Katibu wa jumuiya wa Tanzania (mmatumbi pekee) akishiriki katika mada mbali mbali za wageni Ugirki. Sheria ambayo inatarajiwa kupitishwa bungeni tar 7 Jan.10 kuhalalisha kupatiwa uraia kwa mtu yoyote alokaa miaka mitano kihalali pamoja na watoto wao waliozaliwa Ugiriki au kama mtoto amekua anasoma shule Ugiriki kabla hajatimia miaka 18 at least awe amehudhuria miaka mitatu nyuma,kwa kusema awe ameanza kusoma tokea akiwa na umri wa miaka 15. banda letu maoneshoni athens

maandamano ya wageni kulilia sheria mpya ya uhamiaji

Mheshimiwa Ankal,
naomba tuwekee hili wazi. Kwa mara ya kwanza na katika historia wakaazi waliokaa ugiriki kwa atleast miaka mitano tu kisheria pamoja na watoto wao basi watakula nondo(Passport)za kigiriki.Ikiwa mzazi wa mtoto atakua anaishi kisheria kwa miaka mitatu basi akitimiza miaka mitano tu yeye na mtoto wake wanakula nondo kama kawa.

Sheria isharekebishwa na inapitishwa bungeni Tar 7 Jan.10 kwa kupigiwa kura,WADAU TUNAOMBA DUA ZENU,TUMEDATAA NA POPOTE ULIPO K AMA ULIKAA UGIRIKI RUDI HARAKA UWAHI KULA NONDO LAKO.
Habari zaidi pitia www.tanzaniansingreece.com KATIKA SITE YETU USOME
Mdau Nuramo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Sitaukana Ubongo-Ubongo wangu hata kama utanipa karatasi la kuishi ulaya au america.. Bongo tuko vyema. Hii post ni kwa wale walio-fulia maisha wakimbilia nje. Michu, badili kichwa cha habari plizi

    ReplyDelete
  2. juma m`bongoJanuary 06, 2010

    MNALILIA NONDO ZA UGIRIKI ZA NINI? MUNGU KESHAWAJALIA NONDO ZA BONGO JAMANI WABEBA BOX ACHENI UTUMWA JAMANI, WAKOLONI WAMETUPA UHURU WAKAONDOKA LAKINI SASA MNAWAFUATA HUKO HUKO KWAO NA KUOMBA NONDO KINGUVU ILI MUENDELEE KUWA WATUMWA WAO? ETI UNAWAITA WENZIO WARUDI KWA KWELI MNATUTIA AIBU SANA.

    ReplyDelete
  3. Passiport zetu za kibongo kwani vip?. Mpaka uzifagirie za huko na kuzielezea kula nondo.

    ReplyDelete
  4. tuambie kwanza uchumi hapo ukoje. maana mi nafikiri hiyo nchi alosto kinoma. huwa ninadhani siyo sehemu ya mtu kwenda kuishi kama waendavyo state, uk, canada nk

    ReplyDelete
  5. KUNA DEAL KWA WATU TULIOKO NJE YA GREECE(OTHER PART EUROPE).
    REPLY:kibaha1970@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  6. jamani hivi kwa kiswahili cha mitaani mmatumbi ni nani?

    ReplyDelete
  7. miaka mitano tu? mna bahati wenzetu!! sehemu nyengine za europe kama hujatimiza miaka kumi ya kuishi kihalali wala usifikirie kuomba mkoba wao, unless uwe umeoa au umeolewa na mwananchi. na hiyo pia siku hizi sio rahisi hasa uk

    ReplyDelete
  8. hii kali, yaani kuomba mora uukane uzalendo??? na kuukaribishi ugiriki?

    Sina baya na mtu ni maoni yangu tu.

    Hivi ati kila nikiangalia mabanda mengi ya TZ yaliyoko nje ya nchi mbona mengi huonyesha mavazi ya kimasai, vinyago na urembo urembo ? kwa nini???

    mbona kabila zingine haziwakilishwi, akina jomba chilingi chumuni, nsamaki nchanga???

    siku za sikukuu kama kuwakaribisha wageni wa nje

    siku nyingine inabidi munabadalisha hata kama katika hafla inabidi kupika makande sio kila siku pilau na nyama choma

    ni hayo tu

    Ni mimi

    mjombaake binamu yake jirani yake mdogo wake wa mwisho wa shangazi yake mkubwa anayekaa Tukuyu.

