I.P bro,its going way too much now hawa wanajeshi wamekuwa waonezi sana kwa raia.wapewe adhabu kali kama mfano

    ReplyDelete
  4. Inalilah waina ilahi rajiun poleni wafiwa Mwenyezimungu aiweke mwili wa marehemu mahala pema peponi.

    Feisal nakuona hapo. mdau UK.

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa. Nilikuwa nasoma hii story na inasema kuwa swetu fundikira alichomekewa kwenye foleni na yeye akatoka kwenye gari na kufuata gari iliyomchomekea hapo ndio ugomvi ulipoanza. Ni mapenzi ya Mungu lakini Jamani tuepukana na hasira za ghafla. Yaani kuchomekewa tu imechukuwa uhai wa mtu.

    ReplyDelete
  6. HAWA WANAJESHI NI WAONEVU SANA TENA SAANA, YAANI WAO NDIO WAMCHOMEKEE MTU HALAFU WAMPIGE DUH EBANAEEE!! UONEVU WA HALI YA JUU HUU.
    SIO SIRI MM NAWACHUKIA SANA HAWA WANAJESHI KWA MISIFA YAO KUNA MJESHI MMOJA KAZI YAKE AKIKUONA NA SURUALI NZURI KM KADET KAIMAIND AU MKANDA MZURI YAANI HATA KM RANGI SIO ILE YA JESHI HASWA
    INAFANAFAA KIDOGO TU LAZIMA ATAKUVUA NA KIPIGO THEN ANAONEKA KAVAA YEYE.

    KUNA SIKU WANAJESHI WALIIBIWA NYUMBANI KWAO KISASII CHAO HAKIKUWEZEKANA.
    MIM NAWACHUKIA WEZI LAKINI HIYO SIKU WANAJESHI NILIWACHUKIA ZAIDI JAPOKUWA WALIIBIWA KUTOKANA NA WALICHOKIFANYA.

    ILIKUWA IKIFIKA SAA MBILI USIKU WANATANDA KTK BARABARA YA HUO MTAA WALIOKUWA WAKIKAA ANAEPITA ANAULIZWA UNAENDA WAPI NA KWANINI UNAPITA MTAA HUU THEN WANAWACHUKUA HADI NDANI KWAO WANAAZA KUWACHAPA NA WAYA NA NAKUWAPIGA NDULA ZA MAGOTI

    DAH!! ILINIUMA SANA WATU WASIOKUWA NA HATIA WALIWACHAPA
    KISA WAMEIBIWA WAO NA WAO NI WABABE, TUNASIKIA MAKELELE TU DANI MTU ANALIA. WAKIMALIZA HUYO WANAMTOA THEN WANAKAA TENA BAABARANI UKIPITA TU KOSA LABDA UWE MTU MZIMA ARROUND 50 NDIO WANAKUACHIA LKN KIJANA UKIPITA TU NOMA WANAKUKAMATA NA KUKUINGIZA NADANI KWAO UNAPATA KICHAPO

    HAWA WAONEVUUUUUU
    MIMI NATAWA WANYONGWE AU WAHUKUMIWE MIAKA MIA NANE(800)

    ReplyDelete
  7. TATIZO NI HAYO MAGWANDA YAO WAKIVAMIAA MITAA WATU WANKUWA NA KIJIUOGA KIDOGO LKN KAMA INGEKUWA WANAWALETEA WATU WAKIWA NA NGUO ZA KIRAIA. LAZIMA MPAMBANO UNGEKUWA WA KUTA NIKUVUTE TUNGECHAPANA NAO SANA.

    KAMA MNABISHA SIKU MOJA FANYENI SOO HALAFU MJE KWA RAIA KUWATEA ZA KULETA MTAONA CHA MTEMAKUNI-

    ILA MSIIVAE MAGANDWA YENU NA MSIWE NA BUNDUKI MJE MNAVYOJUA NYINYI BUT NO GUNS WALA UNIFORM ZENU.......NNAHAKIKA PATAV´CHIMBIKA NA MTATOKA BARUTI.

