Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala (Mwenye suti) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni nane kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mbagala Dar es Salaam Mwl. Marcelina Kimario ikiwa ni michango ya wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo hicho kwa shule hiyo ili zisaidie kukarabati sehemu ya madarasa iliyoharibika kufuatia ajali ya milipuko ya mabomu iliyotokea mwezi Februari mwaka jana.
Makabidhiano hayo yamefanyika shuleni hapo mbele ya viongozi akiwamo diwani Mh. Jerome Bwanausi wa kata ya Mbagala Kuu, waalimu na wanafunzi wa shule hiyo. Wengine waliofuatana na Prof. Mukandala ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii Prof. Amandina Lihamba (wa Kwanza kushoto), Mkuu wa Shule ya Elimu Prof. E. Bhalalusesa(wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Bw. Edward Jambo (hayuko pichani).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...