    ReplyDelete
  9. No to Xenophobia - ndivyo vinasema vikaratasi wanavyoonesha mama na mwanae. Hongereni wakongwe wa Perea - niliwahi kukaa mitaa ya Alisia Efksendiu - tukivinjali Omonia na mashati hata wakati wa winter kabla global warming haijavuruga mambo. Hebu nishauri nitakujaje, nitafikaje, nitaingiaje kudai hiyo nondo yangu?

    ReplyDelete
  10. Mcheza kwao hutunzwa!!!
    Yeh,it sounds a very good deal indeed!! But guys, lets not forget, your country needs you. As shit as it may be, it takes you and me to make it a better place.
    The point is these people will give all sorts of attractive offers to remain the man power in their countries (basically to do the 'dos' the white dudes won`t do! in short modern slavery)
    You can become greek alright, or any other citizenship you mention but you will be suprised the way they won`t give u as much attention as your newly adopted passport deserve.
    Fellows, This is the globalisation ERA!! In this era, country`s boundries do not matter anymore, the globe is made to be one big country, in not so long, your passport or skin colour won`t matter any more! What will matter is what will you bring to this newly conceived country???
    My country men, SLAVERY IS STILL VERY ALIVE, the only difference is, THIS ONE IS VOLUNTARY!!

    ReplyDelete
  11. Greece nako kumbe kuna dili?

    ReplyDelete
  12. ugiriki? please!

    ReplyDelete
  13. Sijui iweje ni ukane uraia wa nchi yangu nikaishi huko nje kwa kubaguliwa baguliwa tu. Hainiingii akilini kabisaaa.. Kweli tunamitizamo tofauti.

    Hadi kuandamana na kudai kwa nguvu?!

    ReplyDelete
  14. kwani si kuna DUAL CITIZENSHIP, SIRIKALI YETU INASHINDWA NINI KUTAMBUA UMUHIMU WA HILO..KWA HIYO CHA KUWALALAMIKIA NI SERIKALI NA SI HAWA WATU WALIOKO NJE,

    WANATAFUTA MPUNGA, KAMA WEWE ULIYE NDANI, JE KAMA WAKIRUHUSIWA KUWA NA PASSPORT MBILI, HUO MPUNGA SI UTAKUAINVESTED BACK HOME, I MEAN TANZANIA, NA KILA MTU ANAPIGA BAO.

    TUSILALAMIKE KUWA HAWA WATU WAMEPOTEZA UZALENDO, BALI WANAUJALI UZALENDO NA WANA A LOT TO CONTRIBUTE BACK HOME, OUR NEIGHBOURING COUNTRIES REALIZE THAT, KWANINI SISI TUSIFATE HIVYO.

    SIKU ITAKAPOTEKEA HIGH PROFILE INDIVIDUAL IE SPORTSMAN, EG FOOTBALLER, NDIO MAY BE TUTABADILISHA IMAGINE DROGBA WA TANZANIA ACHEZEA UK, HALAFU ANASHINDWA HATA KUINVEST KWAO SABABU HANA PASSPORT.

    shauri yenu Tanzania, mwanangu anatalent ya football, fanyeni mmpe gamba aje achezee huko,kabla hamjamsikia kwenye news, na wengine wengi kwenye fani za usomi, nk, wapo wengi tu, na hii yote generation tusubiri in 15-20years, the government will realise what they are missing, anyway hao government watoto wao wote wako nje wanasoma na kutafuta maisha, ndio maana hawajali ya wote, wanavutia kwao tu.

    ReplyDelete
  15. Mimi nadhani nyumbani ni popote pale duniani, ambapo mtu anapoweza kumudu maisha yake, kuishi kwa kufuata sheria za pahala husika, na kuwa na uwezo (kama nilivyoandika hapa juu) kumudu maisha yake mwenyewe na kusaidia nyumbani kama ilivyo kawaida yetu.