    ReplyDelete
  8. RIP. Lakini mbona huyu anaonekana ni kijana kapataje watoto wanaosoma chuo kikuu sasa ama ulivyoandika kwenye article?

    ReplyDelete
  9. Kwa kumsaidia mdau anon wa jan26 12.05am aliyeuliza marehemu alikuwa kijana na kapataje watoto wanaosoma chuo kikuu?. nadhani mdau unataka umbea na kujua zaidi undani wa marehemu ambao hautokusaidia kitu, na mwisho utataka kujua kazaa na nani?. anyway kwa kukusaidia na kutoa umbea wako ni kuwa ninavyomfahamu Marehemu amefariki akiwa na umri kati ya miaka 45-47 je hawezi kuwa na watoto walio chuo kikuu ukitizama kuwa watoto wake wamekulia ulaya. (ulaya mtoto wa miaka 19-21 wapo chuo kikuu) sio bongo utakuta mtoto mpaka wa miaka 19 yupo darasa la saba .pili marehemu alikuwa mtu wa kujipenda mcheza mpira toka utotoni kwake , kila siku ni mtu wa mazoezi na lishe nzuri. next time toa rambi rambi usitake kujua ya ndani .
    mdau UK

    ReplyDelete
  10. KWA KWELI HABARI HII NZITO NA YA KUHUZUNISHA SANA KWA WATANZANIA WOTE, HOSUSANI WAKAAZI WA KINONDONI AMBAPO NI MAKAZI YA MAREHEMU NA FAMILIA YAKE. NA PIA NI MATUMAINI YANGU KWAMBA VYOMBO VINAVYOHUSIKA VITACHUKUA HATUA ZINAZOSTAHILI ILI KUHAKIKISHA KWAMBA TABIA HII MBAYA YA BAADHI YA WANAJESHI HAIRUDIWI TENA.
    KINACHONISHANGAZA NI KWAMBA, KWA NINI BAADHI YA WANAJESHI WA SIKU HIZI WAMEJENGA HISIA KWAMBA WAO WAPO JUU YA SHERIA? WHERE DO THEY GET THIS NONSENSE IDEA? MBONA HII TABIA HAIKUWAHI KUONYESHWA NA WANAJESHI WAAZAMANI, TENA AMBAO WENGI WALIPIGANA VITA VYA UGANDA, NA VITA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA? NA AMBAO TUNGEWEZA KUSEMA KWAMBA LABDA WALIKUWA WANASUMBULIWA NA POST TRAUMATIC DISORDER, AMBAYO NI TATIZO KUBWA MIONGONI MWA WANAJESHI WANAOTOKA VITANI.
    WANAJESHI WENGI WA SASA HIVI NI EIDHA WAMEMALIZA FORM-SIX, COLLEGE, AU UNIVERSITY (KAMA SIKOSEI), HIVYO NI WASOMI. KWA MSINGI HUO, WALITAKIWE WAWE NA NIDHAMU YA HALI YA JUU, KWA SABABU YA UFAHAMU WAO WA SHERIA ZA NCHI, NA HASWA HAKI ZA RAIA KWA MUJIBU WA KATIBA YA YETU, LAKINI KILA SIKU UTASIKIA WAMESHAMBULIA RAIA BILA SABABU YOYOTE. MIMI NADHANI JESHI LETU LINA WALAKINI INAPOKUJA KWENYE RECRUITMENT YA HAWA ASKARI WETU, HASWA SUALA LA NIDHAMU. NINA MASHAKA NIDHAMU HAITILIWI MAANANI IPASAVYO, NDIO MAANA WAPUUZI WACHAHCE WASIOSTAHILI KUWA JESHINI, WANALIPAKA JESHI ZIMA MATOPE.
    KWA WAFIWA (FAMILIA YA FUNDIKIRA) POLE SANA KWA MSIBA, MUNGU ATAWAPUNGUZIA MAJONZI. LAKINI HAKIKISHENI HAKI INATENDEKA ILI MSIBA KAMA HUU USIIKUTE FAMILIA NYINGINE YOYOTE HAPO NYUMBANI. MY ADVICE TO YOU; PLEASE GET THE BEST DEFENCE LAWYEAR YOU CAN AFFORD, BECAUSE THE REAL BATTLE LIES AHEAD OF YOU IN FIGHTING FOR YOU BROTHER AND WALALA HOI’S JUSTICE.


