Ankal Issa Michuzi,
Wiki hii nilipata fursa ya kupita huku na kule ndani ya kampasi ya pale juu Mlimani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD a.ka UDSM). Kwa kweli nimeamini kuwa hiki ni chuo kikuu na kikongwe ndani ya bongo.

Taswira ya kwanza kukutana nayo ni ile hali ya hewa tulivu na mandhari ya kijani kufuatia mvua zinazonyesha hivi sasa inapendeza kweli. Vijana wanafanya makamuzi siyo kama enzi zile. Jengo la Nkrumah ni maarufu kwa wengi waliopata kupita mahala hapa.

Ukongwe wa Chuo hiki unathibitika kutokana na nondo nilizozikuta humu ndani kwa mfano Gazeti hili la Tanganyika Standard la Mwaka 1953 limo ndani ya nyumba. Ankal hapo hujazaliwa bado


Ndani ya Maktaba kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wadau wanafatilia kinoma kile kinachoendelea kupitia magazeti. Waandishi hapa wana kazi ya ziada kutoa habari za kina zilizofanyiwa utafiti wa kutosha na zinazo zingatia maadili ya uandishi, hiyo ni changamoto
kwenu.

Makamuzi ya vijana hawa yanakwenda na wakati, tekinolojia ya kisasa inatumika kwa sana tu.

Kuna msemo wa kizungu usemao 'charity begins at home', desturi hii nimeikuta pale Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya kila mwaka kuwa na siku moja ya kutoa msaada kwa vituo vy akulelea watoto yatima na walio katika mazingira magumu, safari hii wamekusanya michango ya bidhaa mbalimbali vikiwamo vyakula, sabuni na mafuta ya kupikia kwa ajili ya msaada kwa wakinamama na watoto waliolazwa katika Taasisi ya Saratani, Ocean Road, jijini Dar es Salaam. Pichani ni Mkuu wa Shule ya Biashara Dr. Marcelina Chijoriga akiongoza
wafanyakazi wengine wa shule hiyo kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya wagonjwa wa saratani waliolazwa katika taasisi hiyo.
Shughuli ya kutoa msaada iliendana na maadhimisho ya siku ya familia ambapo wafanyakazi na familia zao hushiriki michezo mbalimbali na kupata burudani kwa pamoja na hatimaye kupongezana kwa zawadi. Hafla hii ya siku ya familia ya Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanyika katika hoteli ya Kunduchi, Dar es Salaam.
Picha na habari na mdau wa mlimani, Ramadhani Kitwana







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Asante sana kwa hii makala. Sikujaaliwa kula nondo UD lakini nimepita mara nyingi na nakubaliana kabisa na wewe kuwa kuna mandhari nzuri sana ya kusoma na kuishi. Muundo mzima wa chuo kikuu cha Dar unadhihirisha uwezo mkubwa wa kutoa huduma za kitaaluma na utafiti - japo ziwe hazijafikia full potential yake. Naamini UD sasa inahitaji kupanuka kwa kuongeza kampasi nyingine Dar na maeneo ya karibu. Kama ningekuwa na uwezo, ningevigeuza vyuo vya IFM na DIT kuwa kampasi mbili kubwa za biashara na utawala (IFM) na Uhandisi na Teknolojia (DIT). Veta? Sijui inakwendaje!

    ReplyDelete
  2. suala la kusoma kwa mwanafunzi wa ud kipind kama iki wala huwa halishangazi...pale huwa wanatambaa na wiki na hela mfukoni!..sasa shule imekaba na bum wamefulia ni mwendo pasi ndefu a.k.a Lampard...hayo magazet ndo nimejionea hapa maana chuo kile WANAVOKABA na TUNAVOZIMA MOTO ukipoteza mda Sap zinakuhusu!!otheryz ungeenda pia mabwenini na Lecturerooms ushangaze umma!!Asante
    Mdau
    Graduate udsm
    Bsc in Telecomms Eng 09"

    ReplyDelete
  3. Kaka huo msemo ni origin ya Mother Teresa of Calcuta, ndiye alisema "charity begins at home"

    ReplyDelete
  4. Mdau umenikumbusha mbali sana, mzee punch and all that stuff.

    Do they still have those good monkeys?

    Those jamaa walikuwa wanapenda sana kukutoa silesi za mikate asubuhi tulipokuwa tunapata breakfast pale Manzese.

    When back I must visit that place!!

    ReplyDelete
  5. ndugu asante kwa kuifagilia UDSM. huwa sitoki ki-anonymas, lakini kwa leo mtanisamehe kwa sababu nitakazozieleza hapa chini.

    UDSM ni kama mtu anayefagia halafu uchafu anautupa ndani. wageni mkija mtaona pasafi. mbali na mambo mengine, UDSM ni wakiritimba (pengine wachovu)kwa supervision ya dissertation. kuchukua miezi 40 kwa masters ni jambo la kawaida. hiyo ndio sababu inayonifanya nitoke ki-anonimasi kwani dissertation ya kwangu ipo mikononi mwao, ilhali masters nimeanza 2007.

    UDSM inaelezwa vema na methali ya kiswahili 'Uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha......'

    ReplyDelete
  6. ASANTE SANA UKIPITA SIKU NYINGINE MPE HI PROF NINATUBU MATHIAS LEMA, DR NYAORO NA PROF BARTON MWAMILA UJUMBE ............................ ASANTE SANA

    ReplyDelete
  7. MDAU JAN 11, 11:10:00AM - POLE NDUGU YANGU.

    MASTERS DISSERTATION 40 MONTHS?? IS THAT 1ST SUBMISSION OR RESUBMISSIONS FOR SOME REASONS??

    SOUNDS RIDICULOUS.

    ReplyDelete
  8. jamani kuna alimfahamu mdau wa pili alichosema? au ndio lugha ya wasomi?

    ReplyDelete
  9. Hekima Ni Uhuru.

    Kwa watu waliohitimu hiki chuo tukazane tukirudishie hadhi yake.
    HEKIMA NI UHURU

    ReplyDelete
  10. hao wenye computer hawasomi wala nini, wa kwanza kama yuko facebook. na wale wengine wanasikiliza nini ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...