    Hapa suala la "Uzalendo" wala halina uhusiano. Kama unaishi nyumbani, kipato chako cha chini au hata kama ni cha juu, wakati huo-huo unalazimika kupokea RUSHWA, KUIBIA MWAJIRI, KUSAINI MIKATABA YA HOVYO ili mradi una 10 percent yako, kununua bidhaa hafifu kwa bei ya juu kwa kutumia pesa za wavuja jasho, walipa kodi, ili tu kupata HONGO yako na baadae ujigambe kwa kujenga majumba ya kifahari, kununua magari ya bei ambayo haifanani kabisa na kipato chako. HAPA NANI MZALENDO? (Hapa sina maana kwamba kila anaeishi hapa nyumbani anapokea rushwa, kwa sababu hata mimi sipokei, aidha sina maana kuwa kila anaesaini mkataba anasaini mkataba mbovu, ila wale wacheche wanaojihusisha wanajijua). Acheni jamani kama hamu-uogopi uongozi, basi muogopeni MUNGU.

    Tatizo jingine ni watu kukaa kwenye madaraka ya juu katika taasisi za umma kwa muda mrefu kupita kiasi. Wengine wamekalia madaraka kuanzia miaka ya 60 kabla wengi wetu hatujazaliwa mpaka leo bado wapo. Je nafasi za wengine ziko wapi? Kuna watu ni ma-managing director wa mashirika ya umma (????) zaidi ya miaka 10-15 hata zaidi, ni kweli hatujawa na watu competent wa kuwapokea?

    Kuna matatizo mengine ambayo yanasababishwa na wachache hawa wenye tamaa, na ambayo yanaathiri wanachi wote, ni kama vile umeme, na mengineyo. Ufumbuzi wake ni kitendawili.
    Hivi sasa tuna-uongozi unaojituma sana wa Bw JK. Lakini yeye peke yake bila kupewa ushirikiana na watendaji wake na wananchi wote kwa ujumla ni vigumu mno kuleta mabadiliko yote yanayohitajika.

    Kwa hiyo matatizo kama vile umeme, yanaweza kuendelea kuwa sugu na wananchi kuendelea kukosa kabisa au kupata umeme wa mgao. Miaka inaenda. Wenye uwezo wanatumia majenereta. Wenzangu mimi ni mwendo wa mishumaa na vibatari.
    Nadhani tusiwalaumu wenzetu walioamua kuishi nje. Hawa watu hawaukani wala kuudhalilisha utaifa, kwa namna yoyote ile. Huko nje maisha huwa rahisi kama unakibali maalum kinachokuwezeka kuishi kwa uhalali.

    Wengi wa hawa watu wana-ndugu, familia na hata marafiki,ambao huwatumia misaada na wengine wana miradi hapa nyumbani ambayo kwa namna moja au nyingine, aidha inaingiza pesa za kigeni au inatoa ajira kwa wenzetu.

    Suala la uraia "dual citizenship" lilipotangazwa lijadiliwe ili kuwapa nafasi wenzetu wanaotaka kuchukua uraia wa nchi nyingine wakati huo-huo kuendelea kushikilia utanzania, baadhi ya watu walisema "haiwezekani hili lipitishwe kwa vile watu watakuwa wanakula huku na kule."

    Lakini kuna baadhi ya raia wa kigeni hapa nyumbani ambao ni raia wa nchi nyingine pia (mfano Canada,UK, na kwingineko) hawa hawaonekani kuwa wanakula huku na huku. Ila wamatumbi wanaojaribu kulihalalisha hili ndo wanaoonekana kula huku na huku.

    Nawaomba ndugu waliotoa maoni hapa juu na wengine wenye mawazo kama haya, tuwaache wenzetu walioamua kwenda kuishi ughaibuni, mbali na nyumbani, ng'ambo n.k. waendelee kutafuta maisha yao na kusaidi jamaa zao pamoja na nchi yetu kwa namna moja au nyingine.

    Kama na sisi tunataka basi tuende tukaishi huko nje. Kwa wale waliogeuza rushwa kuwa sehemu ya kipato chao halali, waache kuomba pia kupokea (rushwa ni jasho la wazalendo wenzetu), tuone aibu, tujaribu maisha halali hapa nyumbani na popote tunapoishi. Wale wanaosaini mikataba mibovu pia waache. Aliyekuajiri anakulipa mshahara, kama hautoshi mweleze, lakini unaposaini mikataba bila kujali unaangamiza nchi sasa na ni athari ambazo zitaendela kuathiri hata vizazi vyetu vijavyo.