    KARUMANZIRA.

    ReplyDelete
  11. NO mdau jan tue 12.05am alitaka kujua maana kaona kwenye picha kuwa anasura ya ujana!ok marehemu alikuwa na sura ya ujana ila ni mtu mzima ok!na mdau tue 12.48am watoto wa marehemu hawakulia ulaya,ulaya wameenda watu wazima ok!mdogo mtu alitangulia akafata dada mtu!ok mungu akulaze mahali pema peponi swetu!inshallah mungu atakulia mungu hakika!RIP swetu fundikila!

    ReplyDelete
  12. Poleni sana familia ya Marehemu. Mwenyenzi Mungu atawapa faraja.

    Nitoke nje ya mada kidogo, napenda sana majina ya familia hii Swetu, Syalo, Misuka.....ni ya kitamaduni, mazuri sana.

    Turudi kwenye mada......Nataraji sheria itachukua mkondo wake, watuhumiwa wachukuliwe hatua ili familia nyingine zaidi isipate majonzi haya. Hakuna kitu chochote kinacholingana na thamani ya maisha ya mwanadamu. Binadamu sisi tukoje?

    ReplyDelete
  13. Yaani anon wa Tue 26/1 Wewe ni kiboko na nimekuvulia kofia pia nakupa bonge la BIG UP - kiboko ya wakuda.

    ReplyDelete
  14. Wanafamilia poleni sana kwa msiba mzito na wa ghafla. Mungu ailaze Roho ya marehemu pema peponi Amen.
    Kwakweli naona kama wanajeshi hawana kazi za kutosha siku hizi, tuna amani hakuna vita hivyo wanatafuta pa kumalizia nguvu zao. Nadhani wapelekwe kwenye mapori katika mipaka ya nchi yetu kunakosumbuliwa na Majambazi wakapambane huko wasifanye vurugu hapa mjini.

    ReplyDelete
  15. naipa pole famillia ya marehemu ,jamani nimeshtuka sana kusikia hii habari ya msiba ,na wafahamu watoto wa marehemu nilisoma na sylo shule ya mbezi beach ,jamani baba yao alikuwa anawapenda ile mbaya ,nikweli walilelewa kizungu mpaka raha ,jamani duniani tuna pita ,namwomba mungu awafariji sana kipindi iki kigumu ,tulimpenda sana ,baba yetu ila mwenyezi mungu alimpenda zaidi ,pole sylo na misuka ,tuko pamoja kumwombea baba akapumzike salama

    ReplyDelete
  16. hao wanajesh wengi wao ni majambazi kwani ndo hao hao huuwa na ukiangalia hata mashambulizi yao huya hayana huruma hata kidogo. mungu mkubwa atalipa kadiri ya matendo yako, hata ikipita miaka kenda utapata cha akupata tu kama si wewe uliye uwa basi laana huenda kwa watoto na wajukuu zako.

    polen wafiwa, POLE MDOGO WANGU TELUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  17. Wanajeshi na polisi wanajengewa kiburi wanajiona wapo juu ya sheria, mfano hili la wao kutokulipa NAULI wkati wanapata mishahara kama walimu, manesi nk ni jambo linalowafanya wajione wapo juu ya sheria.

    ReplyDelete
  18. sasa wewe anon wa hapo juu 12:43iliyedai nataka umbeya mimi si bora mimi sielewi nauliza kama hii haijakosewa ilivyoandikwa nisije kurudioa uongo nikihadithi badili ya kuongea uongo kama wewe kuwa watoto walikulia ulaya wakati hawajakulia ulaya. waswahili bwana ndo hivyo hadithi itabadilisha watoto walikulia ulaya, kisha itaenda kua walikuliaje ulaya labda baba yao raia wa huko uliza mpaka ikimfikia mtu wa kumi vitu ishirini vya uongo vimeingia kitu kama hujui uliza kama mimi sio kutunga tu kuonekana unaju. Aliyejibu chini yake mdadau wa 1:03 nakushukuru kwa kunielewesha vizuri kuwa ni ana dongo nzuri tu marehamu.inshallah mungu atamrehemu na kuwapa wanawe na familia yake kwa ujumla faraja na nguvu za kuweza kuendelea ma pengo marehemu alilowaachi.

