Na Mwandishi Maalum
Umoja wa Mataifa - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema ,amepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kufariki kwa aliyewahi kuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchini Sierra Leone, Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago.
Ban Ki Moon ameyasema hayo katika salamu zake za rambirambi ambazo amemtumia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe kufuatia kifo cha Balozi Mstaafu Daudi Mwakawago.
Katika salamu zake , Katibu Mkuu , amemuelezea Balozi Mwakawago kama mtumishi na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa sana katika mchakato wa kutafuta maridhiano nchini Sierra Leone.
Aidha Ban Ki Moon anasema, Balozi Mwakawago wakati wa uhai wake aliyatekeleza majukumu yake kwa umakini na uhodari mkubwa. Na kwamba aliitumikia nchi yake Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuia ya Kimataifa kwa heshima kubwa.
“Wakati tunapotafakari utumishi wa kutukuka wa marehemu Balozi Daudi Mwakawago kwa nchi yake na kwa Jumuia ya Kimataifa , tuna kila sababu ya kuwa na shukrani, si kwaajili ya yale aliyoifanyika nchi yake lakini pia kwa aliyoufanyia Umoja wa Mataifa. Kuondoka kwake kumeacha pengo kwa familia yake na halikadhalika kwa wale wote waliomfahamu. Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Familia ya Marehemu Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago”.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...