    Watu walioko Greece HONGERA zenu. Nikijaaliwa hata mimi nitakuja huko.

    Mdau,
    Mkereketwa

    ReplyDelete
  16. Kwa wale mnaopayuka kwa kusema kwamba "ooooh siwezi kuukana u-bongo wangu,... kwani passport ya Tanzania ina matatizo gani,...nk"

    Nenda kajifunze tena tofauti ya "national" and "citizenship". To become a citizen of Greece does not necessarily make you a Greek national. You can be a citizen of one country yet a national of another. Thats why the white british people, for instance, who have acquired some African states citizenships are still British National, swear allegiance to their Queen, and that is where their first loyalty is.

    That is why, (if you remember) during Russian and Geogian war last year(or a year before that), Russia punished Georgia for mistreating Georgian citizens who were Russian Nationals.

    If you go into some museum in Scotland, you will see a potrait of Dr. David Livingston as one of the most "famous africans". Though Livingston may call himself a malawian citizen, he remained a british national.

    Africans who try to acquire foreign citizenships do not reject their nationality as some of you would love to suggest. Human being are supposed to be mobile, and we all understand that the mobility of Africans is very limited, and confined into their small territories. By having access to a greek passport, for instance; an individual will have a wide choice of where to live, and where and when to travel.

    The western world comprises of less than 20% of the world population, yet consumes 85% of the world economy. By restricting movement of people from the so called third world countries, they manage to control the flow of wealth from the west to some other parts of the world. Yet, because westerners can travel easily to the third world freely, then the flow of wealth from third world to the west is unrestricted.

    When Jan Van Riebeck decided to settle in the coast of cape town, he did not reject his dutch nationality,he kept speaking dutch, and he lived as a dutch, though he declared him self African.

    Africans, acheni roho mbaya and wake up. Roho mbaya only facilitates self destruction.

    ReplyDelete
  17. hivi watanzania tutaishi na kuwa wagumu kuelewa mpaka lini (mdau mkereketwa nafkir amemaliza)mana hajui nini mtu anakisema mfano leo zanzibar mwez wa ngap hakuna maji na umeme hiv wewe kwa mtu mwenye akil bado tu unadanganywadanganywa! mtu akishi mahali popote pale ili mrad anapata rizki yake kihalal na wala havunj sheria bas hilo linatosha sasa hiv kote ulaya na america wabongo wameerevuka sio wale wa zaman wa kuogopa kama ukifanya hiv itakuwa vile nyie subirin baada ya miaka kama 15-20 ijayo utaona kwa nin waliamua kuchukua uraia wa uk,america greece na kadhalika baadae mtu akiwa matawi oooh ana asili ya nyumban

    ReplyDelete
  18. mmatimbi ni vocabraly za misoup yaani maana yake ni mtz kwasabu wamatumbi moja ya kabila hapa bongo ktk ukanda wa pwani.

    ReplyDelete
  19. kuna tafauti kubwa baina ya raia, mwananchi na mkaazi wa nchi

    ReplyDelete
  20. Chamkaga, mkereketwa na wachangiaji wote naomba mumueelezea na kuelimisha vizuri juu ya mjadala huu,

    kwa kuongezea kama ilivyoelezwa awali, Tanzania lazima imtambue mtanzania popote aishipo hapa ulimwenguni, yote ni katika kuleta maendeleo ya mtanzania na tanzania kwa ujumla, kwa kuiangalia ktk kila nyanja za kifikra na mtazamo, DUAL CITIZENSHIP IS GOOD FOR EVERYONE, AND A WIN WIN SITUATION ON THE INDIVIDUAL AND THE COUNTRY AS A WHOLE.

    DO YOU KNOW THAT, FOR THE LAST 10YEARS PRIOR 1997, DIASPORA HAVE SURPASSED MINING REVENUE IN TANZANIA BY BILLIONS. I MEAN THEY SENT BACK HOME MORE MONEY TO RELATIVES, AND INVESTMENT TO REVIVE SPENDING, ECONOMY, AND MOST IMPORTANTLY PROVIDING JOBS. WHO CAN SAY THERE IS ANYTHING WRONG WITH THAT.

    I WILL POST THE FIGURE AND SOURCE ONCE, I HAVE THEM WITH ME, BUT THAT'S THE FACTS ANYWAY.