    ReplyDelete
  19. to be honest hata mimi nilimpa sweetu 32 or 33 years and was wondering how he manage to have 19 or 20 year old kids. ningeenda kulopoka sasa huko kuwa kazaa at 13 hivi bure bora tumeeleweshwa michuzi sasa na wewe vitu kama hivi unatoa historia kazaliwa lini etc

    ReplyDelete
  20. Nwapa pole ndugu ...jamaa na marafiki kwa kifo hiki cha kusababishwa na hawa wananchi inauma sana....mimi nilisoma na mtoto wa marehemu Syallo ktk shule ya mbezi beach.,,tulikuwa marafiki wa karibu hat na familia yake baba yao alionyesha upendo wa hali ya juu kwa watoto wake hata sisi marafiki wa watoto wake...hata mtoto wake alipoenda kusoma ...Mama syallo...Mitsuka,syallo.,Mwiza,na FFundikra family wote,Mungu awape roho ya ujasiri katika kipindi hiki kigumu na uvumilivu tupo pamoja daima.OMG R.I.P

    ReplyDelete
  21. Kukamatwa na wawili badala ya wanne ni strategy maalum hiyo kwani kwa Zombe ilifanya kazi. Nyie ngojeni kesi ikianza tutaambiwa kuwa walioua siyo hawa, wauaji halisi wamekimbia na polisi bado inawatafuta, hivyo itakuwa mambo yaleyaleeee! kuwa uchunguzi haujakamilika kwani polisi bado inawatafuta watuhumiwa wengine. Itaendaaaa, mpaka tukisahau baada ya miaka mitatu hivi kutokana na tukio jipya basi ndiyo kusema damu ya Swetu mchangani imeoshwa na mvua!.

    Tunataka kesi hii isichukue zaidi ya mwezi kila kitu kipo, kwa hawa nao kutoa taarifa polisi kuwa marehemu aliwafanyia fujo ni ushahidi tosha. Wahukumiwe kifo haraka kama vile walivyofanyiwa wauaji wa albino ili iwe fundisho kwa mwananchi yeyote yule kujichukulia sheria mikononi, awe mjeshi, baunsa, polisi mvuta bangi, mla unga etc.

    ReplyDelete
  22. Tuone hawa nao kama watakua wameua bila kukusudia. Poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  23. Kwa kweli kifo cha swetu fundikira kimeniuzunisha sana sana, kweli imeniuma sana sana, nimekaa kinondoni mtaa wa kanazi, kuna mpangaji mwenzangu anaitwa mama halima, mke wa marehemu alikuwa anapenda kuja hapo na watoto wake, jamani nawafikiria hao watoto jamani kukosa baba kwa ujinga wa hao wanajeshi jamani, mimi kama amri yangu na wauwawe jamani, wauwawe na tusiwaone kabisa, kupiga gani huko kama wametumwa jamani eeeh, sielewi na hatutaki kusikia serikali inawaachia huru, tutawauwa hao, yaaani wakae wakijua, washenzi sana, kuchomekewa ndio umtoe mtu roho, je ndivyo mafunzo ya jeshi yapo hivyo ata kama wamejibiwa vibaya walitakiwa wasichukue sheria mkononi, ata huyo mwanamke mmmh kama ana mume nampa pole sana, mwanamke gani una roho ya kikatiko namna hiyo jamani, kama hajazaaa jamani, jamani mmmmmh sielewi, mungu amlaze mahali pema peponi marehemu swetu fundikira, wanao na mkeo mungu ndie atakae waongoza katika maisha yao na hawatakwama sehemu yoyote na watakuwa na maisha mazuri kwa nguvu za mungu, na hao wauaji wataungua na moto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...