    DIASPORA FOR DUAL CITIZENSHIP.

    ReplyDelete
  21. Hivi kuomba passport ya Nchi nyingine ndio ume - UKANA UTANZANIA??

    Ina maaana kuwa MTANZANIA unachohitaji ni Passport ya Tanzania Tu??!!!

    Ndio maana tunazidi kuibiwa Tanzania na so called Tanzanians WENZETU..!!

    Network Engineer (NE)
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  22. Suali kwa wote, nina baba yangu na wadogo zangu wawili ambao maisha yao yote hawakusafiri nje ya nchi kwa maana hiyo hawana passport za nchi yeyote, je wao sio watanzania? hivi ni lazima uwe na passport ya nchi kuwa mwananchi? kuna watu wengi tanzania hawana passport jee hawa pia tutasema wameukata utanzania wao?

    ReplyDelete
  23. Mi naona ni ushamba fulani hivi kushbikia uraia wa nchi nyingine.. eti Bongo umeme hakuna ahahahaha Halafu kuna tabia ya watu walioko Ulaya kudhani kuwa walioko nyumbani basi ndio wanan tabu na kwamba wao ndio wameendelea . manapoteza muda Ulaya huku wenzenu watu wanasonga mbele kuboresha maisha na ULAYA tunakuja likizo kutembea na kurudi nyie endeleeni kubeba boxi hadi uzeeni na watoto wenu sijui mnawaambia mnafanya kazi gani wakiwauliza? Pia kutokanan na kudharauliwa baada ya muda fulani kunakuwa na madhara makubwa kwenye level yenu ya Self esteem na ndio mana mnafikia kujikana wenyewe.. jamaa wa Ugiriki wanawacheka tu .. mananke mnashangilia kuwa wao yaani kuwa wagiriki ... lazima mdharauliwe kwa kuwa mmeanza wenyewe kujidharau. na future ya watoto wenu baada ya nyie kufariki mmefikiria? nini nafasi yao kwenye jamii kama hizo? Acheni ushamba

    ReplyDelete
  24. Kukaa nje si kuwa na maendeleo hahahaaaaa....
    Kasumba ya watu walio nje kuona wenzao wa tz wanashida

    ReplyDelete
  25. umekuja li ulaya kutembea lin wewe?we kaa ukijua usifananishe dunia ya kwanza na ya tatu

    ReplyDelete
  26. SIZITAKI MBICHI HIZI !!!! TANZANIA HAKUNA KITU HATA KAZI ZA KUBEBA BOX HAKUNA......MIMI NATAMANI KUWA RAIA WA RWANDA......

    ReplyDelete
  27. Kwa kuwa kuna midomo hapa ambayo haielewi sheria, ngoja niwasaidie.

    Ugiriki ipo katika umoja wa nchi za Ulaya (EU). kwa hivyo, ukipata uraia wao, unaweza kuishi kokote katika nchi za umoja huo. Raia wa EU anapata elimu ya bure katika baadhi za nchi ambazo elimu ni bure kama Sweden na kadhalika.

    Wadau wanaosema kuwa maisha ya nchi za kitajiri ni mbaya kuliko maisha ya Bongo aidha hana elimu ya dunia an uchumi au ana matatizo ya akili.

    Sio wote tunaoishi nje ya nchi tunataabika kama vile sio wote wanaoishi Bongo wana shida zaidi ya umeme, maji safi, elimu bora, matibabu bora na usalama. Mimi Mtanzania mpaka kufa lakini sijatumia pasi yetu miaka 20 sasa kutokana na matatizo ya kupata viza. Sina imani na serikali ya Tanzania, naona watu wa hali ya chini wanazidi kuonewa. Sitaki familia yangu kuishi katika mazingira haya.

    ReplyDelete
  28. UKITAKA KUJUA KAMA GREECE NI BABKUBWA KULIKO KIWANJA CHOCHOTE NJOO UUZE MOJA MOJA KUDADADEKI MIEZI6 TU TUSU,NIJE UK NIBEBE BOX MPAKA NGUVU ZA KIUME ZINIISHIE HOSHI.....GREEK KWA WAJANJA NI KUFINYA TU HAHAHAHHAHAHAHAHAHA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...